Mongolia,Video ya 7:kuna utajiri wa imani na ushirikiano mkubwa wa dini
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Hatimaye Baba Mtakatifu amefika na kuikumbatia nhi ya Mbali ya Katikati mwa Bara la Asia, ambayo kwa muda mrefu alikuwa na shauku ya kuitembelea. Lakini swali linakuja je ni “Kwa nini Papa amekwenda Mongolia? Hata hivyo siku chache kabla ya Papa Francisko ua kuondoka kuelekea Ulaanbaatar, nchini humo watu wengi walishangaa ni kwa nini kinamsukuma Papa huyo mwenye umri wa miaka 87 kufanya safari ndefu ya kutembelea taifa ambalo wanaishi Wakatoliki wasiozidi elfu mbili. Uchambuzi ulianza kusambaa ambao unarejea umuhimu wa kimkakati wa safari ya upapa kwenda nchi iliyoko kati ya Urusi na China, yenye mawazo ya kuvutia mara nyingi. Jambo ambalo huwa la kufurahisha zaidi mtu akitambua na kutoondoa nguvu za kitume ambazo kwa kawaida huonesha kila safari ya upapa.
Kwa hiyo katika Ripoti ya saba na ya mwisho ya video iliyotolewa na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisonari Fides na Teresa Tseng Kuang yi katika matazamio ya safari ya Papa Francisko ya kwenda Mongolia kuanzia tarehe 31 Agosti hadi tarehe 4 Septemba 2023, inafafanua wazi juu ya matarajio makubwa ya Papa katika nchi kubwa ya Asia ya Kati na katika Kanisa lake dogo ambalo lakini ni hai kabisa. Na kupitia picha, historia na shuhuda zilizokusanywa nchini Mongolia, inaruhusu kabisa kuingia katika Nchi hiyo na sababu za safari hiyo katika Kundi dogo la wakatoliki wapatao 1500 tu.