P.Patton,Nchi Takatifu:upatanisho ni kutambua mateso ya wengine
Na Amedeo Lomonaco, na Angella Rwezaula, - Vatican.
Makubaliano, kuachiliwa kwa mateka na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina asubuhi ya tarehe 26 Novemba 2023 katika habari ya mabadilishano mapya, baada ya yale ya tarehe 25 Novemba na siku chache zilizopita ni mwanga wa mwanga. Ni hatua zinazochukuliwa kupitia mchakato wa mazungumzo unaoambatana na matokeo ya kutia moyo: "ina maana kwamba mazungumzo yanawezekana.".Haya ndiyo alisema Padre Francesco Patton,(OFM), Msimamizi wa Nchi Takatifu, katika mahojiano na Radio Vatican - Vatican News, ambaye ameona mwanga katika vita hii iliyoanza tangu tarehe 7 Oktoba na hadi sasa na imegharimu maisha ya watu wasiopungua elfu 15. "Basi tunahitaji kuona kwamba makubaliano ya amani yanashikilia na kwamba mateka wote wameachiliwa. Na juu ya yote tunahitaji kuhama kutoka katika lugha ya silaha hadi mazungumzo."
Njia tofauti na ile ya silaha
Katika njia ambayo imesababisha matunda madhubuti, kama vile kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa, Padre Patton pia alisema "umuhimu wa jumuiya ya kimataifa, hasa kwa uingiliaji kati wa baadhi ya nchi". Imeonekana kwamba inawezekana kufuata njia tofauti na ile ya silaha, ikiwa utashi mwema upo". Suluhisho, alisema msimamizi wa `nchi Takatifu, kuwa sio tu kuwaachilia mateka na wafungwa. Kwanza kabisa, lazima iwe ya kisiasa: "lazima tufikie "kukubalika kwa pande zote kwa haki ya kuwepo" kwa Israeli na Palestina ili kufanya "usahili wa serikali" iwezekanavyo.
Sauti za matumaini
Katika hali ya kushangaza, kama ile inayosambaratisha Mashariki ya Kati, sauti muhimu, inamkumbukwa na Padre Patton, "ni ile ya kibinadamu, ya dhamiri ya mwanadamu kwa sababu inaakisi thamani isiyoweza kulinganishwa ya kila mwanadamu. Bila sauti za kufariji na kutuliza za sauti ya kibinadamu hatuwezi kusonga mbele kwa sababu kila kitu kinapunguzwa kwa hesabu, kwa usawa wa maslahi, kwa matumizi ya vurugu".
Jukumu la Wakristo
Katika Nchi Takatifu - alisema Padre Patton - Wakristo "wanawakilisha, kwa namna fulani, dhamiri na ni daraja kati ya ukweli mbili kwa sababu ya wote wawili kwamba: "Tuna Wakristo kutoka Nchi Takatifu katika Israel, huko Gaza, katika Ukingo wa Magharibi na kwa sababu hii wanaweza kufanya kazi, ingawa ni ndogo, hata iwe muhimu." Nchi Takatifu inahitaji nuru, chachu inayofanya sauti ya dhamiri kukua katika jamii ya Waisrael na Wapalestina, ambapo ni lazima kuwe na sauti zenye mamlaka, na sio tu kati ya Wakristo lakini pia kati ya Waislamu wenye uwezo wa kupendekeza njia, si kwa kiasi tu, bali kwa ajili ya upatanisho.” Hii, alisisitiza, inatumika kwa pande zote mbili.
Lengo la upatanisho
Kulingana na Padre Patton, hadi "ushiriki wa kihisia unaochochewa na janga za vita utakaposhindwa, itakuwa vigumu kuzungumza juu ya upatanisho. Lakini wakati sehemu ya kihemko inapokuwa shwari itawezekana kutekeleza aina zingine za hoja". Jambo muhimu, alisisitiza, ni kwamba mapatano ya amani yanashikilia, kwamba mateka wameachiliwa, na kwamba kuna heshima kwa raia huko Gaza pia na kwamba wakati huu wa ukimya wa silaha unaweza kuruhusu washawishi mbalimbali wa kimataifa kuendelea kufanya kazi. " Matumaini, alifafanua Padre Patton, ni kwamba tunaweza kuondoka kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwasili kwa haraka iwezekanavyo, katika mfumo wa ulinzi wa kimataifa ili kuhakikisha usalama." Kisha upatanisho wa kimataifa lazima pia uungwe mkono ili kupata suluhisho la kisiasa, vinginevyo hali sawa na hiyo itatokea tena katika siku zijazo.
Kutambuana uwepo wa haki ya kila mmoja
Dimbwi la vita, limebainishwa na Msimamizi wa Nchi Takatifu, kwa mara nyingine tena kwamba limefichua tatizo la msingi katika Mashariki ya Kati hasa kwa : "kukosekana kwa suluhisho la kisiasa katika suala la Kipalestina ambalo limeendelea kwa miongo kadhaa". Suala la Palestina linahusiana kwa karibu na lile la Israel na ambalo: lazima tufikie "kutambua haki ya kuishi." Na lazima ikumbukwe kwamba wao ni watu wawili ambao, katika historia yote, wameteseka sana. Kwa hakika 'mzigo' huu mkubwa na wa kushangaza, unapaswa kuwaongoza Waisraeli na Wapalestina "kutambua mateso ya pande zote mbili." Msimamizi Nchi Takatifu kwa hiyo alikumbuka kile kilichosemwa katika mahojiano yaliyotolewa kwa na Gazeti la Osservatore Romano na Rachel Goldberg, mwakilishi wa familia za mateka kwamba: "Lazima tujifunze kutambua mateso yao na wanapaswa kujifunza kutambua mateso yetu". Kwa njia hiyo, tunaweza kuchukua hatua mbele.
Kutazama heshima ya mateso ya wengine
"Sijui kama suluhisho madhubuti linaweza kuwa la Mataifa mawili au kitu kingine, lakini haki ya kuwepo kwa mataifa yote mawili lazima itambuliwe na lazima kuwe na kutambuliwa kwa mwingine, kwa haki ya kuwepo kwa mwingine, utambuzi wa mateso ya mwingine”. Na pia utambuzi wa hadhi ya mateso ya wengine". Kuzingatia mateso ya mtu binafsi, hata hivyo, kutasababisha ugumu zaidi tu", alisisitiza Padre Patton.
Ili kuweza kufanya mazungumzo Padre Patton aliendelea kuwa pande zote zinahitaji "uungwaji mkono wa nje"kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, lakini hii lazima ifanyike kupitia mchakato wa kusindikiza inayojumuisha awamu ya mpito. "Ni dhahiri kwamba kitu lazima kibadilike kwa kina katika mtazamo wa chama cha kisiasa cha Israel na lazima kuwe na mabadiliko ya mtazamo, ambayo yana uthabiti zaidi, pia kwa upande wa ulimwengu wa Palestina,"alihitimisha Msimamizi wa Nchi Takatifu, Padre Patton (OFM).