15 Oktoba sala ya Rosari kwa ajili ya Amani Nchi Takatifu
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Ofisi ya Habari na Mawasiliano kijamii ya Jimbo Kuu,Jumanne tarehe 10 Oktoba 2023,ilitoa taarifa kuwa Jimbo kuu la Roma linatoa mwaliko kwa waamini wote na wenye mapenzi mema kushiriki sala ya Rosari Takatifu kwa ajili ya kuombea Amani ya Nchi Takatifu tukio litakalofanyika Dominika tarehe 15 Oktoba 2023, saa 3.00 kamili usiku, Mbele ya Uwanja wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu Roma, na ambayo itaongozwa na Makamu wa Papa, Kardinali Angelo De Donatis.
Kwa njia hiyo taarifa hiyo imebainisha kwamba kwaWaandishi wa Habari na wahudumu vya vyombo vya Habari wanaotarajia kushiriki, wanapaswa watume maombi ndani ya masaa 48 kabla ya tukio hilo, kwa namna ya pekee kupitia mfumo wa uidhinishaji mtandaoni wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican kwa anuani ifuatayo:press.vatican.va/accreditamenti.