Masalia ya Mwenyekeri Acutis yatakuwa nchini Ireland. Masalia ya Mwenyekeri Acutis yatakuwa nchini Ireland. 

Masalia ya Mwenyeheri Carlo Acustis yatakuwa Ireland

Tunafurahi kwamba masalio ya Mwenyeheri Carlo Acutis yanaweza kufika Ireland kwa sababu tunasadiki,kutokana na uzoefu wake kwamba kwa kujitole kijana huyo kuishi Injili,ni mfano na msaada kwa Kanisa na vijana wengi ambao wanatafuta vidokezo vya kufahamu uzuri wa imani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Askofu Domenico Sorrentino wa jimbo la Assisi – Nocera Umbra – Gualdo Tadino na  Foligno katika matazamio ya hija ya masalia ya kijana Mwenyeheri Carlo Acustis yanayotarajiwa kuanzia tarehe 11-15 Mei katika Jimbo Armagh, Down  na  Connor nchini Ireland amesema: “Tunafurahi kwamba masalio ya Mwenyeheri Carlo Acutis yanaweza kufika Ireland kwa sababu tunasadiki, kutokana na uzoefu wa hapo awali, ambao  kwa kijana huyu, alijitolea na ambaye aliishi Injili kuwa ni mfano na msaada kwa Kanisa na vijana wengi ambao wanatafuta vidokezo vya kufahamu uzuri wa imani.

Askofu Domenico Sorrentino
Askofu Domenico Sorrentino

Kwa mujibuwa taarifa kutoka Jimbo hilo atakayesindikiza kipande cha pericardium yake, yaani Kiungo cha utando ambacho, kama gunia, hufunika na kulinda moyo na mishipa mikubwa ya moyo, atakuwa Monsinyo Anthony Figueiredo, mhusika wa Mahusiano ya Kimataifa.

Mwenyeheri Carlo Acutis alikuwa Gwiji wa Intaneti
Mwenyeheri Carlo Acutis alikuwa Gwiji wa Intaneti

Mwenyeheri Carlo Acutis, ambaye angesherehekea miaka 32 ya maisha yake, tarehe 3 Mei  2023, alikufa kutokana  ugonjwa wa  saratani ya damu akiwa na umri wa miaka 15 tu  mnamo mwaka 2006, na  aliweka maisha yake yote  hasa kwenye Ekaristi ili kukua katika uhusiano wake na Yesu. Akifafanua katika shara lake anaandika kuwa: “Tunapopokea zaidi Ekaristi, ndivyo tutakavyokuwa kama Yesu zaidi”.

Kiini cha Maisha yake ilikuwa ni kuabudu Ekaristi
Kiini cha Maisha yake ilikuwa ni kuabudu Ekaristi

Carlo Acutis kwa hiyo alijaribu kuhudhuria Misa kila siku na kutumia muda katika Kuabudu, akiamini kwamba “tunapojikuta mbele ya Yesu katika Ekaristi, tunakuwa watakatifu. Kutokana na tukio hilo hata hivyo linaturejesha kwamba Masalio ya Mwenyeheri Carlo Acutis tayari yameheshimiwa mnamo mwaka 2022 katika Jimbo la  Marekani, kisha mnamo Novemba 2022 huko Poland na hivi karibuni yalikuwa kwenye  Upatriaki wa Venezia Italia. Kwa hiyo kwa kiangazi hiki  hasa wakati  siku ya Vijana Duniani WYD huko Lisbon  Mwenyeheri Carlo atakuwa  mmoja wa wasimamizi wenza na wa siku hiyo na  masalio hayo yatatembelea majimbo ya  Brazil.

Hija ya Masali ya Mwenyeheri Carlo Acutis huko Ireland
04 May 2023, 14:59