AMECEA,mfululizo wa video fupi:Msukumo wa Uwepo Kamili katika mtandao kijamii!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika video hii, watu kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA)wanashirikisha mawazo yao kuhusu mitandao ya kijamii kwa mtazamo wa Kikristo. Kwa njia hiyo video yenye jina la “Fully Present Inspirations” yaani “Msukumo wa Uwepo Kamili” ni mfululizo wa video fupi ambapo wataalam wa mawasiliano ya imani na watendaji vijana wa vyombo vya habari vya kikatoliki wanashirikisha mawazo yao kuhusu Tafakari ya Kichungaji “Kuelekea Uwepo Kamili”.
Rais wa SIGNIS
Katika mfululizo huo hata Helen Osman ambaye ni mshauri wa Baraza la Mawasiliano la Vatican na Rais wa SIGNIS, Chama cha Kikatoliki cha Mawasiliano Duniani anatoa mtazamo wake kuhusu mitandao ya kijamii kwa mtazamo wa kikatoliki.
Ikumbukwe AMECEA ni Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Wanachama Afrika Mashariki shirikisho linalojumuisha mabaraza ya Maaskofu Katoliki nane ya Afrika Masharikiambazo ni: Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia.