Tafuta

Kampeni ya Comece,Celam,caritas Lac na Caritas Ulaya!

Ujumbe wa pamoja kutoka kwa COMECE,CELAM,Caritas LAC na Caritas Ulaya,kwa ajili ya mtazamio ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa kati ya Umoja wa Ulaya na CELAC,utakaofanyika huko Bruxelles mnamo tarehe 17-18 Julai 2023.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kampeni ni Mpango wa COMECE na  CELAM, pamoja na  Caritas LAC  na Caritas Ulaya,  ambao wanauepeleka mbele katika matazamio ya Mkutano Mkuu kati ya Umoja wa Ulaya na Shirikisho la kikanda linaloleta pamoja Amerika ya Kusini na nchi za visiwa vya  Karibea(CELAC) utakaofanyika huko Bruxelles mnamo tarehe 17 na 18 Julai.

Kampeni ya kushirikisha ujumbe muhimu kwa viongozi wa kisiasa wa pande zote mbili za Atlantiki

Hii ni kampeni iliyoandaliwa kwa njia ya  video ambayo wawakilishi wa Mashirika hayo  wanashirikisha ujumbe mfupi muhimu kwa viongozi wa kisiasa wa pande zote mbili za Atlantiki ili hatimaye kufanya ushirikiano kati ya kanda hizo mbili kuwa fursa ya amani na ukuaji kwa watu wote wanaohusika. Ujumbe huo katika video  wa kampeni unatolewa na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (COMECE), Askofu Mariano Crociata, wa jimbo katoliki la Latina-Terracina-Sezze-Priverno, Italia na Rais wa  Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Amerika Kusini na Visiwa vya Caribiani ( CELAM),  Askofu Mkuu Jaime Spengler OFM wa Jimbo Kuu la Porto Alegre.

Kanisa linatazamia mkutano Mkuu utakaofanyika wa matumaini makubwa

Aidha kuna hata swali kwamba: Je, Mkutano wa Wakuu wa EU-CELAC unawezaje kuchangia katika ushirikiano wa watu sawa/kukuza haki ya kimataifa? Kwa kuzingatia Mkutano ujao wa EU-CELAC, COMECE na washirika wake waliandaa mjadala wa hadhara uliomlika kwa hakika njia za kufanya Mkutano huo kuwa tukio la kukuza haki ya kimataifa na ushirikiano wa watu sawa.

Mjadala wa maandalizi ya Mkutano Mkuu kati ya Viongozi wa kisiasa na COMECE na CELAC

Tukio hilo lilikuwa fursa ya kushiriki baadhi ya vipengele muhimu vya maono ya Kikatoliki kwa ajili ya ushirikiano mpya kati ya Umoja wa Ulaya na nchi za Amerika ya Kusini na Karibia na pia kuwa na mazungumzo yenye kujenga na wafanya maamuzi wa Umoja wa Ulaya na wadau wengine. Hafla hiyo iliratibiwa kwa pamoja na COMECE, tarehe 6 Julai 2023 na Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini (CELAM), Caritas Amerika Kusini na Karibiani pamoja na Caritas Ulaya.

11 July 2023, 12:51