Sinodi ya Bara la Afrika:Ushuhuda wa Hatem Bourial,Mwislamu
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Hatem Bourial alizungumza kama Mwislamu aliyejihusisha sana na uekumene na mazungumzo ya kidini. Katika awamu ya Bara la Afrika ya Sinodi iliyofanyika huko Addis Ababa, Ethiopia kuanzia tarehe 1 hadi 6 Machi, ilileta pamoja zaidi ya washiriki 200 kutoka nchi 41 za Afrika na Visiwani. Washiriki pia walijumuisha Waethiopia kama wenyeji na wageni kutoka mabara mengine, hasa wale wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu wa Vatican. Pia kulikuwa na baadhi ya watu waliowekwa wakfu, mapadre, Maaskofu na Makardinali. Sinodi ya Addis Ababa pia ilikaribisha wageni kutoka tamaduni nyingine zingine za kidini ambo Waislamu na washiriki wa dini za jadi za Kiafrika pamoja na akristo kutoka madhehebu mengine.
Kwa hiyo Bwana Hatem Bourial, Mwislamu kutoka Carthage, na mwandishi wa habari wa Tunisia, ambaye alishiriki katika mkutano wa sinodi, katika mahojiano yake alisisitiza thamani ya mchakato wa Sinodi ya Afrika, akilinganisha na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, ambao alisema ulifungua ukurasa mpya kwa ajili ya Kanisa Katoliki na mahusiano na imani nyingine. Katika mahojiano yaliyofanywa kwa ajili ya Vatican News huko Addis, kwa lugha ya kifaransa Bwana Hatem Bourial alithibitisha kwamba kutembea pamoja, kunamaanisha kuangalia kuelekea sehemu moja. “Ni kukaa katika mawasiliano; kutazamana bila kuamua, kuacha na nyakati fulani kurudi nyuma, kurekebisha lengo la kwanza.”
Akitoa kielelezo cha Waisraeli, ambao katika Maandiko ambao walikuwa “watu waliokuwa wakienda sikuzote,” alikazia kwamba kutembea pia kunamaanisha jitihada na uhusiano ambao ni wa maelewano na wasafiri wenzao lakini pia unajitafakari mwenyewe; na ya mpito inapohusu kundi zima. Akitafakari juu ya safari iliyoshirikishwa, Hatem alipendekeza kurejea kwa tafakari ya Isaya juu ya upanuzi wa hema (Isa 54:2) ikiwa tutafahamu hatari na udhaifu wa huku “kutembea pamoja.” ndipo tunaweza kuelewa vyema kuwa, kuwa pamoja ni nguvu na kuwa wengi na katika ushirika kunawakilisha nguvu Zaidi.
Bwana Hatem Bourial alipendekeza kwamba Sinodi ya Bara la Afrika ieleweke katika mwelekeo wa kiekumene kwa sababu, kwake, ilikuwa ni uzoefu sawa na ule wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, ambao “ulifungua ukurasa mpya” si kwa ajili ya Wakatoliki pekee bali hata katika mahusiano yake na wengine. Kwa hiyo Sinodi pia inafungua ukurasa mpya kuhusu ushiriki, ushirika na ujumuishaji kwa maana ya kujumuika ambako kunajenga harambee na kuwaleta pamoja wakristo, wayahudi na waamini wa Kiislamu na, katika mchakato huo, kunaimarisha kila mtu katika imani yao. Akirejea kuhusu imani yake mwenyewe ya Kiislamu, Hatem alidokeza kuwa kitendo cha kutembea zaidi kinamaanisha na kinajumuisha juhudi kuelekea hamu ya kujiboresha. Kwa hiyo kuwa na uhusiano na wengine ndio msingi wa uhusiano wowote wa kiekumene.
Mwandishi huyo wa Tunisia alisema sinodi ya bara la Afrika imedhihirisha bila shaka uwezo wa Kanisa wa kuunganisha, kujumuisha, na kusonga mbele. Hii ina maana kutakuwa na fursa muhimu kwa wale ambao hawamo Kanisani wala hawaitumii imani yao kwa bidii. Hatem anaamini kwamba utayari na mwelekeo wa kujumuisha na kusikiliza waumini wa dini zingine ni ishara nzuri kwa wale walio katika misikiti na masinagogi. Alihisi kwamba mbinu kama hiyo inaweza kusaidia kutatua "pengo la kutopendezwa" ambalo ulimwengu unateseka leo, na kusababisha upotezaji wa marejeleo ya kidini kati ya watu binafsi na jamii. Ikiwa tunataka kujiweka katika njia ya kiekumene,ni muhimu kufikiri kwa suala la ulimwengu wote.
Hii ina maana ya kujiweka katika mtazamo wa kihistoria: kadiri Mtaguso wa II wa Vatican ilivyokuwa muhimu, sinodi hii itafungua ukurasa mpya ambao ungeweza kudumu kwa nusu karne”. Katika ulimwengu huu wote, Hatem anatetea kurejea kwa mantiki ya kiutamaduni ya Kiafrika ambayo yanaweza kuoneshwa katika Kanisa na mikutano ya kiekumene bila kupoteza mtazamo wa pekee wa Kiafrika. Aidha, alikazi kusema, ukarimu na mapendo lazima viwe msingi wa usindikizwajihaya kwa sababu kupanua hema ya mtu kunamaanisha kuwa na upendo zaidi: upendo wa jirani kuwa mapigo ya moyo wa mapokeo ya Kikristo.