2023.02.14 Mkutano wa kibara wa Makanisa ya Nchi za mashariki wamehitimisha na tamko lao.(13-17 Feb 2023) 2023.02.14 Mkutano wa kibara wa Makanisa ya Nchi za mashariki wamehitimisha na tamko lao.(13-17 Feb 2023) 

Tamko la Mkutano wa kisinodi kwa makanisa ya Mashariki 13-17 Februari

Kudumisha umoja katika utofauti na ushuhuda wa mizizi ya pamoja ya Makanisa.Utambuzi wa vipaji vya walei katika huduma ya Mwili wa Kristo.Wajibu wa vijana na uwezo wao.mwaliko wa uekumene bunifu na kuchochea mazungumzo ya kiekumene.Kanisa kuwa wazi kwa wengine walio tofauti katika ngazi ya kikanisa na kidini.Hayo yamo katika tamko la mkutano wa Kibara kwa Mashariki ya kati Feb.13-17 Feb.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Mkutano wa kibara kuhusu Sinodi katika Makanisa ya Mashariki ya kati ulioanza tarehe 13 Februari hatimaye umehimishwa mnamo Ijumaa tarehe 17 Februari na tamko rasmi- Katika tamko hilo wanaanza kusema kuwa wa ona watu wao katika sala wanamshukuru Roho Mtakatifu, ambaye aliwafikisha pamoja kwa ajili ya Kanisa la Kisinodi, na aliwaongoza kusali pamoja katika ushirika, ushiriki na utume kwa njia ya Mkutano wa kisinodi wa awambu ya kibara Bara kwa makanisa ya Mashariki  ambayo yaliunganisha familia katoliki na Makanisa yake saba huko Bethania - Harissa kwa Juma zima.  Mkutano huo umefanyika katika mazingira magumu kwa eneo lao, zaidi ya yale yote ya kiuchumi na kibinadamu, hasa kutokana na athari za tetemeko kubwa la ardhi lililowakumba ndugu zao huko Siria na Uturuki.

Wakati wa mkutano wa kibara huko Lebanon
Wakati wa mkutano wa kibara huko Lebanon

Kwa hiyo, washiriki wa mkutano huo walitafakari juu ya tukio hilo la uchungu na la kuhuzunisha na kuomba sala za kila siku kwa ajili ya waathirika, waliojeruhiwa na waliopoteza makazi katika maeneo yaliyoathiriwa. Na kwa kuwa wao ni watoto wa Ufufuko, wameendeleza kazi ya mkutano huo, ambao ulikuwa ni hatua ya kibara na kiungo katika mchakato wa safari ya sinodi inayoendelea. Washiriki wa kazi za Mkutano huo pia wamemshukuru Katibu Mkuu wa Sinodi, Kardinali Mario Grech, na Mjumbe Mkuu wa Mkutano Mkuu ujao wa Sinodi ya Maaskofu, Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Luxembourg na Sista Nathalie Becquart, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Sinodi kwa uwepo wao katika kazi ya mkutano  na kuishi nao uzoefu huu wa sinodi, ambao umeongeza chachu katika maisha ya Kanisa Katoliki Mashariki na Ulimwenguni.

Kwa njia hiyo wamethibitisha kuwa hayo yote yanafanyika kama alivyoomba Baba Mtakatifu Francisko kwa watoto wa Kanisa Katoliki ulimwenguni  kupitia kwa upya maisha yao ya Kikristo na kutembea pamoja katika nuru ya Injili na mahitaji ya wakati huu kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi itakayofanyika katika Jiji la Vatican mwezi Oktoba 2023 na 2024, yenye kauli mbiu: “Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume”. Hatua ya Bara iliyofanyika katika Hoteli ya Bethania-Harissa ilijikita zaidi katika sala, utambuzi wa kiroho na kutafakari kwa pamoja, kwa muda wa juma zima yaliojitokeza wakati wa hatua ya kwanza ya mashauriano ya Makanisa mahalia katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati na Ghuba.

Na kuhusu uthibitisho tena wa kanuni msingi za Kanisa wametoa tamko lao kuwa: Sinodi ndio kiini cha urithi wa makanisa yeo  ya Mashariki. Umoja katika utofauti kwa njia ya umoja katika ushirika, utume na ushuhuda wa Makanisa.  Mizizi ya pamoja ya Makanisa kama msingi wa ujumbe wa umoja. Uwepo na vipaji vya walei katika huduma ya Mwili wa Kristo. Wajibu wa vijana, uwezo wao na matarajio yao kwa Kanisa lililofanywa upya huakisi changamoto wanazokabiliana nazo. Umuhimu wa nafasi na utume wa wanawake katika kanisa na ushiriki wao katika kufanya maamuzi na huduma. Liturujia ni maisha yetu na wito wa upyaisho wa kiliturujia unaoendana na matarajio ya vijana wetu, huku wakihifadhi asili yake na alama zake. Mwaliko wa uekumene bunifu na uliofanywa upya na kuchochea mazungumzo ya kiekumene.

Mkutano wa kibara, huko Makanisa ya Mashariki 13-17 Februari 2023
Mkutano wa kibara, huko Makanisa ya Mashariki 13-17 Februari 2023

Kanisa la uwazi kwa wengine walio tofauti katika ngazi ya kikanisa na kidini, kwa njia ya kusikiliza, majadiliano na muungano, kwa kuishi pamoja, mazungumzo, ushirikiano na kuheshimiana ili kuonesha uso wa Mungu mmoja. Ushirika na matumaini katika mateso: kuelekea Kanisa lenye unyenyekevu kama “mbegu ya haradali”(Mt 13, 31-32), lililoitwa kukua na kupanua kati ya changamoto ya kuishi na kukataa kuhama. Utume, ushuhuda na miundo iliyopyaishwa kwa ajili ya Kanisa la Kisnodi zaidi. Utunzaji maalum wa kichungaji kwa familia, wanawake na vijana. Umuhimu wa vyombo vya habari vya kidijitali na utamaduni kama nyenzo bora ya mawasiliano mikononi mwa Kanisa ili kufikisha ujumbe wake kikamilifu zaidi. 

Jinsi gani Kanisa linaweza kuwa la kisinodi katika nuru ya mkutano wa kibara

Kufuatilia moyo wa sinodi katika kila Kanisa kwa swali kuu lisemalo ni jinsi gani kila Kanisa linaweza kuwa sinodi zaidi katika nuru ya  kazi ya mkutano huo wa  kibara wa Makanisa Katoliki katika Mashariki ya Kati. Kipindi cha Kitakatifu cha Kwaresima kinachoanza Jumatatu tarehe 22 ni wakati mwafaka na wa pekee wa kusikia yale ambayo Roho anaeleza kwa makanisa yao wanaposikia neno la Mungu, kuomba, kutubu, na kutenda matendo ya upendo na huruma kuelekea ndugu zao katika mahitaji yao ya kimwili, kiroho na kimaadili, kwa njia ya maombezi ya Mama Yetu wa Lebanon, Mama wa Kanisa na Malkia wa Mitume.

20 February 2023, 13:40