Wito wa Patriaki Pizzaballa:Kilio cha watu kinasikika tunaomba msaada wenu
Bwana awape amani!
Kaka na dada, Upendo na sala huhuisha familia nzima ya Upatriaki wa Kilatini ya Yerusalemu, hasa katika nyakati za shida kubwa. Maisha mengi yameokolewa na mateso mengi yamepunguzwa shukrani kwa usaidizi wenu katika miito ya hivi karibuni kuanzia na: Uviko-19, Gaza 2021; mlipuko wa bandari ya Beirut na tetemeko la ardhi huko Siria na Uturuki. Katika hali zote hizi tumesikiliza na kujibu kilio cha maskini. Kwa mara nyingine tena kilio chao kinasikika katika Nchi Takatifu kutokana na vita hivi vilivyodumu kwa zaidi ya majuma matatu sasa. Mgogoro wa sasa sio tu umesababisha vifo, uharibifu na njaa huko Gaza, lakini pia ukosefu mkubwa wa ajira, hasa katika eneo la Bethlehemu, na matatizo mengine ya kijamii katika Nchi Takatifu. Tunakabiliwa na janga ambalo linaathiri familia nyingi za dini tofauti na taasisi zetu zote, pamoja na shule, hospitali na parokia. Huko Gaza, rasilimali zetu za nyenzo zimepanuliwa zaidi ya kuta zetu ili kujumuisha majirani wanaoteseka na wale ambao wamekimbilia mahali pengine.
Roho ya uratibu ilionekana, kwani washiriki wa eneo hilo pia walisaidia. Tunashiriki karibu kila kitu, kuanzia chakula hadi maji, kutoka dawa hadi vifaa vingine. Katika wakati huu mgumu tumejifunza kwamba ili kujenga upya ulimwengu wa kimwili ni lazima kujenga na kulinda uaminifu kati ya watu. Mamia ya watu kutoka duniani kote wamewasiliana nasi na tayari wametusaidia kutoa usaidizi thabiti. Tunajua tunachopaswa kufanya. Tumefanya hivi kwa moyo wote katika mizozo iliyopita na bila shaka tutafanya hivyo tena. Tusaidie kuzalisha tena muktadha unaohitajika ili, katika jamii hii yenye chuki, mbegu za uaminifu, matumaini na upendo bado ziweze kupandwa. Ninawahakikishia maombi yangu na shukrani kwa kila mmoja wenu!
Katika Kristo.
Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Yerusalemu.
Anahitimisha wito wake Patriaki wa Kilatini huko Yerusalemu, katika matumaini kwamba watu wote ambao watakuguswa na wenye mapenzi mema wanaweza kuendelea kutoa msaada wao wa hali na mali katika kuweza kukabiliana na hali halisi hii ngumu ya watu wasio kuwa na hatia ambao ndio wa kwanza kufa katika vita hivi vya kipuuzi.