CEI yatoa mwaliko wa kusali kwa ajili ya Amani Nchi Takatifu Oktoba 17
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kwa kuunga mkono wito wa Patriaki wa Yerusalemu ya Kilatini, Kardinali Pierbattista Pizzaballa alioutoa kwa ajili ya siku ya Jumanne tarehe 17 Oktoba 2023 kwa sala, kufunga na kujinyima kwa ajili ya amani na upatanisho kwa sababu Mashariki ya Kati haihitaji vita, bali amani, amani iliyojengwa juu ya haki, mazungumzo na ujasiri wa udugu, hata Baraza la Maaskofu Katoliki Italia(CEI)limeamua kufanya siku hiyo kuwa ya kitaifa. Katika ujumbe wake aliouandika tarehe 11 Oktoba 2023, Kardinali Pizzaballa; alikiri kwamba uchungu na kwiwi kwa kile ambacho kinatokea ni kikubwa.
Chuki inazidi kongezeka
Kardinali anaabainisha kuwa kwa mara nyingine tena wanajikuta katikati ya mgogoro wa kisiasa na kijeshi. Wamejikuta ghafla wanaogelea kwenye bahari ya vurugu na ghasia ambazo hazijawahi kusikika. Chuki ambayo kwa bahati mbaya tayari wanafanya uzoefu kwa siku nyingi itazidi kuongezeka tena zaidi na kuvuta ghasia ambazo zitaonesha matokeo na kuunda uharibifu. Yote utafikiri ni kuzungumza kifo. Lakini kwa wakati huu wa uchungu na kwikwi, hawataki kubaki bila kujilinda. Na hawawezi kuacha kwamba kifo na makucha yake (2Kor 15,55)viwe ndiyo neno la kusikia.
Hitaji la kuomba kwa Mungu baba
Kwa njia hiyo wanahisi hitaji la kusali na kuelekeza mioyo yao kwa Mungu Baba. Ni kwa njia hiyo tu wanaweza kuchota nguvu na utulivu wa kuishi katika wakati huu, kwa kumwelekea Yeye katika sala ya maombi, ya kumuomba na hata kwa kilio. Kwa hiyo tarehe iliyochaguliwa kwa kutaka ushirika na Wakristo wa Nchi Takatifu kulingana na maelekezo ya Kardinali Pizzaballa, ambaye kwa niaba ya wanajumuiya wote, aliomba jumuiya za mahalia kukutana kama kwaya kwa ajili ya sala, ili kumkabidhi Mungu Baba kiu yao ya amani, haki na upatanisho tarehe 17 Okotba 2023.
CEI inaomba kusali na majitoleo kitaifa
Katika muktadha huo kwa wakati huu wa maumivu makubwa na wasiwasi mkubwa wa kuongezeka kwa vurugu katika nchi za Mashariki ya Kati ndiyo, mwaliko wa Urais wa Baraza la Maaskofu Italia CEI unaoelekeza Jumuiya za majimbo yote kitaifa ili kujiunga na mpango huo wa Ombi la Patriaki wa Yerusalemu. Na wakati huo huo, Dominika tarehe 15 Oktoba 2023, katika maadhimisho yote ya Ekaristi Takatifu, nia hiyo inaweza kupitishwa kwa wote kwa sala hii: “Baba mwenye huruma na nguvu: 'wewe si Mungu wa machafuko, bali wa amani'. Zima chuki, vurugu na vita katika Nchi Takatifu, ili upendo, maelewano na amani viweze kustawi tena. Tuombe".