Tafuta

Jarida la "Donne Chiesa Mondo", ambalo linahusu wanawake Kanisa Ulimwenguni  mwezi Desemba linajikita kutazama "Maria Mama wa Yesu". Jarida la "Donne Chiesa Mondo", ambalo linahusu wanawake Kanisa Ulimwenguni mwezi Desemba linajikita kutazama "Maria Mama wa Yesu". 

“Donne Chiesa Mondo”:Desemba ni Mwezi unaotazama Maria Mama wa Yesu!

Katika fursa ya siku kuu za mwezi Desemba Jarida la “Donne Chiesa Mondo”,linajikita kutazama mada ya Maria Mama wa Yesu.Ni wanawake wa dini mbali mbali wenye taaluma katika masuala ya kibiblia ambao wanatoa maoni yao,chambuzi,maombi na mapendekezo kuhusu Bikira Maria Mama wa Mungu katika fumbo la Kristo na la Kanisa.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Katika mwezi ambao unajikuta katikati siku kuu kubwa kuanzia na ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili hadi Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, jarida la Donne Chiesa Mondo, yaani Wanawake wa Kanisa Ulimwenguni ambalo kila mwezi kuna makala katika Gazeti la Osservatore Romano, kwa kuongozwa na mhariri wa jarida  la  wanawake Bi  Rita Pinci, kwa mwezi Desemba mada yao inamulika mwanamke mashuhuri sana wa Kanisa ambaye ni Maria, Mama wa Yesu, kwa kukaribisha tathimini, uchambuzi, maombi, maoni na mapendekezo kutoka kwa wanawake ambao kwa imani, masomo, maslahi ya kihistoria na kiutamaduni, ibada na wakati mwingine kwa sababu hizi zote huwekwa pamoja, wamechukua nafasi kubwa kwa miaka hii  kufafanua sura hiyo.  Wataalimungu, wasomi, waamini wa dini mbalimbali, tamaduni na mila, huhuisha mjadala wa kina na ulio wazi, makabiliano huru na yenye kuzaa matunda.

Mafunzo kuhusu Maria Mama wa Mungu

Mtaalamu  wa mafunzo kuhusu Maria (Mariology) Bi Cettina Militello alindika kuhusu Maria Theotokos, yaani Maria Mama wa Mungu na katika hitimisho lake akanukuu Hati ya Mtaguso wa II wa Vatican wa Lumen gentium, yaani Mwanga wa Mataifa na sura yake ya VIII, yenye kichwa: “Bikira Maria Mama wa Mungu katika fumbo la Kristo na la Kanisa”. Katika maandiko yake alibainisha kwamba: “Tunapata ndani yake maono ya usawa ya Maria, kamwe si muungu wa kike au kiumbe katikati ya mwanadamu na Mungu, lakini dada yetu katika ugumu wa jitihada za kila siku za kuamini, mwenzetu katika 'hija ya imani', aliyebarikiwa kwa sababu yeye aliamini katika utimilifu wa maneno ya Bwana”.

Wataalamu mbali mbali kuhusu Maria

Msomi wa kibiblia Bi Marinella Perroni kwa maana hiyo yeye amekazia juu ya kanuni ya Maria kwa Mtume Petro; mtaalimungu Simona Segoloni, yeye anajikita  juu ya mafundisho ya dogma; Mercedes Navarro Porto, ambaye ni Mwalimu wa Mafundisho ya Agano la Kale, amejikita  kutazama nyuso za kibiblia. Baadaye kuna Amy-Jill Levine anayejikita kufafanua Maria katika mtazamo wa Kiyahudi. Vile vile kuna Mprotestanti akiwa na msimamizi wa meza ya Wavaldesi, Bi Alessandra Trotta; na Mwislamu Shahrzad Houshmand Zadeh. Kwa mujibu wa maelezo ya tahariri ya jarida hilo anaandika kwamba, kwa upande wa Papa Francisko, anamwazia Maria kama vile msichana, mwanamke, mama 'wa kawaida'. Ni kawaida ya kuishi kati ya watu na kama watu”, anahitimisha.

Maria Theotokos
02 December 2022, 11:25