Tafuta

Mkutano Mkuu wa 44 wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki Tanzania, WAWATA Taifa, kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Juni 2023 Mkutano Mkuu wa 44 wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki Tanzania, WAWATA Taifa, kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Juni 2023  

Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa WAWATA, Bagamoyo! Kumekucha!

Mkutano Mkuu wa 44 wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki Tanzania, WAWATA Taifa, kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Juni 2023 katika hotuba yake amekazia kuhusu: Lengo msingi la WAWATA, Hija ya kiroho nchini Misri, Israeli na Yordan; umuhimu wa malezi na makuzi ya kifamilia; majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduniani; maridhiano katika familia, mahusiano na mafungamano ya udugu wa kibinadamu mkutano mkuu wa 44 wa WAWATA Kitaifa.

Na Mama Evaline Malisa Ntenga, Bagamoyo, Pwani, Tanzania.

UTANGULIZI: Mheshimiwa Padre Florence Rutaihwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kichungaji, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kama sehemu ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki Tanzania, WAWATA Taifa, kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Juni 2023 katika hotuba yake amekazia kuhusu: Lengo msingi la WAWATA, Hija ya kiroho nchini Misri, Israeli na Yordan; umuhimu wa malezi na makuzi ya kifamilia; majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduniani; maridhiano katika familia, mahusiano na mafungamano ya udugu wa kibinadamu mkutano mkuu wa 44 wa WAWATA Kitaifa. Naye Mama Evaline Malisa Ntenga, Mwenyekiti WAWATA, Taifa na Rais wa Wanawake Wakatoliki Afrika amegusia kuhusu Jubilei ya Miaka 50 ya WAWATA, Semina zinazotolewa na kwamba, Siku ya Jumapili baada ya Ibada ya Misa Takatifu watahitimisha mkutano kwa kuandaa mpangokazi wa kila kanda, vipaumbele vya Taifa 2023-2026 na ikiwezekana kukamilisha mpangokazi wa Taifa kwa kipindi cha 2023/2024. Wanawake Wakatoliki Wajenzi wa Mahusiano ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ulimwengu wa Amani: “WUCWO Women, Artisans of Human Frartenity for the World Peace.”

Wajumbe wa Mkutano Mkuu 44 wa Uchaguzi WAWATA, Taifa 2023
Wajumbe wa Mkutano Mkuu 44 wa Uchaguzi WAWATA, Taifa 2023

Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya akina mama wote kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na afya njema na kwa huruma yake kutuwezesha kukutana tena leo tarehe 9 Juni 2023 toka tulipoachana kama wajumbe wa mkutano mkuu 12/09/2022 baada ya Jubilei ya miaka 50. Namshukuru Mungu kwa namna ya pekee kwa zawadi ya neema ya kutufanya sehemu ya utumishi katika kanisa lake hapa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania. Nafasi hii ya upendeleo itusaidie kuendelea kutakatifuza Malimwengu, tukianza na sisi wenyewe ili mwisho tupate taji tuliyoandaliwa mbinguni. Nawapa pongezi nyingi sana kwa kutenga muda kufika hapa ili tuendelee kuimarishana, kupata marafiki wapya na kushirikishana uzoefu na changamoto za kumtumikia Mungu, hongereni sana. Naomba nimkumbushe ambaye hajapata nafasi ya kumshukuru Mungu kwa namna ya pekee kwa kupata upendeleo kuwepo kati ya ninyi ambao Mungu amewapendelea kumtumikia kwa kipindi cha mwaka 2023-2026 ajitahidi kufanya hivyo wakati huu wa mkutano kabla hajarejea jimboni kwake. Ni muhimu sana kushukuru na ndio namna bora zaidi ya kuomba maongozi ya Mwenyezi Mungu katika safari mtakayoianza pamoja leo. Punga mkono kama umenielewa!! Tutaanza mkutano wetu kwa semina ambayo wakufunzi ni Wakurugenzi wetu Pamoja na Padre Almacheus Rwejuna ambae anamuwakilisha Katibu Mkuu. Lengo ni kuhakikisha tunatembea pamoja. Ninawashukuru sana wakurugenzi wetu kwa kuitikia ombi la kutuandaa mama zenu ili tunaporejea katika majimbo yetu tuwe tumenolewa vizuri.

WAWATA wakiwa kwenye hija Nchi Takatifu, Msiri na Yordani
WAWATA wakiwa kwenye hija Nchi Takatifu, Msiri na Yordani

Mada zitakazotolewa ni: Uongozi ndani ya Kanisa Katoliki ni mada inayotolewa na Padre Leonard Samson Maliva. Mada ya Pili ni Mwanamke Mkatoliki inatolewa na Padre Richard Stanslaus Mbuya Na mada ya Tatu ni: Zaka na Sadaka ni tema inayonogeshwa na Padre Adeodatus Mutangira Rwehumbiza. Na mada ya Nne ni Malezi ya Famili inayotolewa na Padre Dr. Charles Kitima, Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC. Naomba tuwe wasikivu, tuulize maswali na tutakaporejea majimboni tukawashirikishe waliotutuma. Tunao wanahabari hapa kutoka Jugo Media, karibuni sana na ahsanteni sana kwa kendelea kuinjilisha kwa njia ya mtandao. Tunaamini yale tutakayojifunza yatawafikia wengi zaidi kupitia vyombo vyenu vya mawasiliano. Kwa haraka haraka, leo tutakuwa na semina na jioni baada ya chai tutakutana kwa ajili ya Halmashauri ya Utekelezaji, kujiandaa na mkutano mkuu wa kesho. Ratiba ya Jumamosi tarehe 10 Juni 2023 ni kujadili ripoti ya utekelezaji ambayo ilitumwa kwenu takribani wiki mbili zilizopita, tutapokea taarifa kutoka majimboni na kadiri ya muda, uchaguzi baada ya chai ya jioni. Siku ya Jumapili baada ya misa tutahitimisha kwa kuandaa mpangokazi wa kila kanda, vipaumbele vya Taifa 2023-2026 na ikiwezekana kukamilisha mpangokazi wa Taifa kwa kipindi cha 2023/2024.

Jubilei ya Miaka 50 ya WAWATA, Tanzania
Jubilei ya Miaka 50 ya WAWATA, Tanzania

Naye Mheshimiwa Padre Florence Rutaihwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kichungaji, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kama sehemu ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 44 wa Uchaguzi wa WAWATA Taifa, kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Juni 2023 katika hotuba yake amekazia umuhimu wa malezi na makuzi ya kifamilia. WAWATA kama vyombo vya huruma na upendo; utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote kama kielelezo cha utekelezaji wa Waraka wa Kityume wa Baba Mtakatifu Francisko wa “Laudato si” yaani “Sifa iwe kwako” juu ya utunzaji wa nyumba ya wote” unagusia kuhusu: Mambo yanayoendelea kujiri katika mazingira; Injili ya Kazi ya Uumbaji na Amani; Vyanzo vya mgogoro wa Ikolojia na watu; Ikolojia ya mazingira, uchumi na jamii. Njia za kupanga na kutenda na umuhimu wa elimu ya ikolojia inayojikita katika wongofu wa ndani, furaha na amani. WAWATA ihakikishe kwamba, inawashirika vijana katika maisha na utume wa Kanisa, mkazo ni WAWATA Chipukizi. WAWATA iwajengee uwezo wanawake wakatoliki Tanzania kiuchumi ili waweze kutekeleza vyema dhamana na majukumu yao kijamii na Kikanisa, ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. WAWATA iendelee kutoa kipaumbele cha pekee kwa ajili ya ulinzi wa mtoto kwa kushirikiana na Serikali.

Padre Florence Rutaihwa akiwa Assisi kwenye mkutano wa wanawake.
Padre Florence Rutaihwa akiwa Assisi kwenye mkutano wa wanawake.

WAWATA waendelee kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni ili kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watanzania, pamoja na kutafuta suluhu ya pamoja kutokana na changamoto mbalimbali zinazoendelea kuibuka katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia. WAWATA iendelee kushirikiana na Serikali katika kushughulikia maridhiano na mafungamano ya kijamii mintarafu familia ambazo leo hii zinakabiliana na changamoto na migogoro mingi kiasi cha kuhatarisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia. WAWATA isaidie kujenga na kudumisha mahusiano na mafungamano ya udugu wa kibinadamu, ili familia ziweze kusimama imara; WAWATA isaidie kushawishi ustahimilivu miongoni mwa jamii pamoja na kuendelea kupambana na tabia na vitendo vya ushoga na usagaji ndani ya jamii. Huu ni mkutano mkuu wa 44 wa WAWATA Taifa, wajumbe waendelee kumwomba Roho Mtakatifu ili awezeshe kutambua lengo la WAWATA yaani kujitakatifuza na kuyatakatifuza malimwengu na wala si vinginevyo! Uongozi ndani ya Kanisa ni huduma kwa watu wa Mungu.

WAWATA Mkutano Mkuu 44
09 June 2023, 15:05