Frt.Alois:Shukrani ushirikiano wa kutembea pamoja&watu wa jumuiya,harakati na Makanisa
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Jumanne na Jumatano tarehe 14-15 umefanyika Mkutano wa Kamati ya Maandalizi ya Mpango uitwao “Together. Mkusanyiko wa Watu wa Mungu”, ulioandaliwa na Jumuiya ya Kiekumene ya Taize, ikiwa na Mkuu wa Jumuiya Hiyo Ndugu Alois pamoja na baadhi ya waandaaji ili kuweza kutathimini nanba ya kuandaa mkesha. Kuhusiana na mada ya “Kwa pamoja. Mkusanyiko wa Watu wa Mungu” ni nini maana yale, Ndugu Alois, Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya Teize anasema ni katika kuandaa Mkesha wa maombi ya kiekumene ambayo utafanyika mjini Roma tarehe 30 Septemba 2023 mbele ya Baba Mtakatifu Francisko na wawakilishi wa Makanisa mbali mbali, ili kuungana pamoja katika kusifu na ukimya, katika kusikiliza Neno. Vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35, wanaotoka Ulaya kote na kutoka katika hali halisi ya Kanisa, wanaalikwa mwishoni mwa mwezi huo, kuanzia Ijumaa jioni hadi Dominika alasiri ili kushiriki, kwa kutembea pamoja kama Mungu na watu wake. Hii ni Katika fursa ya kuombea Sinodi ya Maaskofu ya Kawaida ya XVI itakayofanyika mjini Vatican.
Mwaliko wa Papa Francisko
Ilikuwa ni Dominika tarehe 15 Januari 2023 mjini Roma, mwishoni mwa sala ya Malaika wa Bwana, ambapo Baba Mtakatifu Francisko alitangaza kwamba shughuli ya Mkutano wa Sinodi ijayo ya Kanisa Katoliki ulimwenguni itatanguliwa na mkesha wa maombi ya kiekumene, mnamo Jumamosi tarehe 30 Septemba 2023 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, jijini Vatican. Papa wakati ule alisema: “Njia ya umoja wa Kikristo na njia ya uongofu wa sinodi ya Kanisa imeunganishwa. Nachukua fursa hii kutangaza kwamba mkesha wa maombi ya kiekumene utafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo Jumamosi tarehe 30 Septemba ambapo tutakabidhi kazi ya Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu. Kwa vijana watakaofika kwenye mkesha huo, kutakuwa na programu maalum katika mwisho ni mwa Juma hilo lililoandaliwa na jumuiya ya Taizé. Kwa hiyo kuanzia sasa ninawaalika kaka na dada wa madhehebu yote ya Kikristo kushiriki katika mkutano huu wa watu wa Mungu.”
Mkesha wa sala ni kwa ajili ya wote hasa wanaoishi pembezoni
Kwa hiyo katika mkutano wa kamati kwa mujibu wa padre Davide Carbonaro, Paroko wa Mtakatifu Maria huko Portico ya Campitelli ambaye ni mhusika Mkuu wa Mchakato wa Sinodi kwa Kanisa la Roma, wakati wa kamati ya washirika katika Nyumba Kuu ya Shirika ya Yesu (Jesuit) kwa kutembelea kujua hali halisi kwa ngazi ya kiekumene(Kanisa la kimetodi, Kituo cha Kianglikani, na Wavaldesi. Kwa namna ya pekee, pia kulikuwa na fursa ya kujifunza kwa ukaribu zaidi na kuthamini kazi ya kiekumene na wahamiaji na wakimbizi wanaowasili jijini Roma kupitia mikondo ya kibinadamu. Waandaaji pia walitaka kuwafungulia watu hawa, ambao wameishi maisha ya kujitenga na kukubalika katika nchi nyingine mbali na nchi yao ya asili, kwa sababu wao ni sehemu ya watu wa Mungu kama alivyo eleza Sr. Natalie Bequart, Katibu msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu na kwamba wangependa washiriki katika mkesha huo pamoja na wale wote wanaoishi pembezoni.
Sinodi na uekumene vyote vinafundisha kufanya uzoefu kwa hiyo hali kadhalika na uekumene kwa mujibu wa Anne-Laure Danet, mchungaji wa Kiprotestanti kutoka Paris Ufaransa ambaye alisema kuwa, inasadikishwa na hili, kuhusu umuhimu wa kuhusika katika sala jijini Vatican katika mkesha wa mkutano wa sinodi. Kwake yeye amesema ni fursa ya ajabu sana kupata kile wanachoita 'uekumene wa mshikamano', ambao kwa hakika unamaanisha kupata nyakati za maombi pamoja. Kwa sababu bila urafiki hakuna uekumene. Wanaamini katika umoja uliopatanishwa; katika siku hizo za mkutano wa maandalizi lengo limekuwa katika kusikiliza Neno la Mungu na hali hiyo hiyo itatokea mnamo Septemba. Changamoto ni kuhamasisha sio tu wakuu wa Makanisa lakini watu wote. Kama wasemavyo kwamba kwenye peke yetu tunakwenda haraka, lakini kwa pamoja tunakwenda mbali”.
Baba Mtakatifu Francisko alikutana kabla ya Katekesi ya Jumantano na Ndugu Alois, Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya Taize tarehe 15 Machi 2023, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo mara baada ya mkutano huo alipata ya kueleza kwa waandishi wa habari kwamba, mkutano wao ulitumika kufanya upya moyo na kusisitiza kwa mara nyingine tena kwamba tofauti za kitaaalimungu katika uekumene hazituzuii kusali pamoja. Kwa hiyo kundi hilo linaripoti kwamba Papa pia alikumbuka baadhi ya uzoefu wake wa ujana wa kiekumene, akitazama ni maendeleo yapi yamepatikana wakati na kabla ya Mtaguso, wakati kulikuwa na hali ya umbali na mashaka kwa waamini wa Makanisa mengine.
Hata hivyo Ndugu Alois kwanza alielezea jinsi gani wanajiandaa katika awamu hiyo ya maombi yajayo kwamba: “Nashukuru sana kwa ushirikiano huu, kwa kutembea pamoja na watu kutoka jumuiya mbalimbali, harakati, Makanisa ambao walikuwa bado hawajajuana lakini wameanza kufanya hivyo. Mkutano huu ambao tumekuwa nao ni kama taswira ndogo ya kile kitakachotokea tarehe 30 Septemba hapa Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati Wakristo wa Makanisa yote wataadhimisha kwa pamoja umoja unaotokana na Kristo. Na kuhusiana na mkutano na Papa aliokutana anao kabla ya Katekesi: “Alisema tusiogope: hata kama Roho Mtakatifu wakati mwingine huleta machafuko kidogo, basi maelewano hutokea. Sinodi si bunge bali ni maelewano yanayotoka kwa Roho Mtakatifu. Ni ujasiri sana kwamba Papa amezindua njia hii ya uwazi kwa Roho Mtakatifu. Jumuiya ya Taizé tunashukuru sana kwa hili”.
Ukifikiria nini juu ya vita vya Ukraine, unafikiri uekumene unaweza kuwa na jukumu muhimu? “Tunaishi katika wakati mgumu sana, kuna vita hivi, kuna magumu mengine, ya kiikolojia kwa mfano, vijana, sasa ni wakati mgumu kweli kweli. Uekumene sio njia ya kushinda magumu yote haya, lakini ni lazima tuchukue kwa uzito Neno la Kristo kuwa Mmoja. Hii si rahisi sasa, na mvutano pia katika Kanisa la Kiorthodox. Ni lazima tuwe na subira na kujaribu kuutazama ushirika kwa kadiri inavyowezekana sasa.
Uvumilivu unsaidia nini? Subira inayowaka. Kwa sababu haiwezekani kukubali mgawanyiko huu unaoletwa na vita, hapana. Tunapaswa kufanya miunganisho. Yeye amekuwa nchini Ukraine wakati wa Noeli. Walitembelea Makanisa mbalimbali, hata kama kuna mvutano kati yao. “Tulifikiri, kabla ya vita, kwamba umoja wa Makanisa ungeweza kuundwa lakini si rahisi hivyo. Kwa hivyo, lazima twende kwa kila mtu. Kuishi kwa ziara za pamoja na maombi ya umoja huu tunatumainia”. Na katika kuelezea juu ya Miaka kumi ya upapa wa Papa Francisko anavyokumbuka alisema anaikumbuka kwa shukrani nyingi. Amekuwa akimkaribisha kila mwaka, na wamekuwa katika wakati wa kushiriki. Amekuwa akivutiwa sana na utulivu wake. Ni zawadi kubwa. Kuna shida nyingi, mizigo anayobeba lakini kuna utulivu huo. Ni mfano mzuri sana kwake binafsi, lakini pia anafikiri ni kwa Wakristo wote.