Mwezi Machi 18  Papa Francisko alikutana na vijana wa "Mpango Policoro" wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI). Mwezi Machi 18 Papa Francisko alikutana na vijana wa "Mpango Policoro" wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI).  (ANSA)

Toleo la III la Mpango wa Policoro wa majira ya kiangazi na Fratelli tutti linaanza!

Toleo la tatu la kambi ya mafunzo kwa waseminari na wahuishaji juu ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa kwa mada:Kuunda ulimwengu wazi, inayohakisi sura ya tatu ya waraka wa Papa juu ya udugu,iko tayari kuanzia tarehe 21 Agosti huku Mtakatifu Gimignano hadi kwenye Abasia ya Mtakatifu Antimo Agosti 26.

Na Angella Rwezaula – Vatican.  

Toleo la III la majira ya kiangazi linalotolewa kwa wanasemina na wahuishaji wa kijamii wa 'Mpango wa Policoro,' unaohamasishwa na Ofisi ya Kitaifa ya Matatizo ya Kijamii na Kazi ya Baraza la Maaskofu, Italia (CEI), litaanza hivi karibuni. Mpango huo, ambao utafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2023, utajumuisha hatua sita, ukiongozwa na mada: Kuunda Ulimwengu Wazi, ambaoi uliochochewa na sura ya Tatu  ya waraka wa Fratelli tutti. Safari hiyo inawalenga wale wanaotaka kuimarisha mafundisho ya kijamii ya Kanisa ili kufanya utambuzi katika wakati huu. Kwa mujibu wa Padre Bruno Bignami, mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa ya Masuala ya Kijamii na kazi ya  Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na mhamasishsji wa Mpango huo ameileza Radio Vatican/Vatican News kwamba mpango wa safari hiyo ulizaliwa kama wazo la kufanya muda wa kutafakari juu ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa, lakini kwa utofauti, au tuseme na fursa ya kukutana na ukweli halisi.  Kwa hiyo “Jambo la kufurahisha ni kukutana na watu wa ndani ambao huruhusu kupata uzoefu. Fursa ni kujikita katika safari ili kusafiri ambapo kwa upande mmoja wanakutana na mafundishoki jamii ya Kanisa, kwa watu wengine wa mahali ambao kwa namna fulani wanaishi. Mpango huo, kiukweli, unaimarisha mandhari ya safari na juu ya vifungo vyote kati ya watu, kuwa utajiri ulioongezwa, ukilinganishwa na njia ya jadi zaidi.

Thamani ya udugu

Mada ya toleo hilo amabyo ni “Kuunda Ulimwengu Wazi inachukua sura ya tatu ya Waraka wa Fratelli Tutti yaani wote ni ndugu. Waraka wa hivi karibu wa Papa Francisko wa kijamii ambao unaruhusu kushughulikia mada kuu ya udugu kwa wakati huu. Kwa hiyo Padre Bruno alisisitiza kuwa  si mada kuu tu  lakini ni muhimu,  kwa sababu leo ​​hii sote tunahisi umuhimu. Tafakari hiyo pia itakwenda kuimarisha mafundishi ya kijamii, kwa mfano kuhusu mada ya amani na haki. Kwa hivyo, udugu kama ulimwengu ulio wazi, ambao unapingana na ulimwengu uliofungwa ambao tunashughulika nao kila siku, ambao unatufanya tuone uzoefu wa dhambi, wa umbali kutoka kwa Mungu na kutoka kwa udugu kama uwezo wa kujenga kitu kizuri kati ya wanadamu.

Mshangao wa mkutano huo

Padre Bruno, akikumbuka matoleo yaliyopita, alisisitiza kwamba, mwanzoni, washiriki, kutoka kwa ulimwengu wao na kutoka kwa majimbo ya , hawajuani kila mmoja. Lakini, kadiri siku zinavyosonga bele, uzuri wa kukutana kati ya wote unazidi kuota mizizi. Safari ni ya ajabu sana katika kukuza urafiki na ujuzi wa pande zote  kwa sababu inakuwezesha kushiriki masaa pamoja kwenye njia na barabara ngumu. Mara nyingi sana fursa hutokea kwa maungamo, kwa mazungumzo ya kiroho, kwa utafiti wa kina wa mada nyingi. Mengi ya watu wasio rasmi wa kawaida huwa matajiri sana, pamoja na yale yaliyopangwa zaidi, kama vile kujifunza ujuzi wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa.  Ninachokumbuka kwa upendo na shukrani hasa ni wakati ambao tunajitolea kwa kila mmoja njiani, ambayo huturuhusu kujadili na kuzungumza juu ya kila mmoja. Tukumbuke Baba Mtakatifu Franisko akizungumza na vijana waliokuwa wanajishughulisha na kozi ya mafunzo ya kijamii na kisiasa, ndani ya Mpango wa Policoro wa Baraza la Maaskofu wa Italia, mnamo tarehe 18 Machi 2023, Papa alisema kuwa leo hii siasa haifurahii sifa bora, zaidi ya yote kwa sababu haina ufanisi na mbali na maisha ya watu, na kuthibitisha kwamba mwanasiasa mzuri lazima ahusishe watu, kuzalisha ujasiriamali na kuwafanya watu wahisi uzuri wa kuwa mali ya jamii.

Vita ni kushindwa kwa siasa

Vita ni kushindwa kwa siasa. Inakula sumu inayomchukulia mwingine kama adui. Vita hutufanya tuguse upuuzi wa mbio za silaha na matumizi yake kwa utatuzi wa migogoro. Kinachohitajika badala yake ni sera bora, alisema Papa, na kwamba kujielimisha kwa amani na kupingana na vita vingine, vita vya ndani, vita juu ya mtu mwenyewe ili kufanya kazi kwa ajili ya amani. Hatimaye, Baba Mtakatifu aliwaalika vijana wa Mpango wa Policoro kutafakari ni nini mwanasiasa bora anapaswa kufanya na kuhitimisha hotuba yake kwa kutoa ushauri. “Wasiwasi wenu si msaada wa uchaguzi au mafanikio binafsi, lakini kuhusisha watu, kuzalisha ujasiriamali ujasiriamali, na kwamba kufanya ndoto kustawi, kufanya watu kuhisi uzuri wa kuwa mali ya jamii. Ushiriki ni muhimu kwenye majeraha ya demokrasia. Ninawaalika mto umchango wenu, kushiriki na kuwaalika wennzenu kufanya hivyo, fanya hivyo kila wakati kwa lengo na mtindo wa huduma. Mwanasiasa ni mtumishi.”

Toleo la III la Policoro
16 August 2023, 17:33