Maaskofu Nchi ya Jamhuri ya Kati wanabainisha kuwa siku zote imekuwa nchi yenye ukarimu na mapokezi lakini watu waaogopa wageni kuchukua ardhi yao (Land grabbing). Maaskofu Nchi ya Jamhuri ya Kati wanabainisha kuwa siku zote imekuwa nchi yenye ukarimu na mapokezi lakini watu waaogopa wageni kuchukua ardhi yao (Land grabbing). 

Afrika ya Kati:Maaskofu waonesha hatarini ya kunyakuliwa ardhi na wageni!

Waafrika ya Kati wako katika hatari ya kuwa na wageni nyumbani kwao,ambapo Maaskofu wanasema ni vema kuwa na tahadhari ya kile kiitwacho:“land grabbing” yaani unyakuzi wa ardhi.” Nhci yao imekuwa na ukaribu wa wageni lakini “katika masuala mengi,hata hivyo,tunashuhudia leo hii kuna mbio halisi ya raia kutoka nchi nyingine za kanda hata kutoka sehemu nyingine za dunia wakinunua ardhi."

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Uhaba wa mafuta, kupanda kwa bei za mahitaji ya msingi na ukosefu wa usalama ambapo maeneo makubwa ya nchi wanaishi. Ndizo changamoto kuu zinazoikabili Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mujibu wa  Maaskofu mahalia  kama walivyobainisha katika maandishi  yao  yaliyotolewa mwishoni mwa mkutano wao uliofanyika kuanzia tarehe 10 hadi 15 Januari 2023 katika makao yao makuu mjini Bangui. Uchumi dhaifu wa Afrika ya Kati pia unakabiliwa na changamoto ya ziada, ya kile kiitwacho ‘Land grabbing’, yaani unyakuzi wa ardhi ya kilimo kutokana na mashirikia ya wageni walioingia humo lakini hata katika nchi nyingine nyingi za kiafrika na mabara mengine  ambazo sehemu kubwa za ardhi zimekuwa mikononi mwa mashirika ya kimataifa yanayotazama maslahi yao binafsi na si nchi hizo mahalia.

'Tunashuhudia mbio za ununuzi wa ardhi'

Kwa upande wa Maaskofu wa Afrika ya Kati katika maadiko yao wamebainisha kuwa “Jamhuri ya Afrika ya Kati siku zote imekuwa nchi yenye ukarimu na mapokezi. Kupinga aina zote za chuki dhidi ya wageni, ukarimu na ukaribishaji wageni zimeandikwa katika moyo wa imani yetu ya Kikristo na katika barua za dhahabu za  maadili ya mababu zetu”. Maaskofu wanaeleza kuwa lakini “katika masuala mengi, hata hivyo, tunashuhudia leo hii kuna mbio halisi ya raia kutoka nchi nyingine za kanda  hata kutoka sehemu nyingine za dunia wakinunua ardhi ...” Kwa hiyo lakini “Hatuna chochote dhidi ya kuingiza mtaji wa kigeni katika kiungo  dhaifu cha uchumi wa Afrika ya Kati, kwa sharti kwamba itatengeneza mali na kazi kwa mabinti na wana wa nchi hii”, wanasema Maaskofu ambao hata hivyo wanashutumu kwa jinsi  ambavyo “viwanja vikubwa vya kilimo kwa  hekta kadhaa na maeneo ya kimkakati, ya uchimbaji madini na misitu vinauzwa”.

Maaskofu walikutana na Rais wa Nchi 14 Januari 2023

Askofu  Nestor-Désiré Nongo Aziagbia, wa jimbo katoliki la Bossangoa na Rais wa Baraza la Maaskofu kwa maana hiyo anakaribisha mapitio ya sheria ya ardhi ambayo kwa sasa Waafrika ya Kati wanaogopa kuwa itakuwa mikononi mwa wageni katika nchi yao”. Wasiwasi huu uliwasilishwa na Askofu Mkuu Aziagbia mwenyewe kwa Rais Faustin Archange Touadéra, wakati wa mkutano kati ya Rais wa  Nchi na ujumbe kutoka Baraza la Maaskofu mnamo Jumamosi  tarehe 14  Januari 2023. Katika kuelezea shughuli za Kanisa Katoliki, Afrika ya Kati, Maaskofu walielezea  kwa Rais hofu ya wananchi juu ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na masuala ya barabara, elimu, afya, uhaba wa mafuta.

Rais Faustin Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alipotembea Vatican 5.3.2019
Rais Faustin Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alipotembea Vatican 5.3.2019

Ndugu msikilizaji na msomaji wa Vatican News, kwa uelewa zaidi, Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo FAO, katika Jukwaa kuhusu Maarifa ya Kilimo cha Familia, walieweza kueleza kidogo ni nini maana ya ‘Land Grabbing’ yaani unyakuzi wa adhi.  Kwa uhakika muhimu wa tafsiri zilizopo, ni kwamba unyakuzi wa ardhi ni suala zito sana linaloathiri mazingira, uchumi, ustawi wa jamii na haki za binadamu. Licha ya unyakuzi wa ardhi duniani kote, lakini hakuna ufafanuzi unaonasa suala hilo kikamilifu. Taarifa zaidi kuhusu unyakuzi wa ardhi zinapatikana kupitia mashirika ya kiraia, ikijumuisha mawazo ya jumla na ufafanuzi maalum. Mashirika ya kiraia kwa kawaida hujumuisha kuwa unyakuzi wa ardhi ni aina ya udhibiti na upataji wa rasilimali, na kwamba hii ni kwa ajili ya uchimbaji na kilimo pia katika maeneo mbali mbali. Pia wanakubali kwamba kuna ukosefu wa usawa wa mamlaka katika unyakuzi wa ardhi, huku mashirika tajiri au yanayounganishwa kisiasa yakitumia mamlaka hayo kwa gharama ya wengine, ambapo mara nyingi kwa angalau kuwa na usaidizi wa serikali yenyewe! Hatimaye, mashirika ya kiraia yanakubali kwamba unyakuzi wa ardhi una athari mbaya kwa jamii za wenyeji, lakini athari zake hazijabainishwa vizuri.

Maaskofu Afrika ya Kati
24 January 2023, 15:17