WYD Lisbon:Vijana 65,000 wa Italia watakuwa katika siku ya vijana
Na Angella Rwezaula,-Vatican.
Katika taarifa kutoka Ofisi ya Kitaifa ya mawasiliano ya kijamii, ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kuhusiana na Tukio la Siku ya vijana duniani ambalo linakaribia, imebainisha kwamba ushiriki wa vijana ni 65,000 wa Italia ambao wanaondoka kuelekea katika Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon, iliyopangwa kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Hao watasindikizwa na maaskofu 106 pamoja na mapadre, watawa wa kike na kiume , waelimishaji na wahuishaji. Katika mji mkuu wa Ureno, ujumbe wa bluu utaonekana ambao unawakilishwa na majimbo 180 utakuwa na nyumba ya Italia ,“Casa Italia”, kama sehemu yake ya kumbukumbu, mahali pa kupata habari na nyenzo, kutatua matatizo, na pia kukutana, kutumia muda pamoja na kubadilishana uzoefu, hata kwa kukaa nyumbani au kwenye mitandao ya kijamii shukrani kwa WIFI bila malipo.
Sekretarieti ya Huduma ya Kitaifa ya Kitengo cha kichungaji cha Vijana ambayo itatoa msaada kwa wale wanaowasindikiza na viongozi wa vikundi, ofisi ya Ubalozi na kituo cha matibabu. Pia watakuwepo wafanyakazi wa Ofisi ya Kitaifa ya Mawasiliano ya Kijamii ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia (CEI )ambao watatoa ripoti kuhusu Siku ya vijana (WYD) kwenye tovuti https://gmg.chiesacattolica.it/ na watasaidia wanahabari wa Italia na waendeshaji vyombo vya habari waliotumwa huko Lisbon. Kukaribishwa kutahakikishwa na watu wa kujitolea wapatao thelathini kutoka Italia yote.
Makao makuu ya rangi Tatu kama Bendera ya Italia huko Lisbon yatazinduliwa na Askofu Giuseppe Baturi, Askofu Mkuu wa Cagliari na Katibu Mkuu wa Baraza la maaskofu Italia (CEI), Dominika tarehe 30 Julai saa 6 Mchaza (saa za Ureno). Ikilinganishwa na mpango rasmi wa WYD, vijana wa Italia watashiriki kuanzia tarehe 2 hadi 4 Agosti katika katekesi zitakazofanywa na Maaskofu katika maeneo ya malazi ya mahujaji. Tarehe 2 Agosti, saa nane mchana (saa za Ureno), Passeio Maritimo de Algés itakuwa mwenyeji wa “Siku Kuu ya Waitalia, ambao utakuwa ni muda wa kushiriki na kutafakari na utatangazwa mbashara na Tv2000 kuanzia saa 3.00 usiku (saa za Kiitaliano). Uzoefu wa timu ya bluu utarekodiwa na Avvenire, Tv2000, InBlu2000 na Shirika la habari Sir na huduma za kujitolea, maalum na za moja kwa moja. Taarifa na sasisho kwa wakati halisi pia kwenye mitandao ya kijamii ya Kitengo cha Vijana na Baraza la Maaskofu wa Italia.
“Ushiriki wa majimbo ambayo yamekuwa yakijiandaa kwa uteuzi huu kwa miezi kadhaa, na ushiriki mkubwa wa vijana unaelezea Kanisa hai na changa kuliko sisi kufikiria. Lisbon itakuwa na uzoefu fulani kwa sababu kadhaa: kwanza kabisa, kizazi ambacho kinashiriki ndani yake, kutokana na masuala ya umri, hakijawahi kupata kitu sawa lakini kinatokana na mateso ya janga; zaidi ya hayo, ni mara ya kwanza kwa mkutano wa dunia wa vijana kufanyika katika bara ambako kuna vita”. Alisema Padre Michele Falabretti, mkuu wa Huduma ya Kichungaji Kitaifa ya Vijana ya Baraza la Maaskofu Italia ( CEI). Kwa kuongezea “Kila WYD ni maabara kubwa: tamaduni tofauti, lugha, asili hufungua moyo kwa uelewa wa kuwepo yenyewe. Toleo hili, hasa, litatumika pia kukuza uaminifu kwa wengine, ufahamu kwamba tunategemeana, kwamba tunahitaji kutambuana kama ndugu na kwamba inafaa kujihusisha. Na kufanya hivyo, kama Papa Francisko ametukumbusha, kwa fumbo hilo la safari ambayo daima iko karibu na wengine na sio peke yetu”.