Papa anasubiriwa kwa hamu huuko Marsiglia Papa anasubiriwa kwa hamu huuko Marsiglia  (AFP or licensors)

Askofu mkuu wa Rabat:Papa anafika Marsiglia kuamsha dhamiri

Kardinali López Romero aliwasili kutoka mji mkuu wa Morocco kwa ajili ya mikutano kuhusu Mediterania,akisubiri kuwasili kwa Papa Francisko: “Hakuna amani bila ushirikiano kati ya mwambao wote wa bahari hii,”alisema huku akitoa wito wa umoja kati ya dini zote ili kuhakikisha uhuru wa kuabudu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Shauku kubwa ya kujenga amani katika Bahari ya Mediterania inawapatia uhai maaskofu 70 ambao wametoka kila ufuko wa bahari hiyo waliofika Marsiglia tangu Jumatano Septemba 20, kwa ajili ya siku mbili kabla ya kuwasili kwa Papa Francisko, 22 Septemba 2023, kuendelea na kazi iliyoanza hapo awali ya  mikutano mjini Bari mnamo mwaka 2020 na Firenze mwaka 2022. Miongoni mwa hawa Kardinali Cristobal López Romero, askofu mkuu wa mji mkuu  Rabat nchini Morocco  ambaye aliongoza Misa ya ufunguzi wa maaskofu 21 Septemba  ​​katika kanisa la La Meja huko Marsiglia. Katika mahojiano na Vatican News  kuhusiana na Kanisa lake nchini mwake  na mikutano hiyo alisema “Sisi maaskofu wa Cerna tuliwapa waamini wetu barua ya kichungaji miaka minane iliyopita, yenye kichwa “Watumishi wa matumaini”.

Mikutano hii kiukweli inaweza kuwa chanzo cha matumaini

Mikutano ya Bari, Firenze na sasa Marsiglia tayari imetusaidia kuelewa kwamba sisi sote ni wa Mediterania, licha ya tofauti zetu. Hii inatualika kuifanya Mediterania isiwe mpaka wa amani, bali amani isiyo na mipaka. Kwa hiyo matunda ya kwanza ya mikutano hii yanapaswa kuthibitishwa kwa amani na kukua katika umoja. Akiendelea alisema: “Kwanza kabisa, tunapaswa kufahamu umoja wetu. Kinachotuunganisha ni muhimu zaidi kuliko kinachotutenganisha. Hii ni mantiki, kwa sababu sisi sote ni maaskofu, tunashiriki imani sawa katika Kristo, ambayo inatuongoza. Kutokana na umoja huu, lazima tuchangie amani na umoja katika Mediterania. Kuna sinema nyingi za migogoro na mivutano katika eneo hili, hebu fikiria Balkan, Kroatia na Serbia, Moroko na Algeria, Ugiriki na Uturuki, Israeli na Palestina, bila kusahau Siria, 'Iraq au Ukraine na Urussi, ambazo ni sehemu ya Bahari Nyeusi na kwa hivyo Bahari ya Mediterania.

Ni lazima tuzingatie kwamba sisi sote ni watu wa kindugu wanaofanya kazi kwa manufaa ya wote, lakini si manufaa ya pamoja ya utaifa bali yale ya ulimwengu mzima. Na kwa nini sio jumuiya ya Mediterranean? Kwa nini kusiwe na ushirikiano wa karibu kati ya mwambao wa kaskazini na kusini na usaidizi kwa mwambao wa mashariki na Mashariki ya Kati? Ninaamini kuwa amani na umoja ni maneno muhimu katika mikutano yetu ya Mediterania.”

Una maoni gani kuhusu hija ya Papa Francisko katika Bahari ya Mediterania, kutoka Lampedusa mwaka 2013, hadi Morocco, hadi nyumbani kwako mwaka 2019, hadi Marsiglia, akitembelea jumla ya nchi 17 zinazopakana na Mediterania?

Takwimu hii tayari ni muhimu na inaleta ujumbe. Ina maana kwamba Papa anatambua umuhimu wa bonde hili la Mediterania na kwamba amejitolea kwake. Kuja Bari, sasa kuja hapa Marsiglia na kusaidia mchakato mzima wa mikutano ya Mediterania. Natumaini uwepo wake hapa unaamsha dhamiri nyingi.

Usimamizi wa  Wakristo, kwenye mwambao fulani wa Bahari ya Mediterania zaidi kuliko wengine, na uhuru wa kidini pia ndio msingi wa mikutano hii. Hii inawezaje kuhakikishiwa katika Mediterania?

Sisi Wakatoliki tunawakilisha sehemu ndogo tu ya ubinadamu katika Mediterania. Kisha, tunapaswa kuzindua miito ya mikutano ya kidini na ya kiekumene ya Mediterania, na Waislamu na Waorthodoksi. Si suala la kutetea tu haki za Wakatoliki au Wakristo, bali ni haki za kila mtu kwa uhuru wa dhamiri na uhuru wa kidini. Wakati Wakatoliki wanateseka katika baadhi ya nchi, Waislamu wanateseka katika nchi nyingine, na Wayahudi ni wahasiriwa wa chuki dhidi ya Wayahudi katika maeneo fulani. Uhuru wa kidini hautapatikana kamwe ikiwa dini hazifanyi kazi pamoja kwa manufaa ya wote.

22 September 2023, 11:47