COMECE kuhusu matokeo ya COP28:wasiwasi wa utekelezaji kwa vizazi vijavyo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa (COP28),kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika huko Dubai kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023, Padre Manuel Barrios Prieto, Katibu Mkuu wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya(COMECE) ametoa maoni yake Jumatano tarehe 13 Desemba 2023 kuwa: “COMECE inakaribisha makubaliano kuhusu baadhi ya masuala muhimu, kama vile kushughulikia Hasara na Uharibifu kwa dhati na kukomesha nishati ya mafuta kwa njia ya haki."
Utunzaji wa Nyumba yetu ya pamoja na haki kwa vizazi
Wakati huo huo Padre Prieto anaakisi jambo jingine kuwa: “Tuna wasiwasi kwamba lugha isiyoeleweka inaweza kuonesha ukosefu wa kujitolea kwa dhati. Tunatoa wito kwa wahusika kuondokana na masilahi ya upendeleo na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya manufaa ya wote, utunzaji wa Makao yetu ya Pamoja na haki kati ya vizazi.”
Kwa upande wa Francescon, Mkuu wa ajenda ya Ikolojia ya Umoja Wabuddha wa Italia kuhusu Cop28 alisema: “Makubaliano ya Dubai yanaweza kuweka misingi ya kukomesha enzi ya nishati ya mafuta mapema haya muongo huu.
Katika maoni ya Silvia Francescon, mkuu wa Agenda ya Ikolojia ya Umoja wa Wabudha wa Italia akitoa maoni yake alisema kuwa: “Nakala iliyopitishwa huko Dubai ina uwezo wa kuweka misingi ya mwisho wa enzi ya nishati ya mafuta mapema hata kwa muongo huu. Sasa ni wakati wa utekelezaji, wa kuoanisha mipango ya kitaifa kwa lengo la kudhibiti ongezeko la hewa chafu hadi 1.5 °C, kwa ajili ya kutimiza ahadi zilizopitishwa huko Dubai za kuongeza vyanzo mara tatu vya nishati mbadala na ufanisi maradufu wa nishati, pamoja na kufuatilia ahadi za fedha za tabianchi.”
Matumizi ya kanuni za Ikolojia kwa uzalishaji chakula
Kwa upande huo alieleza kuwa: “Marejeo ya teknolojia fulani, kama vile CCS, lazima yafuatiliwe kwa uangalifu ili kuzuia kufunguliwa kwa (greenwashing) yaani kuosha kijani na umakini sawa lazima ulipwe kwa mabadiliko ya mifumo ya chakula ambayo haiwezi kukabidhiwa suluhisho za uwongo za kiteknolojia, (Agroecology)yaani matumizi ya kanuni za ikolojia katika uzalishaji wa chakula, mafuta, na madawa pamoja na usimamizi wa mifumo ya kilimo na kilimo cha kuzalisha upya vimethibitisha kwamba ni dawa bora zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.” Alihitimisha Francescon.