Tafuta

2023.08.07:Kundi la Vijana wa Jimbo la Mbinga,Tanzania katika WYD wakiwa na vijana wa Jimbo la Würzburg, Ujerumani ambalo ni ndugu na Mbinga. 2023.08.07:Kundi la Vijana wa Jimbo la Mbinga,Tanzania katika WYD wakiwa na vijana wa Jimbo la Würzburg, Ujerumani ambalo ni ndugu na Mbinga. 

Kutoka Tanzania hadi WYD na mshikamano wa kidugu wa Würzburg

Kati ya vijana kutoka Tanzania walioshiriki Siku ya vijana duniani huko Lisbon kuanzia tarehe Mosi hadi 6 Agosti wengine waliungana na kundi la Jimbo la Würzburg,Ujerumani wakiwa wanatokea Jimbo la Mbinga Tanzania.Vijana na Padre Witney Ngahi wametoa maoni yao kuhusu tukio hili muhimu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baada ya kumalizika kwa Siku ya vijana Duniani, inabaki bado simulizi iliyo hai ambayo inapaswa idumu ili kuzidisha shauku ya vijana waweze kumfuata Kristo kwa mfano bora  wa Mama Yake Maria ambaye mara baada ya kupata tangazo hakukaa kimya bali alikimbia upesi kwenda kumsaidia binanamu yake Elizabeth, kama ilivyokuwa Kauli mbiu ya maadhimisho Siku ya Vijana Ulimwenguni kuanzia tarehe 1 -6 Agosti  2023  huko Lisbon:  “Maria aliondoka akaenda kwa haraka.” Lk. 1:39. Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo aliwasihi vijana kuwa nuru wakitangaza na kushuhudia nuru ya Injili kwa matumaini katika kila kona wanapopita na kutumwa. Na nguzo moja kuu ni kumkaribisha Yesu kuwa kiini cha maisha yao na upendo mkuu. Je nani ambaye atasahau ujumbe wa Papa kwa roho hizi  za vijana milioni moja na nusu ambao walikuwa wakimsikiliza kwa makini sana katika siku mahubiri ya Mwisho ya Vijana duniani?

Utakalo na lifanyike Baba wa Mbingu
Utakalo na lifanyike Baba wa Mbingu

Papa ktika mahubiri yake Dominika tarehe 6 Agosti 203 aliwambia vijana kuwa: “Msiogope vijana wapendwa: kwa sababu ninyi ni kama mvua kutoka katika nchi iliyokaushwa na maovu elfu moja, ninyi ni mwanga wa nuru ya sasa na ya wakati ujao katika pembe nyingi za giza za wakati wetu". Aidha akiendelea alisema "Marafiki, vijana wapendwa, leo sisi pia tunahitaji nuru kidogo, miali michache ya nuru, ambayo ni matumaini ya kukabiliana na maficho mengi sana ambayo yanatushambulia maishani, kushindwa sana kila siku, ili kuyakabili inahitahi nuru ya Ufufuko wa Yesu.”

Kung'ara kwa Bwana: Vijana wafuate nuru ya Kristo
Kung'ara kwa Bwana: Vijana wafuate nuru ya Kristo

Baba Mtakatifu alikazia kusema kuwa: "Siri nzima iko katika hili la kukiliza Yesu anachokuambia. Sijui anachoniambia. Ichukue Injili na usome kile ambacho Yesu anasema na kile ambacho moyo wako unakuambia.  Kumsikiliza Yesu ili kwamba sisi, hata ikiwa kwa nia njema, tuanza njia zinazoonekana kuwa za upendo, lakini hatimaye ni  za ubinafsi unaojificha kama upendo. Jihadharini na ubinafsi unaojifanya kuwa upendo.” Baba Mtakatifu kwa hiyo alsema  kwamba: “Ninyi mnaotaka kuubadili ulimwengu na mnaotaka kupambania haki na amani; kwenu, vijana, ambao naweka juhudi na mawazo katika maisha lakini inaonekana kuwa  kuwa haitoshi; Ninyi vijana, ambao Kanisa na ulimwengu wanahitaji kama nchi ya mvua; ninyi vijana, mliopo sasa na wajao; ndiyo, kwa usahihi ninyi, vijana, leo Yesu anawaambia: “Msiogope!, Msiogope”!

Ushuhuda wa vijana wa Jimbo la Mbinga Tanzania na Würzburg Ujerumani wakati wa WYD
Ushuhuda wa vijana wa Jimbo la Mbinga Tanzania na Würzburg Ujerumani wakati wa WYD

Kati ya vijana wengi waliodhuria siku ya vijana, lakini pia kulikuwa na wengine waliofuatilia kwenye mtandao na wengine katika majimbo yao. Hatua hivyo hata Nchi nyingine kwa mfano kwa wa msaada wa Jimbo Katoliki la Würzburg nchini Ujerumani, kikundi cha vijana kutoka jimbo la Mbinga nchini Tanzania kiliweza kushiriki katika  siku ya vijana Duniani (WYD) mjini Lisbon kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Kwenda katika Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon, Ureno sio shida sana kwa vijana wa Ulaya, au Marekani na sehemu nyingine zenye uwezo kwa mfano Nchi zilizowakilishwa zaidi ni Hispania iliyokuwa na mahujaji 77,224, Italia ilifuatia katika nafasi ya pili kwa kuwa na vijana 65,000, Ureno 43,742 na Ufaransa 42,482. Kwa upande wa Maaskofu 688 kutoka ulimwenguni  kote, makadinali 30, Maaskofu 109 waliofika kutoka Italia,  70 kutoka Hispania, 65 kutoka Ufaransa, 61 kutoka Marekani na 36 kutoka Ureno na kwingineko walio wachache.

Ni Yesu Kristo wa kumfuata na kueneza Neno lake duniani kote
Ni Yesu Kristo wa kumfuata na kueneza Neno lake duniani kote

Siku ya vijana Duniani (WYD) ya Lisbon pia inarekodiwa na  ushiriki mkubwa wa mahujaji kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kireno kwa mfano kutoka Brazil (5,826), Angola (752), Cape Verde (940), São Tomé na Príncipe (513), Msumbiji (312), Guinea-Bissau (122) na Timor ya Mashariki (62). Kulikuwa na mahujaji wenye ulemavu 1,753 (kati yao 153 ni viziwi na 241 ni vipofu). Kama haiyo haitoshi siku ya vijana WYD Lisbon 2023 ilikuwa imeanadaa makazi ya umma 1,626, yenye uwezo wa kubeba mahujaji 294, 151, na familia 8,831 zilifungua milango ya nyumba zao kuwakaribisha mahujaji 28,618. Kwa upande wa chakula, taasisi 1,800 za upishi zilijiunga na WYD, na kuruhusu kuandaa karibu milo milioni 2.7. Kuhusu Tamasha la Vijana yalikuwa ni zaidi ya matukio 600 yenye washiriki zaidi ya 2,500 katika maeneo 90 tofauti.  Jambo jingine la kufurahisha lilikuwa ni liele la kujiwekea lengo la kijani ambapo katika utunzaji wa mazingira walipanda miti 17,980 katia fursa hii ya siku ya vijana duniani (WYD) Lisbon 2023.

Vijana wa Jimbo la Mbinga Tanzania na Jimbo Ndugu la Würzburg Ujerumani katika WYD
Vijana wa Jimbo la Mbinga Tanzania na Jimbo Ndugu la Würzburg Ujerumani katika WYD

Tukirudi tena katika mahujaji kutoka Tanzania,  kama tulivyotangulia kusema hawakuwa wengi sana kama  vijana wa Nchi nyingine, kwa sababu si kuhitaji pesa tu,  lakini pia hata visa. Hii ni kwa sababu haikuwa rahisi sana kupata visa. Licha ya hayo Jimbo Katoliki la Würzburg nchini Ujerumani lilifanikiwa kuwasaidia baadhi ya washiriki vijana kutoka Tanzania katika Jimbo la Mbinga ili kushiriki katika Siku ya Vijana Duniani pamoja na Papa Francisko. Padre Witney Ngahi, mwenye Umri wa miaka 36 aliwasindikiza kikundi hiki cha vijana ambao walioudhuria na kwa hiyo mwandishi wetu wa  habari wa Vatican mmojawapo wa waliokuwa wakituwakilisha katika tukio hilo Stefanie Stahlhofen, alihojiana nao na wakatoa ushuhuda wao. Kimsingi walieleza walivyokaribishwa huko Ujerumani hadi kufika Lisbon katika Siku hizi. Ukarimu wa vijana, shauku na yale mapya waliyojifunza na ambayo waliahidi wakifika nchini  Tanzania wataweza kuwamegea wengine. Na kwa upande wa  Padre Ngai, anasisitiza juu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu anavyo wasihii vijana wasiogope, wampe matumaini Yesu Kristo awe kiongozi wa maisha yao.

Ushuhuda wa Vijana kutoka Jimbo la Mbinga Tanzani walioudhuria WYD Lisbon
08 August 2023, 13:26