CEI:Ujumbe kuhusu kuchagua somo la dini katoliki mwaka 2023/24
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baraza la Maaskofu nchini Italia (CEI) limechapisha ujumbe wake katika matazamio ya uchaguzi wa kupendelea Mafundisho ya masomo ya dini Katoliki (IRC) kwa mwaka wa masomo 2023/24. Katika maelezo ya ujumbe huo unabainisha kwamba takwimu inayohusiana na mwaka wamasomo 2021/2022 umeleta picha halisi ya uthabitisho mkubwa, pamoja na ukuaji mdogo kwa ujumla wa wanafunzi wanaochagua kuhudhuria kipindi cha dini Katoliki (IRC) na wastani wa kitaifa sawa na asilimia 84.44% ya wanafunzi wanaotumia fursa hiyo. Kwa maana hiyo katika ujumbe wa Rais wa CEI uliolekezwa kwa wanafunzi na wazazi wao unabainisha kuwa: “Katika siku chache zijazo, tukiendelea na uandikishaji katika mwaka wa kwanza wa viwango mbalimbali vya shule, mtaombwa kuchagua kama manufaa na Maelekezo ya Mafundisho ya Dini katoliki (IRC). Hili ni chaguo muhimu, ambalo linakuwezesha kushiriki katika ujenzi wa njia ya elimu inayotolewa na shule. Kwa hakika, nafasi uliyo nayo mbele yako ni nafasi ya uhuru na wajibu, njia ya kuhisi hata zaidi njia yako ya ukuaji wa kibinadamu na kiutamaduni ambayo unachukua au kusindikizwa nayo”.
Kwa njia hiyo ujumbe huo unathibitisha kuwa hiyo ni kweli hasa kwa vijana wanaoanza shule ya sekondari, lakini pia inawahusu wanafunzi wote na wazazi wengine, ambao wote ni wahusika wakuu katika kuunda “Mkataba wa Kielimu” ambao ni wa Mafundisho Katoliki (IRC) nchini Italia. Kwa hakika, Serikali, katika mabaraza yake kuu na ya kimaeneo, Kanisa, shule binafsi, pamoja na walimu na wakuu, familia na wanafunzi wenyewe wanashiriki katika uwepo na sifa za mafundisho haya, kwa njia ya maamuzi ya kufahamu ambayo wao watakuwa “raia” kutoka nyumbani kwao na shuleni”. Pia kwa sababu hiyo Mafundisho ya dini Katoliki, (IRC) yanajumuisha uzoefu wa umuhimu mkubwa katika panorama ya kielimu, kama kielelezo cha “mkataba wa pamoja” kati ya mashirika tofauti na watu, mapatano yaliyofanywa kwa faida ya watoto na vijana na, kwa hivyo, kwa jumla katika jamii. Mkataba unaowaona sio waliokusudiwa tu, bali unaowahusisha awali ya yote kila mtu binafsi.
Rais wa Baraza la Maaskofu Italia katika ujumbe huo anaendelea kubainisha kwamba “Kuchagua ni kitenzi kinachoonesha ukomavu na maslahi. Ni kitenzi muhimu ili kuendelea kwenye njia ya maisha. Papa Francisko alikumbusha hayo alipozungumza na wanafunzi wa shule wakati wa ziara yake ya kitume nchini Bahrain kwamba: “Hakuna maisha bila changamoto za kukabiliana nazo. Na kila wakati, unakabiliwa na changamoto, kama ukiwa kwenye njia panda, lazima uchague, ujihusishe, uthubutu na uamue.” Lakini hiyo inahitaji mkakati mzuri kwani huwezi kukurupuka kujiboresha, kuishi tu kwa silika au papo hapo!”. Ili uweze kujifunza kuchagua, Papa aliongeza kwamba “tunahitaji kusafisha mitazamo yetu ya ndani, kujifunza kuhukumu hali, kufahamu umuhimu na kuufanyia kazi moyoni, ili tusibakie kutojali au kuonekana kutokuwa na subira kwa wengine, lakini kujibu na ndoto mpya ya udugu na urafiki wa kijamii ambayo sio tu kwa maneno”.
Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia kwa njia hiyo wanabainisha kwamba wana uhakika kwamba kutumia fursa zinazotolewa na kufundisha dini ya Kikatoliki shuleni kutasaidia kutembea katika mwelekeo uliooneshwa na Papa Francisko, pia shukrani kwa uwepo wa wale wataalamu waliohitimu na waelimishaji wa kweli ambao ni walimu wa Dini Katoliki (IRC), ambao Baraza la Maaskofu wanatanguliza shukrani za dhati. Kwa mawazo na hisia hizi, kwa hivyo, wanapyaisha mwaliko wao wa kutumia mafundisho ya dini ya katoliki, katika shule inayotazama ukuaji kamili wa mtu na kwa utamaduni unaozalisha mazungumzo na amani. Unahitimishwa ujumbe huo kutoka Baraza la Maaskofu Italia kwa ajili ya wanafunzi na wazazi nchini Italia kwenye uchaguzi mwema wa somo la Dini Katoliki kwa mwaka 2023/2024.