Kardinali Onaiyekan ametoa ombi kali la kutafuta suluhisho za amani nchini Niger, na dhidi ya suluhisho yanayoleta kifo na vita. Kardinali Onaiyekan ametoa ombi kali la kutafuta suluhisho za amani nchini Niger, na dhidi ya suluhisho yanayoleta kifo na vita.  (ANSA)

Niger,Kard.Onaiyekan:Hapana vita,bali demokrasia &utawala bora unahitajika

Katika mahojiano na Vatican News,Kardinali Onaiyekan,Askofu Mkuu Mstaafu wa Abuja,Nigeria,anatoa wito wa suluhisho la amani na anaonya dhidi ya chaguzi nyingine zitakazoleta vita,mauaji na vurugu,akizungumzia Niger.Kwa nchi yake anasema:”Wale ambao wanapaswa kuhakikisha watu wako salama wanashughulika na kujipatia faida binafsi.Hilo ndilo tatizo.

Na Deborah Castellano Lubov, - Vatican.

Kardinali John Onaiyekan ametoa ombi kali la kutafuta suluhisho za amani nchini Niger, na dhidi ya masuluhisho yanayoleta kifo na vita. Katika mahojiano na Vatican News, Askofu Mkuu Mstaafu wa Abuja nchini Nigeria ameeleza hayo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya sasa ya Nigeria hasa kwa Wakristo na kutafakari kuhusu Afrika Magharibi kwa ujumla. Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa Umoja wa Afrika (AU) umeisimamisha Niger katika shughuli zake zote kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Julai uliopita na kuwaambia wanachama wake kuepuka hatua zozote zinazoweza kuhalalisha utawala huo. Kwa mujiu wa Shirika hilo, Mapinduzi hayo, yamezusha wasiwasi miongoni mwa washirika wa Magharibi na mataifa ya kidemokrasia ya Afrika ambayo yanahofia yanaweza kuruhusu makundi ya kiasi ya kihalifu yanayofanya kazi katika eneo la Sahel kupanua wigo wao na kuipatia Urussi nafasi ya kuongeza ushawishi wake. Wakati Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, (ECOWAS), imekuwa ikijaribu kufanya mazungumzo na mamlaka ya kijeshi, inasema kwamba, ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa, iko tayari ya kutuma wanajeshi nchini Niger kurejesha utulivu wa kikatiba.

Kwa njia hiyo Kardinali John Onaiyekan anatoa maoni yake kwa Vatican News uchunguzi wa hali ya uhamiaji katika nchi yake, kwa namna ya pekee, anawatazama kwa huruma  wale wote waliokimbia makazi yao ndani ya nchi. Anajikita na kulezea kile kinachopaswa kufanywa kwa ajili yao, na kwa wale wanaohisi maisha bora ya baadaye yapo nje ya mipaka yao, lakini wanajikuta wamekatishwa tamaa na ukweli wa mara kwa mara mbaya. Pia anaomboleza kwa wale wote waliokufa njiani, baada ya kufuata simulizi ya uwongo. Mara kwa mara, Wanigeria, wakiwemo makasisi, hutekwa nyara na kuuawa. Kwa hiyo “Ongezeko la utekaji nyara, mauaji na unyanyasaji wa jumla dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na makasisi wa Kikatoliki katika maeneo mengi ya Nigeria, ni janga ambalo bado halijashughulikiwa ipasavyo na mamlaka mahalia”,Shirika la Habari za Kikatoliki lilitipoti (CAN.) Wakati Kardinali anajaribu kutoa tahadhari kwa sababu ya mateso ya Wakristo, anasema, wote, wakiwemo Waislamu pia, wana masuala yao yanayosababishwa hasa na utawala mbaya, na kuonya dhidi ya wanasiasa wa Kikristo, ambao, alisema: “ni Wakristo kwa jina tu”

Yafuatayo ni mahojiano kamili ya Kardinali na Mwandishi wa Vatican News:

Kardinali Onaiyekan, unalo ombi la amani, kutokana na matukio yanayotokea Afrika Magharibi, na kwa namna ya pekee, kutokana na hali ya Niger?

Kweli, ni katika rekodi sasa kwamba watu wengi ndani ya eneo letu la Afrika Magharibi wamesihi kwamba Jumuiya ya ECOWAS inapaswa kuacha wazo la kutumia nguvu kwa serikali ya Niger, na badala yake kufuata njia nyingine, isiyo ya vurugu ili kutatua mzozo nchini na njia bora iwezekanavyo. Vikundi vilivyotoa kauli za aina hii hadharani ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Nigeria wakizungumza kupitia maaskofu wetu, Rais wa Baraza letu la Maaskofu, Askofu Mkuu Lucius Ugorji wa Warri, na pia Baraza la Maaskofu wa Afrika Magharibi. Baraza la Maaskofu wa Afrika Magharibi pia wametoa  kauli yenye nguvu. Kwa mtazamo wa Kanisa Katoliki, msimamo wetu uko wazi hakuna vita, hakuna mauaji. Sio suluhisho kwa tatizo la mapinduzi ya kijeshi, na hakika huo ni msimamo wangu madhubuti pia.  “Kwa mtazamo wa Kanisa Katoliki, msimamo wetu uko wazi hakuna vita, hakuna mauaji. Sio suluhu kwa tatizo la mapinduzi ya kijeshi, na hakika huo ni msimamo wangu madhubuti pia.”

Katika habari hivi karibuni kulikuwa na ukweli kwamba Wanigeria wengi, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, walifukuzwa kutoka Libya. Je, unaweza kutoa mwanga zaidi, kwa ujumla, kuhusu hali ya wahamiaji wa Nigeria?

Kuna mtiririko wa mara kwa mara wa watu wanaoondoka katika nchi yetu, Nigeria, kupitia jangwa, wakielekea Ulaya. Wanawake na watoto, lakini hasa vijana na wanawake vijana. Tunasikia kila siku kuhusu ajali za meli katika Mediterania na hali ngumu za wahamiaji. Tunajaribu tuwezavyo kuwakatisha tamaa watu wetu wasifanye safari hizi hatari, lakini kwa bahati mbaya, hatufaulu. Wao daima hasa  ni vijana, vijana ambao wanahisi kuwa hali yao katika nchi yetu haikubaliki, na haiwezi kuvumiliwa. Kwa namna fulani wanaamini, kwamba watakuwa na Maisha mazuri Ulaya, ambapo, kulingana na wao, kila kitu kitafanya kazi vizuri. Juhudi zetu za kuwaambia kwamba hii si kweli, hazizai matunda mengi. Hii imesababisha vifo vya maelfu, sio mamia, maelfu ya watu. Hawa ni wanadamu.

Kuna haja ya juhudi kubwa zaidi kwa upande wa kila mtu anayehusika, ikiwa ni pamoja na Ulaya na serikali ya Ulaya, kukomesha janga hili la kawaida la kupoteza maisha ya binadamu. Nina maoni hayo na niliwahi kueleza mara kadhaa huko nyuma kwamba watu hupitia safari za hatari jangwani na kwenye boti zenye misukosuko kwa sababu hawawezi kupata visa vya kisheria vya kawaida vya kwenda Ulaya au Marekani  au kwingineko. Ikiwa kungekuwa na njia ya kuwapatia viza, wangekuwa wanasafiri kwa njia ya kawaida sana bila aina ya hali ya kutisha tuliyo nayo mikononi mwetu. Kikweli, watu wengi ni wakimbizi ndani ya nchi zetu, kuliko wale wanaokwenda Ulaya. Watu wengi wamehamishwa kutoka katika makazi yao na wanaishi kama wakimbizi wa ndani ndani ya mipaka yetu. Watu hawa wanahitaji umakini, lakini labda hawapati usikivu mwingi kwa vile hakuna kipengele cha kimataifa cha mkasa wao. Jambo hili lina msingi wake suala lile lile, watu waliohamishwa kutoka katika nyumba zao, wanaoishi katika mazingira hatarishi na hatari.

Je ni nini kifanyike kuwasaidia watu waliohamishwa ndani ya mipaka ya nchi?

Samahani kusema kwamba inatokea tu kuwa suala la serikali mbaya. Wakati serikali haifanyi kazi yake vizuri, wakati uhamishaji mwingi unasababishwa na mapigano ya ndani na nje, vita kidogo, au wakati mwingine na shughuli za magaidi wanaoua watu na kufanya makazi yao kutokuwa salama, hii hutokea kwa sababu serikali wanaopaswa kuhakikisha usalama wa maisha na mali, hawafanyi kazi zao vizuri. Sheria hazizingatiwi kamwe na kuna kutokujali sana. Wale ambao wanapaswa kuhakikisha kuwa watu wako salama wanashughulika na kujipatia faida. Hilo ndilo tatizo msingi. Nchini Nigeria, wengi wa watu wetu waliokimbia makazi yao ni wakulima na wanavijiji ambao vijiji na mashamba yao yamechukuliwa kuwa si salama na magaidi wenye silaha, wachungaji wa mifugo na kila aina ya majambazi. Kwa nini watu hao wanaweza kuendelea kufanya hivi? Kwa nini polisi na vikosi vya jeshi haviwezi kurejesha kiwango cha chini cha ulinzi na usalama? Jibu ni gumu kulipata, isipokuwa kusema kwamba hatuna serikali inayoweza kufanya ambayo inaweza kutekeleza majukumu ambayo yanapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza. Inasikitisha sana kuona hili.

Kardinali, kabla hujajadili wale walioondoka nyumbani kwao kuja Ulaya, na baadaye wanakabiliwa na tamaa kubwa, wengine kupoteza maisha. Kuna hoja gani ya wao kubaki Nigeria? Ni nini kinachopaswa kuwaweka? Ikiwa ungelazimika kumshawishi kijana ambaye anakaribia kuondoka, abaki, ungesema nini? Nini kifanyike, au nini kinafanywa kuwasaidia katika nchi yao wenyewe?

Naam, nimekuwa na mwingiliano mbalimbali na vijana hapa Nigeria juu ya jambo hili. Ninalazimika kukubaliana nao kwamba mambo katika nchi yangu hayaendi sawa. Hakuna kazi kwa vijana kuweza kujikimu kimaisha. Hawawezi kujitunza, kamwe hawajali kutunza wazazi wao waliozeeka au kuanzisha familia. Vijana wanatazama siku za usoni na hawaoni madoa yoyote angavu kutoka nchi ya Nigeria, na kusema, hatuwezi kuendelea katika nchi hii tena. Tutakwenda popote pengine, na kulingana na wao, itakuwa bora zaidi. Popote tunapokwenda, tunakutana na  kijana ana shahada, shahada ya uzamili ya uhandisi au historia. Anasema, sijali kwenda Ulaya kuwa barman, kuchuma viazi alimradi niko nje ya nchi hii. Wanakwenda ng’ambo si hata kutumia ujuzi na vipaji vyao, bali kufanya kazi yoyote duni ambayo, kwa mujibu wao, wanaweza kupata pesa kwa fedha za kigeni na wanaamini tu kwamba huo utakuwa mwanzo wa maisha bora kwa ajili yao.

Hawakubaliani ninapowaambia kuwa maisha yanaweza kuwa mabaya nje ya nchi kwa mhamiaji haramu kama ilivyo kwao hapa nyumbani. Hawakuamini. Wanasema ikiwa wanaweza kuifanya, wataifanya. Wanakerwa na mimi kuwa siwasaidii kuwapa pesa za kuweza kuwalipa mawakala watakaowabeba kwa hela. Wanasema siwajali. Tunaweza kutumaini tu na kusali kwamba mambo yabadilike ili vijana walio tayari kufanya kazi waweze kubaki katika nchi hii, wapate kazi nzuri, wapate pesa nzuri, na wajithibitishe. Kwa bahati mbaya, sasa hiyo haifanyiki. Ni watoto wa matajiri tu, ambao pia kwa kiasi kikubwa ni watoto wa wale walio madarakani, wanaweza kutarajia kazi nzuri sana serikalini au kwingineko. Kwa maskini, watu wameachwa peke yao na siku zijazo ni mbaya sana.

Mwadhama, umekuwa mtetezi wa sauti ili kuongezeka kwa usalama, ulinzi zaidi kwa Wakristo. Je, hali ikoje kwa sasa? Je, imeboreshwa kwa Wakristo, au la? Je, kuna jambo bado linahitaji kufanywa?

Mara nyingi nasikia mengi yakisemwa kuhusu jinsi Wakristo wanavyoteswa nchini Nigeria, jinsi Wakristo wanavyoteseka huko. Kwa kiasi fulani ni kweli, kuna sehemu nyingi za Nigeria ambapo kuwa Mkristo ni dhima, na ikiwa wewe ni Muislamu, una nafasi nzuri ya kuwa na maisha bora, lakini ukweli ni kwamba taifa zima liko ndani ya  sura mbaya na Wakristo na Waislamu wanateseka katika hali niliyoeleza hapo awali. Sio kana kwamba Waislamu nchini Nigeria wana maisha ya ajabu. Hapana, si kweli kwamba wanafanya vizuri sana. Watoto wao wanapata kazi nzuri huku Wakristo wakiachwa pembezoni. Kuna Wakristo, pia katika korido za madaraka na ambao ni miongoni mwa watawala wa taifa letu. Kwa bahati mbaya, wengi wao ni Wakristo kwa jina tu. Kwa maoni yangu binafsi, sidhani kama hatuna haja ya kuzidisha mambo, suala la Wakristo kuteseka ni kwa sababu watu wengine pia wanateseka.

Afadhali tunapaswa kusisitiza ukweli kwamba kila mtu anapaswa kufanya awezavyo, ili kulifanya taifa letu kuwa mahali pazuri zaidi, na viongozi wa Kikristo, watawala, wanasiasa, wawe na mamlaka maradufu na wajibu maradufu wa kuboresha hali ya maisha katika taifa letu. Hali nyingi za migogoro kati ya Wakristo na Waislamu zinatokana na serikali mbovu, vivyo hivyo kwa sababu hizo hizo tuna mapigano kati ya makabila tofauti, mapigano ya kikabila. Kuna migogoro ya kikabila kwa sababu ya kushindwa kwa serikali. Ambapo Wakristo na Waislamu wanagongana, ni kwa sababu hiyo hiyo. Sikatai kwamba kuna Wakristo wengi ambao wana wakati mgumu nchini Nigeria, lakini mateso yanaenea zaidi ya Wakristo. Ikija kwa mateso ya moja kwa moja dhidi ya imani ya Kikristo, kunawezekana kuwa na matukio na kesi, lakini si nyingi sana, na kwa hakika si sera rasmi ya serikali kuwatesa Wakristo kama tunavyofanya katika baadhi ya nchi nyingine.

Je, kuna kitu kingine chochote ungependa kuongeza?

Chochote tunachosema kuhusu utawala mbovu barani Afrika, lazima pia tuwape changamoto mamlaka na serikali za Ulaya, Amerika, zile zinazoitwa jumuiya ya kimataifa zinazoshughulika na serikali zetu katika nchi hizi na wanaoona kinachoendelea. Wanaona mambo mabaya yanayotokea na wanaendelea kufanya biashara nao kana kwamba hakuna kitu kibaya. Wanaruhusu tabia mbaya kutokea katika nchi yetu, ambayo hawataruhusu au ambayo isingeruhusiwa kutokea katika nchi wanazotoka. Sasa nazungumzia taasisi za fedha, makampuni, makampuni ya biashara, yanayofanya biashara katika taifa letu. Unachukua mfano wa kawaida, sekta ya mafuta. Tunajua kwamba Nigeria ina kiasi kikubwa cha mafuta ya petroli.

Makampuni ya kimataifa yananyonya mafuta katika taifa letu kwa njia isiyo na uwajibikaji zaidi. Kugeuza mataifa hayo yote yenye utajiri wa mafuta kuwa machafuko kabisa ambapo kuna uharibifu mkubwa wa ardhi na misitu, vijijini kote, kwa sababu wanataka kuchukua mafuta kwa bei rahisi iwezekanavyo bila kuchukua tahadhari kama watafanya wakati wanachukua mafuta kutoka Bahari ya Kaskazini au kutoka Ghuba ya Mexico. Huko, hawatafanya mambo kama hayo. Lakini inapokuja kwenye Delta ya Niger, watafanya kila aina ya njia mbaya sana za kunyonya mafuta. Katika suala hili, wakati sisi, kama Wanigeria, tunawalaumu viongozi wetu wa Nigeria, tunatarajia kwamba watu walio nje ya nchi watakuja kuagiza taasisi zao wenyewe, na kutoa changamoto kwa wale wanaowezesha hali mbaya katika nchi zetu kuendelea. Wanaweza kuwa wananufaika nayo, lakini watapata bora zaidi ikiwa wataifanya nchi yetu kuwa nchi bora. Mafanikio ya Ulaya na Amerika yatakuwa bora zaidi, ikiwa watatuacha tujitawale vizuri.

26 August 2023, 14:51