Tafuta

2023.08.24: Provinsi ya  Amerika ya Kati ya Wajesuit inalaani vikali sheria ambayo mamlaka ya Nicaragua ilibatilisha hadhi ya kisheria ya Jumuiya ya Yesu. 2023.08.24: Provinsi ya Amerika ya Kati ya Wajesuit inalaani vikali sheria ambayo mamlaka ya Nicaragua ilibatilisha hadhi ya kisheria ya Jumuiya ya Yesu. 

Nicaragua.Kubatilishwa hadhi ya kisheria ya Kijesuit:ugaidi na ukandamizaji nchini

Nchini Nikaragua uchokozi usio na msingi dhidi ya Wajesuit unaendelea katika muktadha wa jumla ya ukandamizaji.Provinsi ya Amerika ya Kati ya Jumuiya ya Yesu imechukizwa na kifungu ambacho serikali inayoongozwa na Daniel Ortega ilibatilisha hadhi yake ya kisheria na inazungumza juu ya ukandamizaji wa kimfumo ulioainishwa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Provinsi ya Amerika ya Kati ya Wajesuit inaonesha kulaani vikali sheria ambayo mamlaka ya Nicaragua ilibatilisha hadhi ya kisheria ya Jumuiya ya Yesu. Katika taarifa yake, iliyotolewa tarehe 23 Agosti 2023, Wajesuit wanachukizwa na uchokozi mpya dhidi ya watu wa kidini na Kanuni iliyoanzishwa na Mtakatifu Ignatius wa Loyola, kitendo ambacho ni sehemu ya sera ya ugaidi dhidi ya wakazi wa Nicaragua na ukandamizaji wa utaratibu zaidi ambao serikali ya Ortega inatekeleza katika ngazi ya kitaifa na ambayo kikundi cha wataalam kilianzisha nchini Nicaragua tayari imeainishwa na Umoja wa Mataifa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kuelekea utawala wa kiimla
Kulingana na Provinsi ya Amerika ya Kati la Jumuiya ya Yesu, hatua hiyo inalengakuanzishwa kikamilifu kwa serikali ya kiimla ambayo rais na makamu wa rais wa Nicaragua wanawajibika, na hatia ya kuzuia uhuru na kutoegemea upande wowote wa mahakama. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inawaalika viongozi wa nchi hiyo kusitisha ukandamizaji unaoendelea na kupendelea suluhisho la busara ambalo ukweli, haki, mazungumzo, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria vinatawala. Zaidi ya hayo, heshima kamili kwa uhuru na utambulisho wa Kijesuit na watu wanaoshirikiana nao inaombwa. Jumuiya ya Yesu ya Nicaragua inasema iko katika ushirika na maelfu ya waathirika wa Nikaragua wanaosubiri haki na fidia kwa uharibifu uliosababishwa na serikali ya sasa na inaelezea shukrani kwa matamshi mengi ya utambuzi, msaada na mshikamano uliopokelewa kufuatia kuongezeka kwa hasira.

Hakuna uwezekano wa kukata rufaa
Masharti ya serikali 105-2023 yanathibitisha kwamba mali isiyohamishika na mali zinazohamishika za Jumuiya ya Yesu nchini zinapaswa kuhamishiwa serikalini. Kama ilivyo kwa kesi zingine za kufutiwa usajili zilizoanzishwa na serikali tangu 2018, uamuzi huo ulichukuliwa bila taratibu za kiutawala zilizowekwa na sheria kukamilika. Kijesuit hawapewi uwezekano wa kukimbilia kwa hakimu asiye na upendeleo.

Mateso dhidi ya Kanisa Katoliki yanazidi kuongezeka
Kabla ya hatua hiyo ya hivi karibuni ya ukandamizaji, takriban juma moja iliyopita serikali ya Ortega, kwa kisingizio cha mapambano dhidi ya ugaidi, ilikuwa tayari imekiteka Chuo Kikuu cha Amerika ya Kati cha Nicaragua (UCA), kilichoanzishwa na Wajesuit, na makazi ya Jumuiya ya Wajesuit huko Managua bila kutoa muda wowote kwa wale walioishi huko kukusanya na kuchukua mali zao za kibinafsi. Siku tano tu zilizopita, tarehe 19 Agosti 2023 ilikuwa ni  kumbukumbu ya kwanza ya kukamatwa kwa Askofu Rolando Álvarez, wa Jimbo la Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Estelí, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 26 jela bila kesi, kwa mashtaka ya kula njama dhidi ya uadilifu wa kitaifa na kueneza habari za uongo. Tangu wakati huo, mateso dhidi ya Kanisa Katoliki yameongezeka nchini Nicaragua.

Wajesuit kwamefukuzwa nchini Nicaragua


 

24 August 2023, 16:43