Tafuta

Watawa wa UISG wana shughuli nyingi za kuleta pamoja,kasi,mawazo na ahadi za kulinda na kutunza sayari kulingana na waraka Laudato sì na Malengo ya Maendeleo  Endelevu Watawa wa UISG wana shughuli nyingi za kuleta pamoja,kasi,mawazo na ahadi za kulinda na kutunza sayari kulingana na waraka Laudato sì na Malengo ya Maendeleo Endelevu  (Copyright (c) 2020 24K-Production/Shutterstock. No use without permission.)

Watawa wanaoongoza kufanya mapinduzi ya mgogoro wa tabianchi

Masista Wakatoliki wanataka kuchukua hatua madhubuti katika kulinda watu na jamii zilizoathiriwa na janga la tabianchi na upotevu wa bayoanuwai.Msururu wa “Mazungumzo yanayoongozwa na watawa na wadau wa kimataifa pamoja kwa matumaini ya kuendesha harakati ya kimataifa ili kubadilisha maneno kuwa vitendo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Masista katoliki wa Umoja wa Mama Wakuu wa Mashirika Kimataifa (UISG) wana shughuli nyingi ya kuleta pamoja, kasi, mawazo na ahadi za kulinda na kutunza sayari kulingana na waraka wa Papa Francisko wa Laudato sì na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa. Mdahalo wa kwanza wa mfululizo wa midahalo iliyoongozwa na Masista ulifanyika mjini Roma tarehe 16 Aprili 2023  ili kutoa changamoto kwa mashirika ya kimataifa, serikali, mashirika ya kiraia, taasisi za Vatican na wasomi katika mada tatu: kuunganisha majibu ya mabadiliko ya tabianchi na upotevu wa bayoanuwai; kuunganisha huduma kwa watu na sayari yetu; kuunganisha udhaifu katika uongozi.

Sister kuongoza mazungumzo kuhusu mazingira: Sr. Maamalifar
Sister kuongoza mazungumzo kuhusu mazingira: Sr. Maamalifar

Mikutano iliyoandaliwa na mpango wa UISG wa Masista Wanaotetea Ulimwengu, ni kwa ushirikiano na Mfuko wa Kimataifa wa Mshikamano na ambao utafikia kilele chake katika Jukwaa la kwanza l UISG la Utetezi, litakalofanyika jijini  Roma mnamo Novemba 2023. Sista Maamalifar Poreku, Mmisionari wa Mama Yetu wa Afrika, na Katibu Mwenza wa Ofisi ya UISG ya Haki, Amani na Uadilifu wa Uumbaji na Mratibu wa mpango wa shirika la Sowing Hope for the Planet yaani Kupanda matumaini katika Sayari, katika mahojiano na Vatican News, amezungumzia ni kwa nini anaamini kuwa watawa wako mstari wa mbele  katika  kuleta mabadiliko katika ulimwengu ambapo ahadi za mabadiliko ya tabianchi hupuuzwa kila mara na watu na nchi zilizo hatarini zinazidi kutishiwa na kukumbwa.

Masisita wako mstari wa mbele wa kulinda mazingira
Masisita wako mstari wa mbele wa kulinda mazingira

Akijibu kuhusu kile anachofikiri kuhusu watawa wanaweza kuleta nini kwenye mazungumzo ya hali ya juu, mmisionari huyo aliweka wazi uhusiano kati ya imani na ulinzi wa kazi ya uumbaji, huku akionesha jinsi watu wa dini wanavyochukua maandishi na mfano wa Papa Francisko na kuwatia moyo , ukiwasukuma kuwa  wajasiri na wenye kuthubutu kutenda.  Sr. Maamalifar alieleza kwamba mpango wa Sowing Hope for the Planet,   yaani Kupanda Tumaini katika Sayari ni moja ya matokeo ya waraka wa Papa Francisko kuhusu  Utunzaji wa Nyumba yetu ya Pamoja kwani iliwahimiza masista kutafakari jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto yake na iliwapa fursa ya kufanya jambo kuhusu mazingira ili kila mtu yapate mahali pake na kila kiumbe pia apate mahali pake.

Kwa mujibu wake alisema sio tu juu ya wanadamu, kwa sababu mwanadamu na viumbe vingine vimeunganishwa, lakini ni kwamba  kile kinachoathiri moja huathiri kingine, na kupanda matumaini kwa sayari kunamaanisha kuleta matumaini kwa watu wote na kwa umoja wetu nyumbani. Na kile kinachoathiri viumbe vingine pia kinaathiri wanadamu. Wazo ni kuona namna ya kuwawezesha watawa kwa ngazi za chini kuwa makini katika kuchangia ufufuaji wa viumbe hai na pia kuleta mabadiliko ya hali ya tabianchi kwa maana chanya kwa sababu kwa sasa mabadiliko yanayoonekana katika hali ya tabia nchi ni hisia hasi. Tangu Papa Francisko alipotoa waraka huo, mipango mingi yenye sifa imezinduliwa. Alipoulizwa ni kwa nini anafikiri watawa wanaweza kuleta mabadiliko katika mchakato unaoendelea, Sr. Maamalifar alielezea mbinu yao kwa ujumla. Kama Baba Mtakatifu Francisko anavyowaambia, kuwa “mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira sio tu suala la kijamii, lakini linahusiana sana na imani na kama watawa kimsingi,  kila kitu kitu  wanachofanya ni juu ya imani inayo waruhusu kuungana na Muumba na Uumbaji wote”.

Pia kuna mwamko, wa kuwa kufanya peke yao hawana vifaa vya kukabiliana na hali hiyo kwa sababu ni kubwa sana na hawana ujuzi wote unaohitajika kukabiliana nayo lakini kwa kuelimisha, kushirikiana na jamii mahalia na  wale ambao wameathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi na upotezaji wa bioanuwai wanafikiri kwamba wanaweza kutoa hatua chanya ambazo zitakuwa na matokeo madhubuti. Sr Maamalifar, aidha alisema kuna majadiliano mengi juu, maazimio mengi, ahadi nyingi, lakini mwisho, ahadi hizo hazifanyi kazi, hivyo watu wa chini hawaamini tena ahadi hizo. Kwa hivyo, mpango unaotarajia kuwapa Masista ujuzi ili nao waweze kufanya kazi moja kwa moja na jamii zilizoathirika ni kwa sababu mazungumzo peke yake hayaleti matokeo, bali wanahitaji vitendo madhubuti. Na sasa wamekuwa watawa  44 ambao wamewasilisha mipango ambayo wanakwenda kutekeleza, alisema huku akitoa mifano miwili kwamba: mmoja nchini Sri Lanka ambao unalenga vijana na mmoja nchini Ghana ambako ukame umeathiri mazao na hatimaye  lengo ni kupata chakula kwa ajili ya watoto.

Katika yote mawili, alieleza, ni wazi kwamba kinachotokea kwenye mazingira kinamgusa mtu moja kwa moja, na Masista wana uwezo wa kuwa na mtazamo kamili wa suala hilo linalojumuisha kijamii, mazingira na kiroho, yote haya ni muhimu kwa watu binafsi, jamii, mataifa na sayari. Kwa hivyo wanajaribu kushikilia mambo haya matatu pamoja ili waweze kusonga pamoja kwa sababu kuchukua mwelekeo mmoja pekee haitoshi. Kwa kufanya hivyo wanahitaji vitu vidogo na vitendo ambavyo vinakuwa vikubwa, Sr Maamalifar aliendelea, kubadili mwelekeo mbaya wanaoshuhudia, na kusisitiza imani yake kwamba mabadiliko ya kweli yanatoka mahalia kuwa wale walio juu hawahisi athari ya kile kinachotokea sasa. Mabadiliko, yatatoka kwa wale ambao wanabeba mzigo mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi na upotezaji wa bayoanuwai mara tu watakaposaidiwa kuelewa kwa nini wanateseka, ni nini kinachosababisha mateso yao na kuwawezesha kuchukua hatua, alfafanua. Ikiwa watu mahalia wanaelewa kinachoendelea, wanaweza kusimama kidete na kusema: 'Inatosha na itakoma.

Watawa  wanaongoza majadiliano kuhusu mazingira
Watawa wanaongoza majadiliano kuhusu mazingira

Kwa upande wake alikubali kwamba watawa kwa hiyo wanaongoza mapinduzi ambayo sio ya bunduki, sio mapinduzi ya silaha, lakini ni mapinduzi katika vitendo vidogo. Wanataka watu wajue kinachoendelea kwao na kwa hivyo kuelewa, kwanza kabisa, na kisha kuchukua hatua, hatua ambayo inaweza kuleta mabadiliko. Na hato kwa hakika ndio mapinduzi tunayoongoza. Sr. Maamalifar alisisitizia mfano uliotolewa na Papa Francisko kwamba “Mtu huyo ni msukumo kwake binafsi, na anaweza kusema kuwa yeye ni msukumo kwa watu wote wa dini kwa sababu shauku yake na matendo yake, sio tu ya kuzungumza, bali anatenda na hili ndilo wanalohitaji kuona kwa viongozi! Kwa kuhitimsha alisema kwamba: “Hakuna kitakachonizuia, kwa sababu haachi. Haachi katika umri wake katika hali yake. Kwa hivyo ni nini kinapaswa kunizuia?”, alihitimisha.

19 April 2023, 14:41