Kardinali wa Ethiopia:viongozi wa Sudan Kusini wasikilize sala ya Papa!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Katika mahojiano na Vatican New, Kardinali Berhaneyesus Souraphiel wa Ethiopia, Askofu Mkuu wa Addis Ababa, akieleza kuhusu Ziara ya Papa Francisko huko Juba, Sudan Kusini, alisema kuwa: "Wakati, Papa anazungumzia juu ya amani, upatanisho, msamaha na kuishi pamoja bila kuzingatia masilahi ya kikabila au mambo mengine, lakini kama watu wa nchi hiyo mpya, Sudan Kusini, nilisikia watu wakipongeza sana kwa makofi na nina matumaini kwamba viongozi hawa watasikiliza sauti'hiyo ya watu”. Ni matumaini ambayo Kardinali huyo amekuwa nayo wakati akishiriki katika matukio mbali mbali ya Baba Mtakatifu nchini Sudan ikiwa ni hatua ya pili ya Ziara ya 40 ya kitume, maba baada ya kutoka Cong DR iliyoanza tarehe 31 Januari na kuhitimishwa huko Sudan Kusini Dominka tarehe 5 Februari 2023.
Akihojiwa na Vatican News kwa hiyo anashirikisha hisia na matakwa yake asa jambo ambalo lilimgusa na kwamba kwa ujumba tukio zima. Kwamba Papa alifika kama mtu rahisi na kwa urahisi huo pia alizindua wito huo, tena, kwa viongozi wa kiraia wa nchi hiyo mpya, Sudan Kusini. Wao walipata uhuru, na ambayo ni nchi tajiri... Lakini je wamefanya nini? Hakuna cha zaidi ya migogoro na vita, vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha uharibifu mwingi, hasa uharibifu wa maisha. Watoto na vijana wengi wamekufa, akina mama na wazee wamekuwa wakimbizi, katika nchi zao na nje ya nchi.
Kuna mamilioni ya wakimbizi kwa sababu viongozi wa kiraia wanaweka kwanza maslahi yao binafsi na madaraka. Papa Francisko kwa miaka minne iliyopita aliwaalika jijini Vatican kufanya mafungo ya kiroho pamoja. Alibusu hata miguu yao akisema: “Mna wajibu wa kuwa karibu na watu wenu, si kuonesha uwezo, bali huduma, kama wachungaji wema”. Na hiyo ilienda vizuri sana lakini hali halisi bado ndani nchi.
Akielezea juu ya uwepo wao mjini Juba kwa ziara ya Papa pia kwa msaada kwa Baraza la Maaskofu wa Sudan Kusini alisema kwamba ni kweli Sudan na Sudan Kusini wana Baraza la Maaskofu sawa, na wako katika eneo linaloitwa Amecea, yaani Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa kanda ya Afrika Mashariki, Afrika Kusini na Pembe ya Afrika. Kwa hiyo walikwenda kuwa pamoja nao na kuwaonesha kwamba wako pamoja wano na wanawaombe kwa sababu ziara hiyo ya kiekumene na ya amani ni maalum. Sio kwa sababu tu ya uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko, lakini pia kwa sababu Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Kanisa la Scotland walkwenda huko. Watu hawa wote, jumuiya hizo, walikuwa kwenye uwanja wa ndege kuwapokea viongozi watatu wa kidini, ambao pia walisali kwa sala ya kiekumene ya Kikristo.
Kwa maana hiyo Kardinali alisema amavyo amni kwamba Bwana atawasikia, na watakatifu wote na wafia dini wote walioteseka hapo pia watasaidia. Yeye binafsi alisema anaomba kwamba watu wa Sudan Kusini wapate amani. Wengi wamefanyia kazi hilo, wamisionari wengi wametoa maisha yao kwa ajili ya hilo, na marafiki zao na majirani pia wameiombea nchi hiyo mpya. Na vile vile anaamini Bwana atasikia maombi hayo, na machozi, kwa sababu amesikia vijana, ambao wamehamishwa kwa miaka mingi. Wanataka kuwa na maisha ya kawaida, shule ya kawaida wanataka kucheza. Walizungumza na Papa juu ya haya yote na kuomba awaombea na hivyo kwa hakika lilimgusa sana. Hao waliomba baraka kwa watoto wa Sudan Kusini na hiyo ilivutia sana.