Kard.Dziwisz:umwagaji damu ukome nchini Ukrane
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Hatuwezi kukubali kile kinachotokea Ulaya, mbele ya macho ya ulimwengu wote, kwa sababu mkasa huo unawanyima ndugu zetu wa Ukraine ardhi yao, haki yao ya kuishi, lugha na utamaduni wao, kupanda kifo na uharibifu. Huu ndio wito wenye nguvu uliozinduliwa na Kardinali Stanisław Dziwisz, Askofu mkuu mstaafu wa Krakow, aliyeteuliwa na Papa Francisko kuwa mjumbe wake maalum katika maadhimisho ya miaka mia tatu ya kutawazwa kwa Pocha ya Mama yetu Malkia wa Podlasie - Mama wa Umoja iliyofanytika tarehe 15 Agosti 2023 katika madhabahu ya Kodeń, katika jimbo la Siedlce.
Ndugu hawawezi kungambana wao kwa wao
Kardinali Dziwisz katika mahubiri yake alisema: “Ndugu wa Waslavic hawawezi kupigana dhidi ya kila mmoja. Hawawezi kujiua, hawawezi kujiangamiza wenyewe, hawawezi kupanda uharibifu, hawawezi kuzidisha mateso makubwa tunayoshuhudia. Tunahitaji kuusimamisha mkono wa Kaini. Tunahitaji kukomesha chuki, vurugu, vita vya kindugu. Hakuna umwagaji damu tena! Ombi hilo lilitekelezwa moja kwa moja kwa wale ambao wamefafanuliwa na Kardinali kama ndugu wa Slavic, ili ulimwengu upewe mfano wa kuishi pamoja kidugu kati ya watu wetu na sio chuki ya kipofu. Maombi hayo yalilekezwa kwa Mama Yetu wa Kodeń, ili kutikia njia ya mwisho wa vita, upatanisho na amani.
Mahali pa miujiza
Katika barua hiyo ambayo amemtaja Kardinali Dziwisz kuwa mjumbe wake, Papa Francisko alisisitiza kwamba Madhabahu ya Bikira Maria wa Kodeń ni mahali pa miujiza, ambapo watu wengi hufika kusali na kukabidhi maisha yao kwa Maria. Ni hapo kwamba, alikumbuka katibu wa zamani wa Mtakatifu Yohane Paulo II na mstaafu wa Jimbo Kuu la Krakow wakati huo alifanya hija kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu wa Roma. Papa wa baadaye, alikuwa ameona sifa maalum za Mama wa Kristo. Maria Kardinali Dziwisz alisema anaunganisha Watu wa Mungu. Lakini tunajikuta katika nchi ambayo muungano huu wa Watu wa Mungu umekuwa na umuhimu maalum wa kihistoria. Ilikuwa hapo hasa ambapo mkutano wa Makanisa tofauti ya Magharibi na Mashariki ulifanyika. Mtakatifu Papa Yohane Paulo II wa baadaye, wakati wa ziara yake huko Kodeń, alisema kwamba katika eneo la Podlachia, Poland ya Mashariki, Mama alihitajika, uwepo wa Mama, wa Mama anayeunganisha, wa Mama anayejua yote. watoto, bila kutofautisha kama wanazungumza Kipolandi, Kirusi au Kilithuania”.
Historia ya madhabahu
Sherehe hiyo iliambatana na kuvishwa mataji mapya kwenye sanamu za Maria na Yesu, iliyobarikiwa na Papa Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 3 Agosti 2022. Mahujaji wengi walifika katika hafla hiyo kwa mwaliko wa Askofu Kazimierz Gurda, jimbo la Siedlce na wasimamizi wa madhabahu ya Wamisionari wa Oblate wa Maria Safi wa Moyo. Historia ya madhabahu ya Kodeń ilianza mwanzoni mwa karne ya 17. Mikołaj Sapieha alipona baada ya kusali katika Kikanisa cha Kiapa, kwa mwaliko wa Papa Urbano VIII, mbele ya sanamu ya Mamama. Sapieha alidanganya kwa picha hiyo na kuipeleka. Kwa Kodeń mnamo 1631, ambapo bado ipo sasa hao . Picha ya Mama wa Mungu ilikuwa moja ya sanamu za kwanza za Kipolandi kuvikwa taji za upapa mnamo 1723.