2023.07.21 Baraza la Vijana wa Mediterane huko Firenze umehimitimishwa tarehe 16 Julain 2023. 2023.07.21 Baraza la Vijana wa Mediterane huko Firenze umehimitimishwa tarehe 16 Julain 2023. 

Baraza la Vijana la Mediterania,Cei: ni mkutano wa mashuhuda,sio itikadi

Katika Mkutano wa Baraza la Vijana wa Mediterania,ambao ulikuwa wa kwanza kabisa ulioanzia jijini Roma mnamo Julai 11 na kuendelea huko Firenze tangu Julai 12 hadi 15,ulihitimishwa,Dominika tarehe 16 Julai 2023 kwa kuwachagua hata viongozi kutoka pande za Asia,Ulaya na Afrika.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Vijana wa Mediterania, ambao ulianza jijini Roma mnamo Julai 11 na kisha kuendelea huko Firenze tangu tarehe 12 hadi 15, ulimalizika Dominika tarehe  16 Julai  2023 katika “Villaggio La Vela”  huko Castiglione ya Pescaia (Grosseto). Katika kikao cha mwisho, vijana 34, kutoka nchi 19, wawe wa kutoka Ulaya, hata Afrika na Asia waliridhia Kanuni ya Uendeshaji wa Baraza na walicha wakuu Emile Fakhoury (Lebanon), Maher Dridi (Tunisia), Aleks Birsa Jogan (Slovenia) na Pilar Shannon Perez Brown (Hispania), ambaye pia ni mratibu wake.

Katika siku za kwanza za Septemba mkutano wa kwanza wa bodi utafanyika ambapo, pamoja na waendelezaji, mpango wa kazi utafafanuliwa kwa misingi ya mapendekezo mengi ambayo yamejitokeza katika siku hizi za kwanza za kazi, zilizoelezwa kwa mada nne tofauti. Mkutano utakaofuata wa Baraza utafanyika mtandaoni katika Juma la kwanza la Oktoba 2023. Sherehe ya kuhitimisha ya Ekaristi katika Kanisa la Kijiji cha La Vela ilikuwa muhimu sana, ambapo sala na lugha za kila nchi ya asili zilisikika. Misa hiyo iliongozwa na Padre Paolo Tarchi, ambaye aliandamana na kikundi cha wajumbe vijana kila siku kwa mtazamo wa kiroho.

Tukio lililofungwa katika siku za hivi karibuni huko Firenze Italia lilileta pamoja mada mbili msingi za Baraza la Maaskofu wa Italia: nafasi ya vijana na ukweli wa imani katika bonde la Mediterania. Don Gianluca Marchetti, katibu msaidizi wa Maaskofu wa Italia amesema kuwa Kanisa limechagua kuwasaidia vijana, si kuchukua nafasi zao, bali kuwasaidia kutembea kwa kujitegemea bila hukumu na kufungua nafasi za ubunifu kwa ajili yao. Hatua ya kuwasili ya safari, ishara ya kinabii ya kazi iliyotolewa kwa watoto. Baraza la Vijana la Mediterania, lililoanzishwa na Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI), liliwakilisha fursa kwa vijana wengi kushiriki, kujadiliana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao. Padre Gianluca Marchetti, katibu msaidizi wa Baraza la Maaskofu Italia ( CEI), aliiambia Radio Vaticana juu ya madhumuni ya mkutano huo “Baraza la Maaskofu wa Italia limechagua kujihusisha na shughuli  hii, kwa kuwaamini vijana. Mada ambayo inawakilisha, alisema ni  ufunguzi wa safari “kwa mtindo wa Papa Franciko.

Lazima tushukuru kwanza kwa mikutano mingi ya maaskofu wa nchi zinazopakana na Bahari ya Mediterania", alifafanua Padre Marchetti, akizungumzia hali halisi tofauti,  kutoka kwa Wahispania hadi Wafaransa, akipitia maaskofu wa Kilatini wa mikoa ya Waarabu, kwa ushirikiano na mkutano wa maaskofu wa Malta na Sinodi Takatifu ya Kigiriki -ambayo kupitia umoja wao na shukrani kwa kazi ya Askofu Mkuu wa Italia, aliidhinisha kazi kamili ya Askofu ya uzoefu wa kweli wa sinodi haupaswi kuchukuliwa kuwa rahisi ”. Maelewano ambayo, pamoja na ushirikiano na taasisi za Firenze zilizounganishwa na takwimu ya Giorgio La Pira, kama vile Kituo cha Wanafunzi wa Kimataifa, mfuko wa La Pira na Msingi wa Yohane Paulo II, uliwezesha kuundwa kwa Baraza la Vijana la Mediterania. Taasisi hizi za Firenze, kulingana na katibu mkuu wa CEI, huweka roho ya kinabii ya La Pira, uwazi wa kimataifa na mtindo wa udugu ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu katika eneo hili la kukutana kati ya tamaduni. Mchango wao umekuwa muhimu kusema kidogo.”

Baraza la Vijana wa Mediteranea umehitimishwa.
21 July 2023, 17:23