Baraza la Maaskofu Katoliki la Jamhuri ya Dominica. Baraza la Maaskofu Katoliki la Jamhuri ya Dominica. 

Dominica:Ujumbe wa Noeli na 2023:Askofu Mkuu Breton,kitovu cha Noeli ni Kristo

Katika Ujumbe wa Siku Kuu ya Noeli na Mwaka Mpya 2023 wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Santiago de los Caballeros,Jamhuri ya Dominica amebainisha kuwa bado kuna watu ambao kama wachungaji wanyenyekevu wa Betlehemu wanafurahi kiroho kwa ajili ya mtoto anayezaliwa katika umaskini wa holini.Kwa 2023 raia wote waweze kutambua kazi ya kujitolea ya jeshi na polisi kwa faida ya nchi.

Na Angella Rwezaula: – Vatican.

Tunateseka na  upepo wa nguvu sana unaotafuta kuharibu roho ya Noeli. Na zaidi pepo hizo mahali ambapo Noeli karibu haitajwi kwa jina kwa sababu ina manukato ya Kristo. Kwa sasa wanasema  siku kuu njema” ambayo inaweza kuwa kila kitu. Katika tafakari hiyo Askofu Mkuu Freddy Breton, wa Jimbo Kuu la los Caballeros, na Rais wa Baraza la maaskofu wa Jamhuri ya Dominica alifungua ujumbe wake wa matashi mema ya Noeli 2022 na mwaka mpya 2023. Askofu Mkuu katika ujumbe wake alizingatia zaidi kuwa roho ya Noeli haijapotea, hata ikiwa mzunguko wa biashara unafanya kelele zaidi na kufurahia  ubora wa habari. 

Dumisheni thamani za kweli za watu wa Jamhuri ya Dominica

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Breton amebainisha kuwa pamoja na hayo yote “bado kuna watu ambao kama wachungaji wanyenyekevu wa Betlehemu wanafurahi kiroho kwa ajili ya mtoto anayezaliwa  katika umaskini wa holini. Kwa kusukumwa na zawadi hiyo, wanamshukuru Mungu, wanasheherekea na familia zao na wanakwenda kusaidia wengine. Hiyo ndiyo Noeli ya kweli na wanaelezea hata kwa kuwakumbuka wale ambao wako mbali na ardhi walizozaliwa na kutafuta kukutana na ndugu wapendwa, kwa kusukumwa na shauku ya kushirikishana. Askofu Mkuu Breton kwa maana hiyo aliwaalika waamini kudumisha thamani za kweli za watu wa Jamhuri ya Dominica ya roho ya Noeli ya kweli ambayo ndiyo iwe kitovu.

Matashi mema ya 2023:Elimu,uaminifu kujitolea kwa polisi na jeshi

Matashi yake Askofu Mkuu Breton kwa ajili ya mwaka mpya 2023 kwa hiyo katika ujumbe huo alisisitiza  baadhi ya mapendeleo ya dhati. Kwanza kabisa ni matumaini kuwa elimu iweze kuwa dhabiti kwa ngazi zote, kwa ajili ya kuwa na usimamizi mzuri wa fedha zinazo kwenda kwa lengo hilo. Kipaumbele kipewe kulinda hadhi  ya mtu binadamu na uminifu uweze kushamiri kama ubora wa juu, kwa wafanyakazi wa umma na katika maisha ya faragha hasa kwa vijana. Katika mwaka mpya 2023, raia wote wanaweza kutambua kazi ya kujitolea ya jeshi na polisi kwa faida ya nchi, na mamlaka zenye uwezo hatimaye zinaweza kutokomeza vuguvugu baya la ufisadi ambalo huathiri sehemu ya Jumuiya hiyo na vile vile viwango vingine vya ngazi ya kijamii.

Wagombe waoneshe ukomavu wa kuunda jamhuri ya Dominika

Zaidi ya hayo, Askofu Mkuu anatumaini kwamba, hakutakuwa na haja ya kuwarejesha watu makwao wa eneo la Dominica, na ikibidi, watatekelezwa kwa uzingatiaji wa sheria na kwa heshima kamili wa hadhi ya binadamu. Matakwa ya mwisho kwa mwaka 2023 unaoanza, ambao utakuwa mwaka kabla ya uchaguzi, yanahusu vyama vya siasa na wananchi. Askofu Mkuu anaamini kwamba “wanaoneshe ukomavu wa kutosha katika michakato na matendo ya maisha ya kidemokrasia, na daima na zaidi ya yote watafute mema ya nchi yao, yaani, wanaume na wanawake wote wanaounda Jamhuri ya Dominica. Mungu awajaalie Noeli yenye baraka na mwaka mpya uliojaa hekima, ndiyo yamekuwa  matashi yake mema ya  mwisho.

Pamoja na kufurahia utulivu,bado kuna pengo kati ya maskini na matajiri

Katika miaka ya hivi karibuni, Jamhuri ya Dominica imefurahia utulivu fulani wa kisiasa ambao umeiruhusu kuingia katika mikataba ya kimataifa na kufaidika na ukuaji wa uchumi kutokana na kilimo, ujenzi, biashara na utalii. Hata hivyo, pengo kati ya maskini na matajiri bado ni kubwa, wasiwasi kuhusu hali ya wahamiaji wa Haiti ambao wanafanya kazi katika mashamba ya miwa na wanaishi kwa sehemu kubwa katika mazingira yasiyo ya kibinadamu. Miongoni mwa matatizo makuu ya kitaifa yanayopaswa kutatuliwa, ambayo mara nyingi hutajwa na Maaskofu katika hotuba zao, ni janga la rushwa, ukosefu wa uwazi na uaminifu, ambao pia hufikia nyadhifa za juu katika siasa na jeshi.

Ujumbe wa Noeli 2022 wa Jamh ya Dominica
16 December 2022, 17:54