WYD Lisbon 2023: Kikundi cha vijana Watanzania:kushuhudia upendo wa Kristo
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika Siku ya XXXVII ya Vijana Ulimwenguni (WYD) kwa Mwaka 2023 iko mlangoni kufunguliwa katika Jimbo kuu la Lisbon nchini Ureno, kuanzia tarehe 1- 6 Agosti 2023, ambayo inaongozwa na kauli mbiu: “Maria aliondoka akaenda kwa haraka” (Lk 1:39.) Zikiwa zimebakia saa chache sana kuanza maadhimisho hayo, Radio Vatican imepata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na baadhi ya mahujaji walioko huko Lisbon kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Kwa upande wa mahujaji hawa, wanayo furaha kubwa isiyo na kifani kushirikishana furaha hii ya mkutano na wenzao hasa kupata uzoefu mpya kutoka kwa vijana wanaotoka mataifa mbali mbali, tamaduni, kabila na rika tofauti katika sayari hii.
Hii ni moja ya matukio adimu na ambayo kiukweli yanatoa tafakari kubwa ya maisha ya vijana. Kwa kuongozwa na kauli mbiu ya Siku ya vijana duniani huko Lisbon 2023 ambayo Bikira Maria mara baada ya tangazo la Malaika alikimbia upesi kwenda kumsaidia binadamu yake Elizabeti (Rej. Lk 1,29) na ambaye tayari alikuwa ni mjamzito, inawagusaje mada hii? "Sisi tunataka kufuata nyayo za Maria bila kusubiri na wakati huo huo tukisubiri kwa hamu kubwa ujumbe wa Papa Francisko ambaye hatujuhi atatuleza nini hapa Lisbon”. Alijibu hayo Joseline Kalemera kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Tanzania anayeshiriki katika siku hii ya Vijana. Kwa kuongeza alisema: “Huu ni mwaliko kwetu sote, vijana kike na kiume waliolewa, au hawajaolewa au kuoa au bado na wengine ambao wameanza maisha ya familia ili kama kijana Maria tuweze kuiga mfano bora wa kukimbia kwa haraka kutoa huduma kwa wengine wenye kuhitaji zaidi. Hiyo ndiyo hatua ya kushuhudia upendo wa Kristo ambao tunaombwa." Alisema Joseline.
Ikumbukwe Siku ya Vijana Ulimwenguni 2023 inatarajiwa kufunguliwa rasmi kwa Misa Takatifu mnamo tarehe 1- 6 Agosti 2023. Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuondoka tarehe 2 Agosti kulekea Lisbon. Maandalizi ya kila Siku ya Vijana Duniani, yana utambuzi wake na mvuto unaozinduliwa kwa ajili ya mkutano wa vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Ili hilo litimie Papa aliwakabidhi kwa walinzi, watakatifu na wenyeheri waliotangazwa kuwa watakatifu au walioko kwenye mchakato wa kuwatangazwa watakatifu. Katika Siku ya WYD Lisbon 2023, Kamati ya Maandalizi mahalia iliwatambulisha watakatifu 13 wasimamizi hao wakiwa ni wanawake, wanaume na vijana ambao “walionesha kwamba maisha ya Kristo yanajaza na kuokoa vijana wa kila kizazi”.
Watakatifu na wenyeheri wasimamizi wa Siku ya Vijana duniani 2023
Hawa ni Mtakatifu Yohane Paulo II, mwanzilishi wa Siku hii, Mtakatifu Vincent, Mtakatifu Anthoni wa Padua, Mtakatifu Bartholomayo wa mashahidi, Mtakatifu Yohane wa Brito, Mjesuit, Mwenyeheri Joanna wa Ureno, Jonh Fernandes, Mjesuit, Mwenyeheri Ignatius wa Azevedo; Mwenyeheri Maria Clara Mtoto Yesu, Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati, Mwenyeheri Chiara Badano, na Mwenyeheri Carlo Acutis.
Je Siku ya vijana miaka iliyopita ilifanyika wapi?
Ndugu msomaji Lisbon kwa hiyo ni mji uliochaguliwa na Papa Francisko kuwa toleo lijalo la kimataifa la Siku ya Vijana Duniani, 2023. Hata hivyo kumekuwa na Matoleo ya kimataifa ya WYD mengine ambayo kwa hakika yanahusisha matendo ya kidini na kiutamaduni na kuleta pamoja mamia ya maelfu ya vijana kutoka ulimwenguni kote hadi kwa takriban ya juma moja. WYD ilizaliwa kwa mpango wa Papa Mtakatifu Yohane Paulo II, baada ya mafanikio ya mkutano ulihamasishwa mnamo mwaka 1985 jijini Roma, katika fursa ya 'Mwaka wa Kimataifa wa Vijana': Toleo la kwanza WYD kwa hiyo lilifanyika mnamo 1986 jijini Roma na tangu wakati huo siku ya vijana imepitia katika miji mbali mbali kama ifuatayo: Buenos Aires (1987), Santiago de Compostela (1989), Czestochowa (1991), Denver (1993), Manila (1995), Paris (1997), Roma (2000), Toronto (2002), Sydney (2001), Cologne (2005), Sydney (2008), Madrid, 2011, Denver (1993), Manila (1995) Lio De Janeiro (2013), Krokow(2016), Panama (2019) na Sasa Lisbon (2023) na Je ijayo itakuwa nchi gani? Ni swali na shauku ya kujua hilo.