Safari kuelekea siku ya Kimisionari na mioyo inayowaka Oktoba 22

Shukrani kwa michango ya wamisionari,watawa na walei,tunajaribu kueleza kwa maneno rahisi maana ya kuwa na moyo unaowaka na miguu inayotembea.Barani Afrika tunafanya kazi ili nchi zote ziwe na ujumbe wa Siku ya Utume wa Kimisionari Duniani katika lugha yao ya asili.Venezuela ‘Wamisionari wanaoshiriki mkate na kushiriki maisha.’

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari(Fides) limefafanua  hali halisi ya mipango mbali mbali ya uhuishaji wa kimisionari ambayo Kurugenzi za Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa duniani kote zimezindua katika miezi hii  katika  maandalizi ya Siku ya Kimisionari Duniani kwa Mwaka 2023 itakayoadhimishwa Dominika, tarehe 22 Oktoba 2023, imeangukia katika mazingira ya ndani. "Mioyo inayowaka, miguu inayotembea"  ni kauli mbiu inayojikita kuakisi  Siku iliyowekwa  ya Utume wa Kisimisonari kama ilivyoonesha na Baba Mtakatifu katika Ujumbe wake kuelekea  kilele cha  Siku hii na ambayo inatoa msukumo kutoka katika historia ya wanafunzi wa Emau, katika Injili ya Luka (rej. 24,13-35). Ujumbe huu unarudi kama kielelezo kwenye karatasi na nyenzo pepe iliyotayarishwa, katika tafakari na katekesi inayotolewa, katika shughuli zinazopendekezwa kwenye mabara yote. Pia mwaka huu 2023, kama matokeo ya harambee kati ya Kurugenzi za PMS, zinazoratibiwa na Kurugenzi za Malta na Australia, video ya kimataifa ya kusherehekea Siku ya Kimisionari Duniani 2023 imefika katika  Shirika la Kipapa la Habari za kimisionari (Fides) ambapo ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha  shughuli za PMS "@wearestillhere" yaani, (bado tuko hapa), iliyozinduliwa miaka 4 iliyopita, katikati ya janga la uviko.

Shukrani kwa michango ya wamisionari, watawa na walei, tunajaribu kueleza kwa maneno rahisi maana ya kuwa na moyo unaowaka na miguu inayotembea. Ni dakika tatu ambapo ulimwengu wote "unapitiwa" na dhamira ya PMS inaoneshwa, shukrani kwa msaada wa picha na muziki unaosikika. Wakati huo  zile zilizoundwa na Kurugenzi za Italia, Scotland na Canada ni mfululizo halisi wa video zinazopata msukumo kutoka kwa maisha ya kawaida ya wamisionari wengi wanaofanya kazi kimya  kimya na kwa kuvuna matunda katika jiji kama  vile katika pembe za mbali zaidi za dunia. Miongoni mwao ni Sr Mary ambaye anafanya kazi katika mtaa wa mabanda wa Kibera nchini Kenya na ambaye anazungumziwa katika kampeni ya kuchangisha pesa ya PMS ya Kiingereza katika Dominika Oktoba  22. Kwa hiyo hadi kufikia Dominika tarehe 22, itawezekana kutembelea seminari ya Conciliar "El Domund al descubierto"("Siku ya Wamisionari Ulimwenguni hadharani") huko Pamplona, Jengo halisi, lililobuniwa na Shirika moja la  Hispania miaka 9 iliyopita, na lengo la kuhamaisha utume kati ya watu kupitia maonesho na matukio yanayohusiana.

Barani Afrika tunafanya kazi ili nchi zote ziwe na ujumbe wa Siku ya Utume wa Kimisionari  Duniani katika lugha yao ya asili. Usimamizi wa PMS wa Guinea Bissau mwaka huu 2023 umejitolea kutoa nyenzo zote za uhuishaji katika lugha ya Krioli. Nchini Kamerun lengo lake  badala yake ililenga mafunzo ya wanasemina ambao katika kila Jimbo watahamasisha ufadhili wa Dominika ya kimisioanri , wakati huko Nigeria mwezi wa umisionari utamalizika na Kongamano la Kitaifa la Wamisionari huko Owerri lililopangwa kufanyika  Jumanne tarehe 24 hadi 27 Oktoba 2023 .

Nchini Amerika ya Kusini uongozi wa Venezuela umechagua kuelekeza kampeni ya uhuishaji wa kimisionari kwenye mada "wamisionari wanaoshiriki mkate na kushiriki maisha." Nchini Costa Rica, kama inavyotokea katika nchi nyingi duniani, Misa Takatifu itatangazwa kwenye televisheni ya taifa na parokia ya wamisionari; Wakati huo huo nchini Brazil kazi kubwa ilifanyika katika kuwasilisha mada ya Siku, kuanzia nembo ambayo inawakilisha  moyo ambamo msalaba unatokea hna kuleta  ladha ya utamaduni wa kiasili wa Amazonia. Hii ina maana ya utafutaji wa njia mpya za shughuli ya umisionari kulingana na uzoefu wa Kanisa huko Amazonia. Katika  Bara la Asia, miongoni mwa mipango tunaona ile ya PMS ya Taiwan na pia katekesi ya Kurugenzi ya PMS  huko India na kujitolea kwa PMS ya huko Japan katika tafsiri na usambazaji wa nyenzo za uhuishaji za kimisionari kati ya watu.

PMS yahamasisha siku ya Kimisionari duniani 22 Oktoba 2023
21 October 2023, 10:21