MARIA LIA ZERVINO na MONICA SANTAMARINA,rais mpya wa WUCWO MARIA LIA ZERVINO na MONICA SANTAMARINA,rais mpya wa WUCWO 

Monica Santamarina ni rais mpya wa WUCWO

Shirikisho la Umoja wa Wanawake Wakatoliki Duniani,WUCWO limemchagua Rais wao.Mama mjane wa watoto 4 na bibi wa wajukuu 8.Uchaguzi ulifanyika huko Assisi wakiwa katika Mkutano 14-20Mei:Tutaendelea kutembea kuelekea taaluma ya Dunia.Umoja wa Mashirika wanawake wa Kikatoliki katika masuala ya fedha,uongozi,kamati na vikundi vya kazi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Monica Santamarina wa Mexico, mweka hazina mkuu wa zamani, ndiye rais mpya wa Shirikisho la Umoja wa Wanawake Wakatoliki Duniani (WUCWO, UMOFC),  shirika la kimataifa lililoanzishwa mnamo mwaka 1910, lililopo katika nchi zipatazo 60 ambazo takribani taasisi mia moja za wanawake wa kikatoliki zinamiliki, na  kwa ujumla ya takriban wanawake milioni nane waliwakilishwa katika Mkutano wao. Uchaguzi wa rais mpya ulikuja mwishoni mwa Mkutano Mkuu ambao ulifanyika huko Assisi kuanzia tarehe 14 hadi 20 Mei 2023, ukiongozwa na mada “Wanawake wa WUCWO, mafundi wa udugu wa kibinadamu kwa amani duniani”. Tukio hilo lilileta pamoja wawakilishi kutoka pande zote za dunia, kwa lengo la kushughulikia changamoto za kimataifa na kuchambua nafasi ya msingi ya wanawake katika kukuza amani. 

Wajumbe wa UMOFC,WUWCO
Wajumbe wa UMOFC,WUWCO

Katika zaidi ya mashirika 67 kutoka sehemu mbalimbali za dunia yalihudhuria mkutano huo yakiwa na jumla ya washiriki 832 kutoka nchi 38 katika mabara yote. Kwa hiyo, mwisho wa mkutano huo, uchaguzi wa viongozi wakuu kuanzia na Rais Santamarina, ambaye ni mama mjane, mwenye  watoto wanne na Bibi wa wajukuu nane, mshauri wa zamani wa kisheria na mwalimu na alikuwa mshauri wa masuala ya kijamii katika Taasisi ya Kitaifa ya Wanawake nchini Mexico na mwanachama wa Umoja wa wanawake Katoliki nchini Mexico na aliwahi kuwa rais wa Umoja huo nchini mwake  tangu 1996 hadi 2001.

Wanawake kutoka mabara yote wakatoliki walifika Assisi
Wanawake kutoka mabara yote wakatoliki walifika Assisi

Santamarina na wenzake watawakilisha shirikisho hili kwa miaka minne ijayo, yaani kuanzia 2023-2027.  “Asante kwa uaminifu wa kunichagua kama mgombea”, alisema. Tutaendelea kwa kuunganisha mema yote ambayo yamefanyika ambayo yamekuwa mengi na tutaendelea kuelekea kwenye taaluma ya WUCWO, UMOFC, katika masuala ya fedha, Sekretarieti, mihimili ya uongozi, kamati na vikundi vya kazi”, aliendelea Santamarina, akielezea baadhi ya vipaumbele vya shirikisho lao, akianza na vijana ambao anatarajia kukuza mazungumzo kati ya vizazi. Rais pia alieleza kuwa anakusudia kufanya kazi ili shirikisho la  wanachama liwe vifaa muhimu vya kutekeleza maazimio sita (maeneo ya kuingilia kati) yaliyoidhinishwa na Mkutano wao mkuu.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UMOFC,WUWCO
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UMOFC,WUWCO

Moja ya vipaumbele vya WUCWO, UMOFC itakuwa ujumuishaji na ukuaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Uangalizi wa Wanawake, ambayo inataka kusikiliza na kutoa uonekano wa mateso na uwezo wa wanawake, hasa walio hatarini zaidi, ili kukuza vitendo kwa niaba ya maendeleo yao fungamani ya familia zao na jamii zao. Azimio jingine linahusu utetezi wa uhuru wa kidini kama haki  msingi ya binadamu kwa ajili ya kukuza udugu na amani. Mashirika yanayoshiriki yanaahidi kufanya kazi kwa kutobagua, kukemea ukiukwaji wa uhuru wa kidini na kuendeleza mwingiliano wa dini mbalimbali. Mgogoro wa chakula duniani, unaohusishwa na utunzaji wa sayari yetu, ulikuwa mada ya azimio lingine lililopitishwa wakati Mkutano mkuu. Wanawake wa UMOFC wamejitolea kuitikia wito wa haraka wa kuchukua hatua wa waraka wa Laudato si', kushughulikia masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Ngoma za Kiutamaduni katika Mkutano Mkuu wa WUWCO
Ngoma za Kiutamaduni katika Mkutano Mkuu wa WUWCO

Shughuli zinazolenga kuchakata tena, kupunguza uchafuzi na kuhamasisha  ubadilishaji wa ikolojia. Ahadi zaidi inahusu usindikizaji na malezi ya vijana na wanandoa katika njia ya upendo wa kifamilia, kutambua umama na baba kama njia za utakatifu. UMOFC itaitikia mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wa kujenga mustakabali na wahamiaji na wakimbizi, wakijitolea kuwa vyombo hai vya ukaribu thabiti. Uangalifu hasa utatolewa kwa tatizo la uhamiaji wa kulazimishwa na ubaguzi katika soko la ajira, ambalo linaathiri zaidi wanawake. Zana za usaidizi zitawekwa ili kukabiliana na changamoto hizi.

Mkutano Mkuu wa UMOFC
Mkutano Mkuu wa UMOFC

Hatimaye, WUWCO,  UMOFC inapenda kuendeleza malezi ya wanawake ili waweze kushiriki kwa uwajibikaji katika mchakato wa ujenzi na maamuzi ya Kanisa. Lengo ni kuhimiza uongozi wa kike katika kutafuta manufaa ya wote kwa njia ya malezi ya kiroho, kiakili na kichungaji. Muungano unajitolea kumuunga mkono Rais Santamarina katika mamlaka yake na kushirikiana kikamilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa wakati Mkutano Mkuu . Shirika hilo litaendelea kuendeleza uwezeshaji wa wanawake wa kikatoliki duniani kote, kushughulikia changamoto zilizopo na kufanyia kazi mustakabali wa amani, haki na mshikamano, alisisitiza Santamarina, Rais mpya wa  Shirikisho la Umoja wa Wanawake wakatoliki duniani(WUWCO).

Rais Mpya wa Shirikisho la Umoja wa Wanawake Katoliki duniani
23 May 2023, 15:26