Askofu Liberatus Sangu na makuhani  wapya wa jimbo la Shinyanga, Tanzania mara baada ya upadrisho wa Padre Sosthenes Ntemi Charles. Askofu Liberatus Sangu na makuhani wapya wa jimbo la Shinyanga, Tanzania mara baada ya upadrisho wa Padre Sosthenes Ntemi Charles. 

Tanzania,Askofu Sangu kwa Sosthenes:Jibidishe kutenda kwa unyenyekevu,utii&upendo

Waamini wakatoliki,Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wameaswa kumuomba Roho Mtakatifu ili awasaidie katika kutenda kazi ya kuhubiri na kutangaza Injili ya Kristo.Hayo yalisemwa na Askofu Liberatus Sangu,Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga wakati wa mahubiri ya Misa ya utoaji wa Daraja la Upadre,tarehe 20 Julai 2023.

Patrick P. Tibanga- Radio Mbiu Kagera.

Mnamo tarehe 20 Julai 2023,  Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania alitoa homilia yake, kwa waamini wakati wa Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya utoaji Daraja Takatifu ya Upadre kwa aliyekuwa Shemasi Sosthenes Ntemi Charles, wa Parokia ya Mtakatifu Luka, Bariadi,  jimboni humo. Katika mahubiri hayo aliwahimiza na kutoa wito kwa Wakristo wote na wenye mapenzi mema kuomba Roho Mtakatifu ili awasaidia kutenda kati ya kuhubiri na kutangaza Injili ya Kristo.

Shemasi Sosthenes kabla ya kupata daraja la upadre
Shemasi Sosthenes kabla ya kupata daraja la upadre

Askofu Sangu katika mahubiri hayo alisema kuwa ukimpokea Roho Matakatifu utampeleka kwa watu wengine kwa upendo, huku upendo huo ukianzia kwa familia, Jumuiya na jamii inayokuzunguka. Vile vile aliwataka wakristo wanapompokea Roho Mtakatifu ili waishi na kumuonesha kwa vitendo kwa watu wanaowazunguka badala ya kuwa  watu wa masengenyo na vitendo ambavyo havimpendezi Mwenyezi Mungu.

Litania ya watakatifu wakati wa daraja la Upadre , huko Shinyanga, Tanzania
Litania ya watakatifu wakati wa daraja la Upadre , huko Shinyanga, Tanzania

Hata hivyo Askofu  Sangu akimgeukia Padre mpya  alimwomba afanye utume wake kwa upendo, huku akimhubiri Kristo, bila kuchoka na wala kukata tamaa, na akiongozwa na Roho Mtakatifu. Hakuishia hapo bali alimtaka Padre mpya Sosthenes Ntemi Charles, kujibidiisha katika kufanya kazi yake ya utume aliyoitiwa na  Mungu kwa unyenyekevu, utii na upendo mkubwa huku akiongozwa na Mungu mwenyewe.

Sala ya kumwombea Shemasi Sosthenes kabla ya daraja la upadre
Sala ya kumwombea Shemasi Sosthenes kabla ya daraja la upadre

Askofu Sangu alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa utume wake ndani ya Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania kwa sababu tangu apewe majukumu rasimi ya kuwa askofu wa Jimbo hilo, amewapadrisha mapadre 33 na kwa idadi hiyo imepelekea kufikia mapdre  kwa saa 78 ndani ya jimbo la Shinyanga.

Askofu Liberatus Sangu baada ya upadrisho wa Padre Sosthenes
Askofu Liberatus Sangu baada ya upadrisho wa Padre Sosthenes

Na hii ni kutaka kuonesha wazi kwamba Mungu anazidi kuita katika shamba lake kubwa  kila wakati ambalo kama alivyowambia wanafunzi wake kuwa: “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. (Mt 9,37-39;  ( Lk 10,2).

Mkumbatio wa kibaba kati ya Askofu Sangu na Padre mpya Sosthenes tarhe 20 Julai 2023.
Mkumbatio wa kibaba kati ya Askofu Sangu na Padre mpya Sosthenes tarhe 20 Julai 2023.

Njoo mnifuate, nitawafanya wavuvi wa watu. Bwana Yesu anasema. Aliyechagua Kristo hana haja ya kutazama nyuma bali ni kumkimbia na kuwaacha wafu wazikwe wafu wao.

 

22 July 2023, 15:00