Ikame ni moja ya madhara makubwa yanayokumba nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ikame ni moja ya madhara makubwa yanayokumba nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

Kampeni2023 kuhusu usalama wa chakula,Cameroon,Chad &Ivory Coast!

Mtu hataishi kwa mkate peke yake:chakula kwa ajili ya Afrika ndiyo kauli mbiu inayoongoza Kampeni 2023 ya Shirika wa Wamisionari wa Pime ambayo imezinduliwa katika lengo la kukidhi haja ya uhaba wa chakula, kwa wale ambao hawana uhakikisho,mara kwa mara na wa kwa ujumla,hupatikanaji wa maji na chakula kwa ajili ya maisha ya watu hasa kwa nchi ya:Cameroon,Chad na Ivory Coast.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Baada ya mgogoro wa kiafya na wa vyakula ulimwengu mzima unaokabiliwa na bado kupambana nao uliotokana na janga la Uviko-19, ni kujikita leo hii kuishi kipindi kigumu sana kwa sababu ya vita kati ya Urussi na Ukraine. Matokeo ya mgogoro huu kiukweli yanajidhihirisha duniani kote kwa shinikizo kubwa katika masoko ya ndani na juu ya bei ya bidhaa za kilimo na mahitaji msingi  kama vile nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, tayari zinakabiliwa na athari za hali hii mbaya zaidi kuliko wakati mwingine wowote ambayo inahatarisha rekodi mpya za watu wanaoishi katika hali ya uhaba wa chakula, yaani, ambao hawana uhakikisho, mara kwa mara na wa kwa ujumla, upatikanaji wa maji na chakula kwa ajili ya maisha ya watu, ambayo wakati mwingine hakuna hali nzuri vya kutosha vya vifaa vya usafi.

Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe, katika fursa ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji juu ya Upotevu na Upotevu wa Chakula mnamo tarehe 29 Septemba 2022, alisisitiza umuhimu wa kuingilia kati kwa ajili ya wale ambao hawana chakula cha kutosha ambapo inatathiminiwa karibu theluthi moja ya idadi ya watu duniani kwamba “ni tatizo ambalo hatuwezi kumudu kulipuuza [...]: ni muhimu kujibu ipasavyo kilio cha kuhuzunisha cha wenye njaa wanaodai haki”. Kutokana na hali hii ya dharura, pia ilihisiwa katika baadhi ya Utume wa Wamisionari wa  PIME kama vile  za Cameroon, Chad na Ivory Coast, wazo la kukuza Kampeni mpya ya Kituo chao  huko Milano kwa mwaka wa 2023 juu ya mada ya usalama wa chakula lilizaliwa. Mpango huo pia unataka kuwa ishara ya mshikamano na matumaini katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya uwepo wa wamisionari wa Taasisi hiyo nchini Ivory Coast.

Ujumbe ambao Kituo cha Kimisionari  PIME kingependa kuwasilisha mwaka huu ni wa kufikia ujumbe huo kwa upanda wake wakiongozwa na kauli mbiu: “Mtu hataishi kwa mkate tu”  kwamba ndiyo kiukweli jibu la Yesu kwa mwaliko wa shetani wa kubadilisha mawe ya jangwani kuwa mkate, ili kushibisha njaa yao baada ya siku 40 mchana na usiku 40 za kufunga. Na anaongeza: “Lakini katika kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu”. Mada iliyochaguliwa kwa ajili ya Kampeni mpya kwa hiyo inalenga kuibua mada na lengo linalojiwekea: kukuza usalama wa chakula nchini Cameroon, Chad na Ivory Coast. “Si mkate tu”, hata hivyo, pia inarejeea hitaji la mwanadamu kulima na kuhifadhi sio tu lishe ya kimwili, lakini pia kuona baadhi ya haki za kimsingi zikitoshelezwa kama vile elimu na huduma za afya na kupata mipango ya kuzuia na uhamasishaji . Kwa hakika, kulisha uzoefu chanya na kielimu husaidia kukuza masuluhisho endelevu, ya kiikolojia, asilia na ya gharama nafuu ili kuboresha usalama wa chakula katika jamii ambako utume PIME unaendelea kuwapo

Kampeni ya 2023  shukrani kwa Mfuko wa S146  wamebainisha kwamba  itawasaidia wamisionari waliopo Kamerun, Chad na Ivory Coast kuhamasisha hali tofauti, lakini zote zinahusishwa na suala la usalama wa chakula: elimu na mafunzo katika mazoea sahihi ya chakula; kuongeza uelewa kwa akina mama na familia juu ya sifa za lishe ya vyakula; maendeleo ya kilimo na kilimo cha bidhaa mpya endogenous na virutubisho; kukuza fursa mpya za kuongeza mapato; usambazaji wa maji ya kunywa na programu za kuongeza uelewa wa viwango sahihi vya usafi wa mazingira; programu za afya za kupunguza, kuzuia na kutibu utapiamlo na kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

Kampeni iitwayo “Si mkate pekee yake. Kulisha nchini Kamerun, Chad na Ivory Coast” itahusisha, nchini Italia, sekta zote za Kituo cha PIME huko Milano, Italia kutoka  mawasiliano hadi kukuza matukio, kutoka katika uingiliaji wa elimu hadi majumba ya Makumbusho ya Watu na Tamaduni, kuanzia  uhuishaji wa wamisionari hadi kufikia Maktaba na  shambani, vyote hivyo vitahusisha wamisionari mbalimbali wanaofanya shughuli kadhaa. Asilimia 70 ya michango itakayotolewa itaelekezwa kwa mipango ya maendeleo endelevu itakayotekelezwa katika nchi tatu zinazohusika. Asilimia 30 itakayobaki, hata hivyo, itafadhili uendelezaji wa mipango na shughuli mbalimbali za mawasiliano, kiutamaduni, kielimu na uhuishaji wa kimisionari. Kwa maana huyo wanaomba kwa kila mmoja mwenye mapenzi mema kusaidia iwezekanavyo kamoeni hiyo: “Saidia Kampeni S146 - Sio kwa ajili ya  mkate pekee. Kulisha nchini Cameroon, Chad na Ivory Coast.”

Saidia Wamisionari wa Pime katika kampeni 2023 ili kusaidia nchini Cameroon,chad na Ivory Coast
15 December 2022, 15:17