Nikaragua,wamefukuzwa watawa wawili wa Costa Rica
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Watawa wawili wa Costa Ria wa Shirika la Wadominikani wa Tangazo Sr. Isabel na Cecilia Blanco Cubillo, waliokuwa wanatoa huduma yao katika makao ya wazee katika Kituo cha Mfuko wa Susana López Carazo, walifukuzwa Jumatano tarehe 12 Aprili 2023 kutoka Nicaragua. Watawa hao wawili hapo awali walikuwa wakisimamia nyumba ya Rivas tangu mwaka wa 1958. Wote wawili waliwasili Costa Rica siku hiyo mchana.
Monasteri ya watawa wa Ktrappist ilichukuliwa
Vile vile Siku moja kabla, mnamo tarehe 11 Aprili 2023 serikali ya nchi ya Nicaragua ilitaifisha nyumba ya watawa wa Kitrappist, iliyoko Mtakatifu Pedro de Lóvago, Chontales, na kuikabidhi kwa Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo ya Nikaragua, INTA. Watawa wa Kitrappist waliondoka kwenye monasteri mnamo tarehe 24 Februari iliyopita na walifika Panama siku iliyofuata. Shirika la Masista wa Cistercian wa Utunzaji lilifika Nicaragua kutoka Argentina mnamo tarehe 20 Januari 2001.
Kufukuzwa
Mnamo Julai 2022, Wamisionari wa Upendo, walioanzishwa na Mtakatifu Mama Teresa wa Calcutta, walifukuzwa kutoka Nicaragua baada ya Bunge la Kitaifa kubatilisha hali yao ya kisheria. Mwanzoni mwa Juma Takatifu, Mmisionari Mklaretia wa Panama, Padre Donaciano Alarcón, alifukuzwa kwa ajili ya kumuombea Askofu Rolando Álvarez, Askofu wa Jimbo la Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Estelí, aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 26 jela, tangu tarehe 9 Februari 2023 baada ya kuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu tarehe 19 Agosti 2022.
Jumuiya ya Wakatoliki imepitia ugumu sana katika kipinidi cha Juma Takatifu baada ya Rais Ortega kupiga marufuku matukio ya kiutamaduno ya wakati huu. Zaidi ya maandamano 3,000 yamepigwa marufuku nchini humo na takriban watu ishirini wamekamatwa.