Tafuta

Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, Burkina Faso. Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, Burkina Faso. 

Burkina Faso:Maaskofu wanaomba amani

Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu lakini pia ni matunda ya juhudi za kibinadamu,amekumbusha hayo Kadinali Ouédraogo,wa Burkina Faso katika nchi iliyoharibiwa na vurugu za magaidi. Ni wakati wakihitimisha mkutano wao mnamo Mei, 20.Na wakati huo huo,takriban watu 40 waliuawa katika mashambulizi ya wanajihadi nchini Burkina Faso tarehe 27 Mei 2023.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Afrika Magharibi (CEREAO/RECOWA) waliomba amani na kuombea magaidi waongoke. “Mungu aguse mioyo yao. Maombi haya lakini sio Burkina Faso pekee. Hii ni kwa ajili ya Nigeria, Mali, Niger na nchi zingine zote za Kiafrika ambazo zimefichwa kutoka katika uangalizi wa vyombo vya habari lakini zinakabiliwa na vurugu za watu waovu,” na kwa hiyo walisihi ombi lao wakati wa mkutano wao uliofanyika  tarehe 20 Mei  2023 huko Ouagadougou. Maaskofu wa Burkina Faso walisali kwa ajili ya nia hiyo maalum wakati wa misa ambayo iliwekwa mwisho wa siku ya kitaifa ya kufunga na kuombea amani na mshikamano wa kijamii. Askofu mkuu wa Ouagadougou, Kardinali Philippe Ouédraogo, alisisitiza kwamba: “Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu; amani pia ni matunda ya juhudi za kibinadamu”, akiwataka watu wa Mungu nchini Burkina Faso “kuungana na sauti zao kumwomba Mungu neema ya amani”.

Ghasia ukanda wa sahel

Takriban watu 40 waliuawa katika mashambulizi ya wanajihadi nchini Burkina Faso mnamo  Jumamosi tarehe 27 Mei 2023. Hii ilitangazwa na mamlaka mahalia  kulingana na ambayo wanabainisha kuwa wanachama 20 wa wanamgambo wa hiari wanaounga mkono jeshi (VDP Volontaires pour la Défense de la Patrie), waliuawa huko Bourasso katika Mkowa  Kossi, karibu na mpaka na Mali, na Watu wengine 20 walipoteza maisha katika mkoa huo siku ya Dominika tarehe 28 Mei 2023. Wakati wa shambulio la Jumamosi kwenye Kambi ya Wanamgambo hao (VDP), jeshi la wanahewa liliingilia kati na kuwapiga magaidi hao na kuua takriban thelathini kati yao, kulingana na msemaji wa jeshi hilo.

Tangu 2015 Burkina Faso inakosa usalama 

Hata hivyoi ni tangu mwaka wa 2015, nchini Burkina Faso imekuwa ikiishi kwa ukosefu wa usalama kutokana na ghasia zinazofanywa na makundi mbalimbali yenye silaha, baadhi yao yakiwa na mafungamano na Al Qaeda au Serikali ya Kiislamu. Makundi hayo ya kijihadi ni ya kimataifa, yanafanya kazi pamoja na Burkina Faso, nchini Mali na Niger.

Waziri Mkuu alitangaza mapambano na ugaidi tarehe 30 Mei

Waziri Mkuu wa Burkina Faso Kyélem de Tambèla alitangaza tarehe 30  Mei kwamba hana nia ya kukabiliana na magaidi. “Haiwezekani sisi kujadiliana na wasio wa kawaida (...). Hatutawahi kujadiliana, wala uadilifu wa eneo la Burkina Faso, wala mamlaka yake. Tutatetea eneo letu na wakazi wetu kwa gharama yoyote ile,” alisema Kyélem de Tambèla katika hotuba yake kwa Bunge la Mpito la Kutunga Sheria ambapo pia alitarajia kuleta idadi ya VDPs kutoka 50,000 hadi 100,000.

01 June 2023, 15:02