Tafuta

Picha ya Bikira Maria wa Guadalupe.Ulimwengu mzima utasali salamu Maria hadi tarehe 13 Machi wakati wa kumbu kumbu ya miaka 10 ya Upapa wa Francisko. Picha ya Bikira Maria wa Guadalupe.Ulimwengu mzima utasali salamu Maria hadi tarehe 13 Machi wakati wa kumbu kumbu ya miaka 10 ya Upapa wa Francisko.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ave Maria katika maadhimisho ya miaka 10 ya Upapa wa Francisko

Mpango huo uliozinduliwa na Sinodi ya Kidijitali mwezi mmoja kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu ambayo Papa ataadhimisha tarehe 13 Machi.

Vatican News.

Ramani ambayo ina mishumaa mingi inayowashwa ili kumwonesha ari ya Papa Francisko ya msaada unaotolewa kwake wa sala za waamini kutoka  ulimwenguni kote, kwa kuzingatia kumbukumbu ya miaka 10 ya upapa wake. Wazo la kuanzisha tukio la maombi  ya maadhimisho hayo kwa njia ya mitandao lilikuja kutoka katika  sehemu ya Sinodi ya Kidijitali ambayo ilizindua pendekezo kupitia kiunga ambacho kitakuwa hai hadi  mnamo  tarehe 13 Machi 2023 katika siku ya kumbukumbu hiyo ya upapa wake.

Maombi yetu kwa Papa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa inasomeka kuwa: “huduma ya Petro ni neema kubwa ambayo Yesu alitoa kwa Kanisa lake na lazima tuishukuru kila wakati. Kwa hiyo, maombi yetu yanapaswa kuwa zawadi bora zaidi, ili Mungu amsaidie katika huduma yule ambaye amemchagua kwa ajili ya huduma hiyo, kwa sababu juu ya mwamba huu anajenga Kanisa lake kwa muda na historia”. 

Mishumaa midogo

Kwa yeyote anayetaka kushirikisha mpango huo atapata kutoka katika  tovuti mwaliko wa kusali Salamu Mariamu mmoja au zaidi na mwisho tutamtumia Baba Mtakatifu ramani hiyo iliyojaa 'mishumaa midogo'  inawakilisha 'Salamu Maria' wanayo mwombea, huku wakimshukuru Mungu kwa huruma zake.”

Sinodi ya kidijitali

Sinodi ya Kidijitali ni mtandao wa wamisionari wa mtandaoni ambao wameitikia wito wa Papa wa kushiriki katika safari ya sinodi kwa kufanya mazungumzo na wale wanaoishi katika bara la kidijitali na kuleta uzoefu wao wa Kikristo. Huo ni mpango unaosindikizwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Maandalizi ya kumbu kumbu ya miaka 10 ya Upapa wa Francisko
14 February 2023, 16:25