Patriaki Clementa:WYD Lisbon,litakuwa tukio la kizazi!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Siku ya Vijana Duniani inayokuja itakuwa ni fursa ya kipekee ya kukaribisha na kujitangaza ulimwenguni kwa Lisbon na Ureno. Hayo yamesemwa na Kardinali Manuel Clemente, Patriaki wa mji huo, katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuwasilisha ratiba ya ziara ya Papa Francisko katika mji mkuu wa Ureno kuanzia tarehe 2 hadi 6 Agosti 2023 iliyotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican.
Mchakato wa maandalizi ulianza mwaka 2017
“Hatuwezi kukosa fursa hii”, alisisitiza Patriaki huyo ambaye, kama ilivyoripotiwa na Shirika la Kikanisa, alikumbuka mchakato wa safari ya maandali iliyoanzishwa na jiji na Kanisa mahalia kuanzia 2017, wakati Lisbon ilitoa nia yake ya kuandaa tukio hilo. Ni mchakato wa safari ambao ulihusisha makumi ya maelfu ya watu waliunganisha ulimwengu wa Kikatoliki na taasisi za Ureno ili kuwakaribisha vijana watakaowasili kutoka katika sayari nzima. Hakuna kitu kingine zaidi ya kizaji kama hicho ulimwenguni alisisitiza Patriaki Clemente, akitumaini kuwa mahujaji watakaribishwa katika mazingira ya familia, katika tukio ambalo itaashirikisha kizazi. Kwa hakika, watakuwa wahusika wakuu wa siku zijazo, kwa maana ya jumuiya ya kiekumeni zaidi, inayounga mkono zaidi, na ya kindugu zaidi
Meya: Mahujaji milioni moja wanatarajiwa
Furaha kubwa kwa juhudi ambayo kila mtu atajitolea masaa 24 kwa siku pia ilioneshwa na meya wa Lisbon Bwana Carlos Moedas, kazi katika Uwanja wa Tejo ambapo mkesha wa vijana na Papa utafanyika jioni ya tarehe 5 Agosti 2023 na Misa Takatifu Dominika asubuhi tarehe 6 Agosti, imekamilika na itawasilishwa kwa umma tarehe 10 Juni 2023 alisema Meya wa Jiji la Lisbon huku akiongeza kuwa madhabahu ambayo itakuwa mwenyeji wa sherehe za mwisho itakamilika ifikapo tarehe 9 Julai 2023. “Ilikuwa kazi isiyo ya kawaida. Lakini tuko tayari”, alisisitiza tena, akitarajia uwepo wa mahujaji zaidi ya milioni. Lisbon itakuwa jukwaa la ulimwengu,” alisema meya, akiwaalika “vijana kuwa mabalozi wa jiji , kwa kujiandikisha na Manispaa na familia ili kufungua nyumba zao na kuwakaribisha.”
Mnamo tarehe 3 Agosti, mkutano na wanafunzi wa chuo kikuu na Papa
Miongoni mwa mikutano ya Papa, ambaye mnamo tarehe 5 Agosti pia atakwenda kwenye Madhabahu ya Maria wa Fatima, pia wale walio na wakimbizi na wakazi wa mpango wa makazi ya kijamii, pamoja na mamlaka ya kisiasa na wawakilishi wa mashirika ya kiraia. Tarehe 3 Agosti, alikumbuka Askofu Américo Aguiar, askofu msaidizi wa jiji hilo na rais wa Mfuko wa Siku ya Vijana (WYD) Lisbon 2023, Papa Francisko atakutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ureno juu ya mada: ‘ikolojia fungamani’, ‘udugu wa binadamu’, ‘Uchumi wa Francesco’ na ‘Mkataba wa Elimu ya Ulimwenguni’.