Tafuta

 Nembo ya  Mkutano wa Vijana wa Taize huko Rostock Nembo ya Mkutano wa Vijana wa Taize huko Rostock 

Mkutano wa Rostock:Mwanga wa Yesu hauzimiki kamwe

Hata mwanga unaowaka wa mishumaa michache usiku, una nguvu zaidi kuliko uovu na uharibifu wa vita. Ndugu Alois,ambaye ni mkuu wa jumuiya ya Taizé,alikumbusha hayo wakati wa mkutano wa maombi,Jumatano 28 Desemba jioni huko Rostock kwa vijana.Katika kutafakari,alizungumzia mambo muhimu ya sasa na kukazia ujumbe wa imani wenye tumaini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kristo anakuja ulimwenguni.Ndiyo  ujumbe wa Noeli ambao Ndugu Alois, ambaye ni Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya Taizw aliwaeleza mamia ya vijana ambao wamewasili hivi karibuni katika jiji la kaskazini mwa Ujerumani kuudhuria mkutano wa vijana Barani Ulaya ambao ni kama utamaduni sasa wa kila mwishoni mwa mwaka.  Ndugu Alois kwa maana hiyo alisema “Yesu ndiye nuru ya ulimwengu ambayo inatishwa na hata haionekani, lakini hata hivyo nuru yake haizimiki kamwe.

Mkutano wa Vijana wa Taize na ndugu wa Lvivi
Mkutano wa Vijana wa Taize na ndugu wa Lvivi

Kiongozi huyo aliweza kuelezea pia juu ya uhusiano kati ya Jumuiya ya Taizé na kaskazini-mashariki mwa Ujerumani kwamba umekuwepo tangu miaka ya 1960, na zaidi huyo mkuu wa  jumuiya hiyo ya Tazie ni mwenye  asili ya Ujerumani.Katika kuelezea alisema Ndugu wa Jumuiya ya  Taizé walijiunga na Jumuiya hiyo wengine kutoka hapo  katika Pazia la Chuma  ambalo lilikuwa  bado linagawanya Ulaya. Makanisa yalichukua jukumu kubwa katika kukomesha mgawanyiko huo wa Ulaya alisisitiza Ndugu Alois. Na baadaye vijana wengi kutoka Mecklenburg-Vorpommern walikwenda na kujiunga na Jumuiya Taizé.

Wakristo kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Shirikisho hata hivyo ni wachache katika jumuiya, lakini hawakuwa wamejitenga kamwe wenyewe. Badala yake, hali hiyo iliwahimiza kutafuta mazungumzo na kila mtu. Kwa hiyo hii inaonesha wazi kwamba ni upamoja tu unawezekana kukabiliana na changamoto zinazotukabili na kujenga jumuiya na jamii  ambayo uaminifu hujengwa, alisisitiza kiongozi huyo.  Hata hivyo kabla ya kuelekea njia kuelekea Rostock, awali  ya yote kiongozi huyo, alikuwa amekwenda Ukraine siku tano kabla ya Noeli na baadaye baadhi ya vijana wa Kiukreni  waliweza kufika Rostock katika mkutano huu.

Kwa hiyo Ndugu Alois  aliwambia jinsi ambavyo wanakaribishwa kwa moyo mkunjufu. Aidha alisema huko  Kiev walikuwa wameshirikishana nao maisha ya kila siku ya watu hawa wajasiri. Mara kwa mara, jioni au hata mchana, taa zinazimika katika vitongoji vyote. Lakini hii haiwazuii vijana kusali pamoja kwa kuwasha mishumaa yao. Huko Ukraine, kuna nyimbo nyingi za zamani za siku kuu ya Noeli.  Mkuu wa Jumuiya hiyo akiendelea na tafakari na aliwaomba wao wafute machozi machoni pao, kwa sababu Mwana wa Mungu amekuja kuokoa ulimwengu kwa upendo wake. Nuru inaangaza angani na kweli ndiyo Kristo alikuja ulimwenguni. Alikuja pia katika giza na usiku. Na katika giza kuu, mwanga wake tayari umeaangaza.  Kwa maana hiyo aliwashukuru vijana wa Ukraine kwa ujasiri wao na uvumilivu wao katika imani.

Katika tafakari hiyo alisema kuwa hata hivyo katika dunia ya leo hii kuna watu wengi waliovunjika moyo. Aliwafikiria wahamiaji aliokutana nao katika kisiwa cha Lampedusa wakati wa Noeli mwaka jana 2021.  Wengi wao walikuwa wamefika kisiwani baada ya kuvuka kwa hatari. Wengine waliokolewa kutoka kwa dhiki za baharini. Pia alisisitiza kuwa wasiwasahau watu wa Haiti, wanaokabili hali mbaya sana. Na zaidi kuwaombea watu wa Mashariki ya Kati. Hivi karibuni alibainisha jinsi alivyo zungumza na mtawa kutoka Latakia nchini Sria. Yeye na dada zake wanatunza watoto wa jirani zake na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya mustakabali wa nchi. Wanawake na wanaume hawa, vijana hawa na wakati mwingine hata watoto wamechagua tumaini mbele ya shida. Ndugu Alois kwa njia hiyo aliomba vijana hao kuwaombea jioni hiyo na kutoa shukrani kwa ushuhuda wa ujasiri wanaoutoa.

Mkutano wa Vijana ulioandaliwa na Jumuiya ya Kiekumene ya Taize huko  Rostock ulianza  tarehe 28 Desemba 2022 na utahitimishwa  tarehe Mosi Januari 2023, ambao unaudhuliwa  na maelfu ya vijana kutoka barani Ulaya. Wengi wa washiriki ni kati ya umri wa miaka 18 na 35. Hawa ni wenyeji wa miji na jumuiya katika eneo hilo na wanakaa na watu binafsi kwa muda wote wa mkutano. Lengo kuu la Mikutano ya Vijana ya Ulaya ni urafiki na uaminifu. Maombi ya pamoja katika sehemu tofauti za mapokezi na katika eneo la HanseMesse Rostock-Schmarl, mabadilishano kati ya wenyeji na wageni vijana, mikutano ya pande zote na kushiriki maisha yao husika yanafanya iwezekane kutajirisha na kuunda jumuiya mpya wakati wa siku za mkutano, kwa mujibu wa Taarifa za waandaaji ambao ni Jumuiya ya Kiekuemena ya Taizé.

30 December 2022, 12:54