WYD,Lisbon2023:Wanahija wa China kuelekea Lisbon
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Hii ya ajabu isiyopangwa ilikuwa ni neema ya Mungu. Tungetarajia nini zaidi ya hii, kuanza safari yetu ya WYD huko Lisbon? Ni zawadi kutoka kwa Mungu, heshima kubwa na mshangao wa ajabu. Haya ni maneno yaliyotumiwa na wavulana na wasichana wa Kichina ambao mara baada ya kutua Roma hivi karibuni Julai 21 baada ya safari ya masaa 12 na bila kupumzika wakati, wakiwa katika Jiji la Milele Roma ambalo lililokuwa na joto kali la majira ya joto, waliweza kuwepo katika ziara isiyo pangwa kutembelea Jumba Propaganda Fide, ambalo ni jengo la kihistoria linalotazamana na Uwanja wa Hispania ambayo ni Makao Makuu ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji.
Mahujaji wa China walikaribishwa kwa moyo mkunjufu na Monsinyo Samuele Sangalli, Katibu Msaidizi wa Baraza hilo kwa niaba ya Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle Mwenyekiti Shirikishi wa Baraza hilo. Kundi hilo la wasichana na wavulana 50, wakisindikizwa na wazee na baadhi ya wanafamilia wazee, walisafiri kuelekea Ureno, ambako watashiriki katika Siku ya Vijana Duniani Lisbon 2023. Roma kilikuwa ni kituo cha kwanza kwenye hija yao huko Ulaya. Wote wakisikiliza kwa hisia salamu iliyoletwa kwao na Monsinyo Sangalli, ambaye kwa maneno mepesi alionesha furaha kwa ajili ya mkutano huu ambao haukupangwa kati ya kaka na dada katika imani, ambao ulifanyika mahali palipojaa ishara na mwangwi wa maombi ya upendo ya Kanisa la Roma kwa Wakatoliki wa China.
Mahujaji wote kutoka mikoa mbalimbali ya China bara pia walipokea Rozari ya kimisionari kama zawadi, waliyopewa katika makao makuu ya kihistoria ya Shirika la Propaganda Fide lililotuma wamisionari kama Matteo Ricci na Padre Teodorico Pedrini nchini China. Mara moja kila mtu alivaa Rozari ya kimisionari shingoni mwao. Kisha, katika Kikanisha cha Wafalme Watatu, kazi ya msanii mkubwa Francesco Borromini, waliimba wimbo wa Salamu Maria kwa lugha yao ya asili (tazama video), wakiongozwa na machozi kwa uzoefu wa kuweza kumwomba Maria mahali kutoka kwa wamisionari wengi sana, katika nyakati zilizopita, waliiacha ili kuleta zawadi ya Injili nchini China, wakitoa maisha yao yote kwa ndugu zao wa China.
Katika ziara yao kwenye jumba la Propaganda, mahujaji wa China pia walifurahia kuona sanamu hiyo na kusikiliza historia ya Kardinali Celso Costantini Mwakilishi wa kwanza wa kitume nchini China, ambaye baada ya miaka iliyotumika katika ardhi ya China pia alikua Katibu wa Shirika la Wamisionari, akifanya kazi sana katika Jumba hilo la Uinjilishaji. Hisia na furaha ya siku yao ya kwanza ya hija iliwafanya kundi zima kusahau ugumu wa safari hiyo ndefu. Mahujaji wa kundi la Wachina wanatoka majimbo ya Shaanxi, Shanxi na Hebei. Mdogo wa kikundi alikuwa na umri wa miaka 15. Baadhi yao walipokea ubatizo hivi karibuni, wengine bado hawajabatizwa na wanaona hija ikiwa ni hatua ya kwanza katika safari ya maisha mapya ambayo yanashamiri baada ya kukutana na Yesu. Baada ya Roma, kundi la mahujaji pia lilikwenda Assisi, Avignon, Lourdes, Zaragoza, Madrid na Salamanca, kabla ya kufika Lisbon. Mahujaji walijiandaa kwa safari hiyo kwa kuhudhuria mafunzo ya katekisimu na kushiriki katika mafungo ya kiroho. Kabla ya kuondoka kwenye Jumba la Propaganda, mahujaji walitaka kukusanyika tena katika Kanisa la Wafalme Watatu, na kwa mara nyingine tena kumshukuru Yesu na Maria kwa kuishi uzoefu usiosahaulika wa kutembelea maeneo ambayo wamisionari wengi waliondoka kutoka kizazi hadi kizazi, wakiongozwa na hamu ya kutangaza furaha ya Injili ya Kristo nchini China na duniani kote.