KardinaliKevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha KardinaliKevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha 

Matendo Katoliki.Shauku kwa ubindamu uliopyaishwa katika Kristo

Katika tukio la Mkutano wa siku mbili kupitia mtandaoni na moja ka moja katika Kituo cha Domus Mariae,Roma lilikuwa ni Jukwaa la Kimatiifa la Chama cha Matendo Katoliki kinacho kusanya vyama shirikishi ulimwenguni kote.Kardinali Kevin Farrell,alisema'katika ulimwengu wetu usio na dini,si jambo la kawaida hata kidogo kwa ahadi za kidini kuhamasisha shauku hivyo ni ujasiri.'

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Siku mbili ya tarehe 26 na 27 Novemba 2022,  lilifanyika Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki, chombo kinachokusanya na kuratibu vyama vya Matendo ya Kikatoliki duniani kote, kwa kuadhimisha Mkutano wake wa nane ukitanguliwa na mkutano wa kimataifa. “Hatua Katoliki. Shauku kwa ajili ya ubinadamu uliopyaishwa  katika Kristo" ndiyo ilikuwa mada kuu katikati ya hafla hiyo ambayo ilifanyika kwa muda  masaa mawili wa alasiri mtandaoni na ana kwa ana, kwenye ukumbi wa Armida Barelli, wa Domus Mariae jijini  Roma. Shughuli hizo zilifunguliwa  mchana saa 8 kamili tarehe 26 na Rafael Ángel Corso, ambaye kwa sasa ni Mratibu wa FIAC, na Giuseppe Notarstefano, Rais wa kitaifa wa Chama cha Matendo katoliki Italia.  Katika ufunguzi, wao kwanza walisikiliza ujumbe wa video na salamu kutoka kwa Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha.  Mwenyekiti huyo aliwasalimu waliokuwepo na waliounganishwa mtandaoni, akikumbuka kwamba wao walichagua  mada ya mkutano wao “Hatua Katoliki. Shauku kwa ajili ya ubinadamu uliopyaishwa  katika Kristo.

Si jambo rahisi kuhamaisha shauku

Kwa mujibu wake alibainisha kwamba Chaguo la kutumia neno shauku kufafanua utume wa Chama cha Matendo katoliki ni la ujasiri. Katika ulimwengu wetu usio na dini, si jambo la kawaida hata kidogo kwa ahadi za kidini ya kuhamasisha shauku. Ikiwa tunafikiria juu yake, leo, hii  kwa idadi kubwa ya watu, mambo ambayo huamsha shauku ni yale yote yanayohusiana na mtu binafsi: kusafiri, sanaa, michezo, uwezekano wa kufanya kazi na, kwa hivyo, kuwa na ustawi mkubwa zaidi, kuwa na mahusiano ya kiuchumi, kihisia na kimapenzi. Haya ni mambo ambayo huchochea shauku fulani kwa sababu kwa namna fulani hulisha umimi. Kardinali alisema leo hii tunashuhudia kukimbia kuelekea ubinafsi. Inaonekana kwamba tunatafuta kile tu ambacho ni cha nyanja finyu ya kibinafsi na kile kinachohusiana na wakati huu, hadi sasa, kwa kitu ambacho hutoa kuridhika sasa tu na kwa ajili yangu. Kwa upande mwingine, kile kinachojenga mahusiano, na ambacho kinaacha alama kwa jamii, na hakiangalii mambo ya hapa na pale, bali kinalenga kuweka misingi ya maisha bora ya baadaye, kwetu na kwa wengine, kwa bahati mbaya  kinaamsha maslahi madogo sana.

Kuhisi kama wajumbe wa upendo wa Mungu

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha  aliendelea huku, akiwatia moyo washiriki hao kwamba katika uso wa haya yote, wanaweza kuelewa vizuri kwamba ni ujasiri na dhidi ya usasa kuzungumza juu ya shauku na zaidi ya yote, kuunganisha shauku hiyo na ubinadamu, kwa kupyaishwa katika Kristo, na hivyo kwamba  hakuna kitu kizuri zaidi kuliko kujiweka katika utumishi wa Bwana na kazi yake ya kubadilisha na kuokoa watu. Kwa maana hiyo kujisikia kama wajumbe wa upendo wa Mungu, vyombo vya neema yake kufikia kila moyo, kugusa kila roho, kufanya upya kila uwepo, ndiyo kweli inaweza kuwaamsha watu wengi, hasa vijana, kutoka katika sintofahamu za  kutokujali. Tunapotambua kwamba sisi Wakristo tumechaguliwa, tumeitwa na Bwana kwa ajili ya utume wa ulimwengu wote, na kwamba imani yetu ni hazina ya hekima, furaha na upatanisho ambayo tunaweza kushiriki na wengine, je tunawezaje kutohisi shauku ya kufanywa upya kuwa wanadamu katika Kristo”? alihitimisha.

Uchaguzi wa Katibu Mkuu 2023-2026

Katika hitimisho la Mkutano huo wa VIII, nchi Wanachama wa chama hiki kwa uratibu wa Vyama vya matendo Kikatoliki ulimwenguni, walichagua Katibu Mkuu ambaye ataongoza Shughuli za Fiac kwa miaka mitatu kuanzia 2023-2026.  Kwa wahusika wapya wa Fiac walitumiwa ujumbe na matashi mema kutoka kwa Papa Francisko ambaye pia aliwasalimia washiriki wa Mkutano huo waliokuwa Roma kabla ya sala ya malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro Dominika tarehe 27 Novemba 2022.

Kardinali Farell
03 December 2022, 11:47