Tafuta

2023.02.02 Maaskofu wa Afrika wakizungumza na vyombo vya habari Vatican News wanayo ya kusema. 2023.02.02 Maaskofu wa Afrika wakizungumza na vyombo vya habari Vatican News wanayo ya kusema. 

Maaskofu wa nchi zenye migawanyiko&ghasia kuwa karibu na Papa

Kardinali Ambongo:“Ilihitaji ujasiri kufanya hivyo,tusikubali kugawanywa na siasa”.Kardinali Kambanda,Rwanda:“Maneno ya Francisko yamenigusa,msamaha ni ufunguo na njia ya kuishi pamoja.Na Askofu mkuu Bonaventure Nahimana wa Burundi,"Upatanisho ni ufunguo wa kuishi pamoja."

Andrea Tornielli - Kinshasa

“Kwa pamoja leo  hii tunaamini kwamba kutoka kwa Yesu daima kuna uwezekano wa kusamehewa na kuanza upya na pia kupata nguvu ya kujisamehe mwenyewe, wengine na historia! Kristo anataka kutupaka mafuta kwa msamaha wake ili kutupatia amani na ujasiri wa kusamehe kwa upande wake, ujasiri wa kutekeleza msamaha mkuu wa moyo”. Papa Francisko alipotamka maneno haya katika mahubiri ya Misa katika uwanja wa ndege wa N'dolo mjini Kinshasa, pembezoni mwake, wakati wa maadhimisho ya Ekaristi, walikuwa ni maaskofu wa nchi ambazo watawala wao wanapigana wao kwa wao kwa njia ya wanamgambo na makundi ya waasi, na nchi ambazo zimekuwa, na ni ukumbi wa jeuri na vita visivyoelezeka, vinavyochochewa si tu na nguvu za nje bali pia kutoka ndani mwake. Pamoja na washirika wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, altareni na kisha kwenye chakula cha mchana pamoja, walikuwepo, miongoni mwa wengine, maaskofu wa Rwanda, Burundi na Congo Brazzaville. Kabla ya kuondoka kuelekea nchi zao, baadhi yao walikusanyika kuzunguka meza katika hoteli ambapo walisimulia tukio hilo kwenye vyombo vya habari vya Vatican, huku wakieleza jinsi uwepo wao hapo na ushirika wa kiaskofu unavyoweza kusaidia mchakato wa amani.

Askofu Mkuu Ambongo:Papa kati yetu ni matumaini

“Tunapitia wakati maalum, kairos, hatupaswi kugawanywa na siasa lakini tuone nini tunaweza kufanya pamoja,” alisema hayo Kadinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Kinshasa. “Ujumbe wa Papa ulikuwa wa nguvu sana. Wakati wanasiasa wanapanda chuki miongoni mwa watu, wanachoche, chuki dhidi ya wageni na kuchochea kutoaminiana miongoni mwa watu; Maaskofu na Kanisa wameitwa kuchukua njia nyingine, na lazima wasiingilie katika mantiki hiyo”. Kwa hiyo Kardinali Ambongo amewashukuru wajumbe kutoka Rwanda “kwa kuja hapa Kinshasa. Ilihitaji ujasiri kufanya hivyo. Ujasiri wa kutekeleza utume wa pamoja”.

Kardinali Kambanda, Rwanda:kutembea katika njia ya msamaha

Naye Kardinali Antoine Kambanda, Askofu mkuu wa Kigali, nchini Rwanda, alisisitiza akikumbuka matakwa ya Papa Francisko kwamba angependa pia kwenda Goma, mpakani na Rwanda, lakini haikuwezekana kutokana na vurugu na mapigano yanayoendelea. “Kwa hiyo alisema  sisi maaskofu tulikuja hapa sita kati ya wanane. Ujumbe wa amani ambao Papa amekuja kutuletea unatuhusu sisi sote. Unatugusa sote. Ulinigusa mimi binafsi.” Kardinali Kambanda hata hivyo alikumbuka kwa hisia kali ya mauaji ya halaiki yaliyotokea nchini mwake mnamo 1994, wakati katika siku mia moja watu wasiopungua 800 elfu waliuawa kutokana na mzozo wa kikabila na kisiasa. “Hayakuwa mauaji ya kimbari yaliyosababishwa na wengine, kutoka nje. Ilitengenezwa na Wanyarwanda. Kutoka miongoni mwa idadi ya watu wanaoishi pamoja kwenye vilima sawa. Kila kilima kilikuwa na msiba wake. Na leo hii tunaweza kujiuliza: ni jinsi gani ya kuishi vipi pamoja baada ya kupitia mauaji ya kimbari?”. Jibu la Kardinali Kambanda linalingana na lile ambalo Papa alikuwa amemaliza kutamka kuwa: “Msamaha ni njia ya kuishi pamoja. Ili kuishi pamoja tunapaswa kujisamehe wenyewe. Msamaha ndio ufunguo. Msamaha ni neema kutoka kwa Mungu na inahusu kila mtu: watu, na wakosaji binafsi, lakini pia familia”. "Njia ya msamaha, aliongeza Kadinali huyo wa Rwanda, “ni huruma, kwa kutambua kwamba mwingine pia anateseka na kwamba mateso yangu yameunganishwa na yake. Huu ndio ufundishaji wa msalaba”. Uzoefu waliouishi wa nchi yake "tunashirikishana na washirika wetu katika uaskofu. Msamaha pia unaruhusu upatanisho wa amani ya kumbukumbu”.

Burundi, Askofu Mkuu Bonaventue:Kupanishwa na kukaribisha

Kwa upande wa Askofu mkuu wa Gitega, Bonaventure Nahimana, na rais wa Baraza la maaskofu wa Burundi,  alisema “Upatanisho ni ufunguo wa kuishi pamoja, ni ufunguo wa kutatua migogoro ya kidini, kikabila na kisiasa”. Na ndiyo  juu ya hili kwamba mchakato wa sinodi ya Makanisa ya Burundi umelenga. Majimbo  yote yanahusika. Ni lazima tuishi kwa msamaha ili kweli tuwe na jumuiya za kindugu zilizo wazi, zinazokaribishana. Pia ni wazi katika kumkaribisha mwingine kama ndugu, hata akiwa mgeni. Tuna wakimbizi wengi wa Congo nchini Burundi. Jinsi tunavyoishi hivyo, ndivyo tutaaminika”, alifafanua katika vyombo vya habari Vatican.

Congo Brazaville, Askofu Mkuu Bienvenu:Wote tunahitaji amani

"Tuko hapa na wajumbe wengi, sio tu wa maaskofu, bali wa watu , alieleza pia Askofu mkuu Bienvenu Manamika wa Brazzaville, na  rais wa Baraza la Maaskofu wa Congo Brazzaville, kwamba “ziara ya Papa itakuwa na  matokeo makubwa katika kanda” . Hata kama nchi yake haijaathiriwa moja kwa moja na migogoro, lakini “bado tunahusika”, alisema.  “Kuna msemo usemao kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikikohoa, sisi Congo Brazzaville tunapiga chafya na kupata mafua.” “Sote tunahitaji amani, aliongeza kusema "Mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC hautuachi na utulivu". Alikumbuka majeraha ya vita ambayo tayari yamewakumba. "Ni lazima tuchukue maneno ya Papa Fransisko kwa uzito" kwa hiyo, ni ujumbe ambao unaweza kuondoa kuzuka kwa vita”. Askofu Mkuu Manamika alibainisha kwamba "kuwepo tu kwa Mfuasi wa Petro kunatia matumaini na unatazama kila mtu: “Ninatumaini kwamba maneno yake pia yatasikilizwa na mashirika ya kimataifa yaliyo chini ya mwavuli wa tasnia uzinduaji wa viwanda. Ni watu wanaoteseka na hali hii, bila haki bila hadhi hakuna amani”. Migogoro ya ndani, alihitimisha, “inategemea maslahi makubwa zaidi. Lakini wakati ‘tembo wanapopigana ni nyasi zinahumia’. Na nyasi ni watu. Kwa hilo lazima sote tufanye kazi na kuomba kwa ajili ya amani”.

Kisangani DRC,Askofu Mkuu Utembi Tappa:Lazima tujifunze kusamehana

Askofu mkuu Marcel Utembi Tapa wa Kisangani, na  rais wa Baraza la maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alibainisha kuwa "Lazima sote tujenge amani. Kwa msamaha, kwa ugunduzi upya wa jumuiya inayotuunganisha na utume tulionao. Tunapaswa kujiridhisha kuwa msamaha wa kibinafsi na wa kitaasisi unahusishwa. Kama watoto wa Mungu waliobatizwa, kaka na dada, ni lazima tujifunze kusameheana. Papa anafahamu vyema kila kitu kinachotokea hapa, na jinsi gani kinachotokea hapa ni tishio kwa ajili ya amani, tatizo ambalo linahusu kanda nzima ya bara. Alitualika kukuza ufahamu wa udugu unaotuunganisha na ambao hauhusu nchi moja tu bali ukanda mzima. Sisi sote tumeitwa kuwa wamisionari wa amani. Ilikuwa wito wake mkubwa kwa majimbo, mashirika ya kiraia, kwa Kanisa, kwa wachungaji",alisisitiza Papa.

Ziara ya Papa Francisko DRC
Ziara ya Papa Francisko DRC

Ujasiri wa Maaskofu hawa wakiungana pamoja na Mfuasi wa  Petro, ni ishara ndogo lakini kubwa ya matumaini kwa nchi hizi zinazoteswa, ambapo migogoro ya kikabila na kisiasa inahusisha Wakristo wa pande zote mbili. Papa Francisko alisema katika mahubiri yake kwenye uwanja wa ndege wa N'dolo: "Wakati huu uwe mzuri kwenu ambao katika nchi hii wanajiita Wakristo lakini wanafanya vurugu; kwenu Bwana asema hivi, weka chini silaha zenu, na kumbatiwa na huruma”.

Maaskofu wa DRC,Rwanda
02 February 2023, 15:01