Bikira Maria wa Rosari huko Pompei, Italia. Bikira Maria wa Rosari huko Pompei, Italia. 

Tanzania,Pd.Kyaruzi:Tusali Rozari kwa ajili ya wakosefu&kumkimbilia Bikira Maria

Lazima tubaki imara kwani tunajua yeye ndiye msaidizi wetu na Roho Mtakatifu atakaa kwetu kama tutatimiza amri za Mungu.Kristo anatuunganisha katika amri ya mapendo,tupendane,tukiishi maisha ya upendo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na tukumbuke kusali Rosari.Alisema Padre Kyaruzi,Paroko wa Kagondo,Bukoba-Tanzania.

Na Patrick Tibanga,- Radio Mbiu-Bukoba,Tanzania

Wakristu wametakiwa kumtukuza na kumhimidi Mungu kwa makuu anayoyatenda na kutumia vizuri karama walizojaliwa na Mungu pamoja na kuwa na upendo kwa jirani zao. Hatuo yametolewa na Padre Medericus Kyaruzi Paroko wa Parokia ya Kagondo  wakati wa homilia yake katika Dominika ya 6 ya Pasaka, tarehe 14 Mei 2023 katika Kigango cha Mayondwe, Parokia ya Kagondo,  Jimbo Katoliki la Bukoba Tanzania. 

Mwimbie na mwimidi Bwana kwa sauti aliyokupatia

Padre Kyaruzi katika mahubiri hayo alisema kuwa kila mkristo anatakiwa kuutambua ukuu wa Mungu kwa yote anayowajaalia ikiwemo sauti na kuhubiri ukuu wake na kuyatangaza makuu yake. “Tumepewa na kujaliwa mengi na Mungu, kila mmoja wetu amejaliwa sauti ya kuimba, uwezo wa kusema na kuhubiri, tunahubiri ukuu wa Mungu na kuyatangaza matendo yake kwa sauti ya kuimba, mwingine anasema siwezi kuimba kwa sauti yangu mbaya, hiyo hiyo ndio Mungu kakupa, mwimbie na umwimidi yeye,” alisema Padre Kyaruzi.

Tubaki imara na msaidizi ni Roho Mtakatifu

Kwa kuendelea na mkazo zadi Padre Kyaruzi aidha amewataka waamini kuishi amri kuu ya mapendo kwa kudumisha upendo, kuweka nia pamoja na kusaidiana katika mambo mbali mbali ili Roho Mtakatifu aweze kuwashukia, nao kuwa karibu na Mungu, kuyaishi maisha ya sala na kubaki imara katika imani na kumtanguliza Kristo. “Lazima tubaki imara kwani tunajua yeye ndiye msaidizi wetu na Roho Mtakatifu atakaa kwetu kama tutatimiza amri za Mungu, Kristo anatuunganisha katika amri ya mapendo kwahiyo tupendane, tukiishi maisha ya upendo kwakuwa kitu kimoja, kuweka nia pamoja na kusali pamoja daima Roho Mtakatifu atashuka kwetu,” alisema Paroko huyo.

Mkesha wa Sala huko Fatima tarehe 13 Mei 2023
Mkesha wa Sala huko Fatima tarehe 13 Mei 2023

Kwa kuhitimisha mahubiri yake Padre Kyaruzi aliwahimiza  waamini kusali Rozari Takatifu na kuwaombea wakosefu pamoja na kumkimbilia Mama Bikira Maria na kuuombea ulimwengu wote kupitia Rozari Takatifu.  Ni katika fursa ambayo Mama Kanisa alikuwa akikumbuka tokeo la Bikira Maria huko mlima wa Ria nchini Ureno mnamo tarehe 13 Mei 1917 alipowatokea watoto watatu: Francis, Lucia na Yasintha Malto. Katika fursa hiyo, aliyemwakilisha Papa Francisko ni Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin. Kwa hiyo katika mahubiri Padre Kyaruzi alisema: “Huu ni mwezi wa Mama Maria, aliwapotembelea watoto wa Fatima, aliwaambia tusali Rozari, tuwaombee wakosefu, tuombee amani na kuwaombea wale wote wasiomwamini Mungu, kwa hiyo tusali Rozari takatifu katika familia zetu na tupeleke furaha kama Bikira Maria alivyomtembelea ndugu yake Elizabeth, na hivyo tumkaribishe Kristo katika familia  na maisha yetu kwani kwa kuwakaribisha hao, Roho Mtakatifu atatuletea furaha, mapendo, unyenyekevu na utu wema.”

Mama Maria wa Fatima: Hija ya Papa mnamo 12 Mei 2017
Mama Maria wa Fatima: Hija ya Papa mnamo 12 Mei 2017
16 May 2023, 13:19