Kenya:Timu za upekuzi ambazo zinafyeka kichaka imebainisha kuwa iko tayari kuongeza idadi ya miili iliyopatikana. Kenya:Timu za upekuzi ambazo zinafyeka kichaka imebainisha kuwa iko tayari kuongeza idadi ya miili iliyopatikana.  (AFP or licensors)

Kenya:mjadala kuhusu mauaji ya waamini wa madhehebu fulani

Kwa kukabiliwa na kuenea kwa makanisa mapya ambayo mara nyingi yanaanzishwa na wahubiri wa kushitukiza bila taaluma yoyote ya kina ili kuwaongoza waamini,viongozi wa kidini nchini Kenya wameomba taasisi za Serikali kuanzisha tena mjadala juu ya udhibiti wa vikundi na taasisi za kidini.Hivi karibuni wamekuta watu wamekufa kwa njaa

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Mauaji ya Shakaola huko Kenya ambapo watu 110 walikufa kwa njaa kwa amri ya kiongozi wa ibada yao kwa “kulazimishwa kufunga ili kumwona Yesu”. Wengi  wao wanaweza hata kuwa wameuawa kwa ajili ya kuchukuliwa mali zao. Miongoni mwa waathirika  pia ni watoto, ambao mama zao walikuwa wamemfuata nabii wa uwongo. Kwa hiyo katika taarifa iliyotolewa tarehe 3 Mei 2023 na Shirika la Habari za Kimisionari Fides, ilibainisha kuwa: “Sio tu watu waliokufa kwa njaa bali pia baadhi ya waathriwa wa mauaji, miongoni mwa wafuasi zaidi ya 100 wa dhehebu fulani la Kenya, waliopatikana wamekufa katika msitu wa Shakahola, mashariki mwa Kenya, kwenye kaunti ya Kilifi karibu na mji wa Malindi. Tangu tarehe 21 Aprili 2023, mamlaka ya Nairobi imekuwa ikiokota miili iliyozikwa kwa haraka katika makaburi ya halaiki. Katika vyumba vingine walipata familia nzima na wazazi wamezikwa karibu na watoto wao. Timu za upekuzi ambazo zinafyeka kichaka hicho imebainisha kuwa iko tayari kuongeza idadi ya miili iliyopatikana”.

Mchungaji wa Uongo Paul Mackenzie aliyekuwa drevawa Taxi na kuanzisha kanisa lake
Mchungaji wa Uongo Paul Mackenzie aliyekuwa drevawa Taxi na kuanzisha kanisa lake

Askofu Mheria:Dini haiwezi na haipaswi itumiwe kusababisha kifo

“Dini haiwezi na haipaswi kuwa sababu ya watu kupoteza maisha. Pia ni makosa kuamini kwamba watu wanapaswa kufanya mambo ya kipekee ili kupata baraka”, alitoa maoni yake Askofu Mkuu Anthony Muheria, wa Jimbo Kuu Katoliki Nyeri nchini Kenya.  Na kwa upande wa Askofu Mkuu Martin Kivuva Musonde, wa jimbo Kuu katoliki la Mombasa, na pia Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kenya, katika taarifa yake kuhusiana na tukio hilo ovu alisema:  “Tunalaani vikali mahubiri ya ibada yaliyoratibiwa na mchungaji huyo... aliyewaongoza wafuasi wake kufunga hadi kufa”.

'Ushawishi wa kufunga hadi kufa ili kukutana na Yesu'

Wengi wa waathiriwa walishawishiwa kufunga hadi kufa kwa dhana ya  "kukutana na Yesu na Mchungaji Paul Mackenzie Nthenge wa Kanisa la  “Good News International Church”, yaani Kanisa la Habari Njema Kimataifa”. Mackenzie ni dreva wa Taxi ambaye alikuja kugeuka mchungaji na mwinjili wa televisheni mnamo mwaka wa 2003, ambaye kuhubiri kwake kupita kiasi kumemfanya akamatwe mara kadhaa tangu 2017. Kati ya uchunguzi  wa miili 30 iliyopatikana, wengi wa watu wanaonekana kufa kwa njaa, lakini katika kesi kama mbili watoto walikufa kutokana na kukosa hewa, na sio kwa kukosa chakula. Hata kabla ya kufanya uchunguzi wa maiti, polisi na waendesha mashtaka walisema pamoja na watu hao kufariki kwa njaa, huenda baadhi ya wamini wa dhehebu hilo walinyongwa, kukosa hewa au kupigwa na vitu butu hadi kufa. Baadhi ya wahanga hao wametoweka kwa miaka mingi kwa  familia zao. Wengi wap  wanatoka Kenya, lakini kuna wengine wanatoka Tanzania na Nigeria.  Kwa maana hiyo vyombo vya madola  vya Serikali kwa upande wa haki imetangaza kuwa itawashtaki watu 18 kwa ‘ugaidi, akiwemo Mackenzie.

Kuna zaidi ya makanisa 4,000 nchini Kenya yaliyosajiliwa

Nchini Kenya kuna zaidi ya makanisa 4,000 yaliyosajiliwa na karibu 85% ya wakazi milioni 53 ni Wakristo. Zaidi ya milioni 11 ni Wakatoliki, waliogawanyika  katika majimbo 26. Kwa kukabiliwa na kuenea kwa makanisa hayo mapya ambayo mara nyingi yanaanzishwa na wahubiri wa kushitukiza bila taaluma yoyote ya kina ya  kuwaongoza waamini  hadi kuishia pabaya, viongozi wa kidini wa Kenya wameomba taasisi  za Serikali kuanzisha mjadala juu ya udhibiti wa vikundi na taasisi za kidini.

Wachungaji wa uongo chini Kenya wasababisha vifo zaidi ya 100

 

04 May 2023, 16:56