Kila tarehe 4 Januari Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu  Angela wa Foligno. Kila tarehe 4 Januari Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Angela wa Foligno. 

4 Januari ni kumbukizi ya Mtakatifu Angela wa Foligno:‘Nafasi yangu ni duniani’

Mtakatifu Angela wa Foligno Mfransiskani Msekulari(OFS)(Foligno,1248-4 Januari1309)alikuwa wa ibada ya kina ya fumbo na wa elimu ya juu,aliyetangazwa mwenyeheri 1693 na Papa Innocent XII na kutangazwa Mtakatifu na Papa Francisko mnamo tarehe 9 Oktoba 2013. “Uzoefu wa waamini wa kweli unatuwezesha kwa majaribio kujua, kupenya na kugusa Neno la uzima ambaye alifanyika mwili."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kila tarehe 4 Januari ya kila mwaka, Mama Kanisa anamkumbuka kiliturujia, Mtakatifu Angela wa Foligno. Ni Mtakatifu Mtawa wa Shirika la Wasekulari(OFS) la Mtakatifu Francis wa Assisi nchini Italia mara baada ya kifo cha mumewe na watoto wake, akifuata nyayo za Mtakatifu Fransis, alijitoa kikamilifu kwa Mungu na kukabidhi uzoefu wake wa kina wa maisha ya fumbo kama inavyoeleza wasifu wake juu ya uzoefu wake wa maisha ya ibada ya kina(Mysticism of Passion,Penance and Divine Darkness) hasa alipotambua kwamba "ili kumtumika vema na kufanana na Bwana aliitwa kuishi utakatifu katika uthabiti wa maisha ya kila siku." Kwa hiyo  Angela alizaliwa Foligno nchini Italia mnamo 1248 katika familia tajiri na mapema alibaki yatima kwa kumpoteza baba yake  na wakati huo huo akapata elimu ya juujuu  tu kutoka kwa mama yake ambayo ilimfanya atumie ujana wake wa kuwa mbali na imani. Alikuwa mzuri sana, mwenye akili, mwenye shauku na  hivyo akaolewa na mwanamme mashuhuri huko Foligno ambaye alizaa naye watoto kadhaa.

Maisha mabaya na kutojali kwa ujana wake  hata hivyo kulipinduliwa katika muda wa miaka michache na mfululizo wa matukio kwa mfano, tetemeko la ardhi kali la mnamo mwaka 1279, kimbunga cha haraka na kisha vita vya muda mrefu dhidi ya Perugia vilimfanya ajiulize juu ya hatari ya maisha na kuhisi hofu ya kuzimu. Tamaa ya kukaribia sakramenti ya kitubio ilizaliwa ndani yake, lakini, kulingana na historia  yake, aibu ilimzuia kukiri kikamilifu na kwa sababu hiyo alibaki katika mateso. Kwa kusali Angela alipata hakikisho kutoka kwa Mtakatifu Francis wa Assisi kwamba mapema angeweza kujua huruma ya Mungu. Angela kisha alirudi kwenye maungamo na wakati huo huo alikuwa amepatanishwa kabisa na Bwana. Katika umri wa miaka 37, licha ya uhasama wa familia yake, uongofu wake ulianza kama ishara ya toba na kujikatalia mambo, mapenzi  yake binafsi.

Mtakatifu Angela wa Folignoa 4 Januari
Mtakatifu Angela wa Folignoa 4 Januari

Angela mara baada ya kifo cha mapema cha mama yake, mume na watoto, mwanamke huyo aliuza mali yake yote na kugawa mapato kwa maskini, huku akaenda kuhiji huko Assisi kilomita chache  kutoka Foligno hasa  kwa kufuata nyayo za Poverello yaani Maskini Francis wa Assisi na mnamo mwaka 1291 alijiunga na Utawa  wa Tatu la Mtakatifu Francis wa wakati ule huku akijikabidhi kwa mwongozo wa kiroho wa Ndugu Arnaldo, ambaye pia walikuwa na undugu wa damu na  ambaye baadaye alikuwa mwandishi wa wasifu wake, katika wasifu wake wa ‘Kumbukumbu’ maarufu.' Katika maandishi hayo kwenye kumbu mbu hatua za wito wa Angela na furaha yake ya mara kwa mara na uzoefu wa fumbo, unaofikia kilele cha kukaa ndani ya nafsi ya Utatu Mtakatifu, imegawanywa katika “Hatua” thelathini. Mojawapo ya vifungu vya hatua hizo vinabainisha kuwa: “Niliona kitu kilichojaa,” alimwambia muungamishi wake kuhusu ono la Mungu wa Utatu, “utukufu mkubwa sana, ambao siwezi kusema, lakini ilionekana kwangu kwamba yote yalikuwa mazuri. (…)

Siku Kuu ya Mtakatifu Angela wa Foligno, 4 Januari

Baada ya kuondoka kwake, nilianza kupiga kelele kwa sauti kubwa (…) Upendo usiojulikana, kwa nini unaniacha?.”  Kwa hiyo kijana aliyekuwa na hofu ya kulaaniwa kwa maovu yake, alianza kuacha nafasi ya ufahamu wa kutoweza kujiokoa yeye mwenyewe kwa njia ya mastahili yake, bali  kwa  njia ya roho iliyotubu,na kwa njia ya upendo usio na kikomo wa Mungu. Mwelekeo wa maombi wa kudumu, uliooneshwa hasa katika kuabudu na kusali mbele ya Ekaristi, na siku zote Angela uliunga mkono kwa shughuli za upendo pamoja na maskini zaidi, kusaidia wenye ukoma na wagonjwa ambao ndani yao alimwona Kristo Msulubiwa. Akiwa tayari anajulikana maishani kama Magistra Theologorum, yaani kama Mwalimu wa Taalimungu, alihamasisha taalimungu inayojikita katika Neno la Mungu, juu ya utii kwa Kanisa na uzoefu wa moja kwa moja wa Mungu katika udhihirisho wake wa karibu zaidi. Akiwa amehusika kwa shauku katika mabishano yaliyorarua shirika la Wafransikani, wakati ule, Angela alivutia karibu kwa sifa yake   kwa watoto wa kiroho ambao walimwona ndani yake kama mwongozo na mwalimu wa kweli wa imani na kwa sababu hiyo sura yake ilijumuisha moja ya mifano ya fikra za kike katika Kanisa. Tayari hata kabla ya kifo chake, ambacho kilitokea huko Foligno mnamo  tarehe 4 Januari 1309, na kuzika huko katika Kanisa la Mtakatifu Francis, watu walimpatia jina la Mtakatifu kwa njia isiyo rasmi. 

Mtakatifu Angela wa Foligno
Mtakatifu Angela wa Foligno

Ibada yake ilitambuliwa tarehe 7 Mei 1701. Na mnamo tarehe 9 Oktoba 2013, Baba Mtakatifu Francisko alikamilisha kile ambacho watangulizi wake walikuwa wameanzisha kumtangaza Angela wa Foligno kuwa Mtakatifu kwa usawa. Kwa njia hiyo Angela aliishi kwa mfano wa  Mtakatifu Fransis wa Assisi katika toba na kumwiga Yesu Kristo kwa kiasi kikubwa, huku akitafakari juu ya Mateso yake, kama vile Margherita wa Cortona na baadaye, Camilla wa Varano, yaani, Maskini Clara, Sr. Battista. Tukirudi katika maandishi ya “hatua thelathini” Angela alisimulia kile kilichotokea katika nafsi yake, tangu wakati wa uongofu wake hadi 1296, wakati maonesho haya ya fumbo yaliyogawanyika zaidi na kutoa njia ya udhihirisho mpya wa kiroho, hasa ule wa ‘umama wa kiroho’ ambao ulikusanyika karibu na ‘Lella wa Foligno" kama ukweli wa karamu za kiroho zinazotamani ukamilifu. Angela alikuwa akiwatumia barua nyingi na pia walikuwa wakipata farraja ya  afya yao. Umaskini, unyenyekevu, upendo, amani ndizo zilikuwa mada zake kuu. Kwa sababu aliandika kuwa: “Mema kuu ya roho ni amani ya kweli na kamilifu ... basi yeyote anayetaka pumziko kamili na ajaribu kumpenda Mungu kwa moyo wake wote; Mungu, ambaye peke yake anatoa na anaweza kutoa amani. Mtakatifu Angela anabainisha kuwa: “Uzoefu wa waamini wa kweli unatuwezesha kwa majaribio kujua, kupenya na kugusa Neno la uzima ambaye alifanyika mwili, kama yeye mwenyewe anavyoahidi katika Injili: “Mtu akinipenda, alishike neno langu. Kisha Baba yangu atampenda na tutakuja kwake na kuishi ndani yake” (Yh 14:23); na tena: “Kwa wale wanaonipenda, nitajidhihirisha.” Kwa wale walio waaminifu kwake, Mungu huwapa uzoefu huu na fundisho la uzoefu huu kwa ukarimu wa hali ya juu." (Rej 8]

Uzoefu.

Angela anapozungumza kuhusu uzoefu anarejea utimilifu wa ahadi hiyo, ambayo kwa hiyo inakuwa kweli kwa nafsi yake. Uzoefu haudokezi tu kile anachohisi, anachohisi, anachokiona, lakini kwa usahihi kabisa wa uzoefu, kwa nafsi yake, wa ahadi ya Yesu. Si hivyo tu, bali ana ujuzi wa uzoefu huu, yaani, anaweza kutengeneza yake, ingawa kwa njia duni na hii ni zaidi hivyo zaidi kuthubutu njia yake inakuwa. Kwa hiyo uzoefu huo una pande mbili, moja juu ya ubinadamu wake iliyohusika kikamilifu na zaidi katika hamu yake kwa Mungu na moja juu ya uwezekano wa kusema 'Mungu' kwa maneno ya kweli kutokana na uzoefu alionao Kwake. Ni kile, hasa katika Maagizo, anachokiita 'maarifa ya Mungu na ujuzi wa nafsi', ni kama  pande mbili za sarafu moja. Aina hii ya 'maarifa' ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko unaohusisha nafsi na Mungu katika uhusiano unaozidi kuwa wa karibu na wa fumbo.

Kwa hiyo mvutano wa Angela kwa Mungu ni fumbo la maisha yake. Katika kifungu cha kumi na tisa, baada ya simulizi la uzoefu mkuu wa kwanza wa utamu wa Mungu katika kutafakari ubinadamu na umungu wa Kristo, hata kabla hajapata fursa ya kugawanya mali zake zote kwa maskini, aliacha shauku yake iseme.  “Bwana, ninachofanya ni kukupata tu. Nitakupata kila kitu kitakapokamilika?" na mara baada ya: “Sitaki dhahabu wala fedha, na kama ungenipa ulimwengu mzima, nisingependa chochote ila Wewe tu”.[11] Tukizungumza juu ya faida saba maalum ambazo hutolewa na wema wa Mungu, tunaona mvutano wa roho yake kwa maneno haya: “Zawadi ya sita ni zawadi ya hekima. Bwana, nifanye nistahili kujua na kuelewa upendo wa dhati ambao umetupa zawadi ya hekima yako. Kweli, hii ndiyo zawadi ya karama: kuweza kukupitia katika ukweli!”. [12]

Imani  kwa Angela ina nguvu hii ya uzoefu, kama anavyoripotiwa katika hatua ya kumi na saba akisema: “Kwa kulinganisha, imani niliyokuwa nayo hadi sasa ilionekana kwangu kuwa imekufa na machozi yangu ya zamani yalikuwa matokeo ya jeuri. Kuanzia wakati huu kiukweli niliteseka ukweli wa mateso ya Kristo na uchungu wa Mama wa Kristo: basi, chochote nilichofanya, hata kama kikubwa, kilionekana kidogo kwangu, na nilitamani toba kubwa zaidi. Hivyo nilijizika katika mateso ya Kristo na nikapewa tumaini kwamba ndani yake ningepata uhuru wangu.” [13] Ni kile ambacho, siku zote katika kifungu kile kile, alikuwa amekifahamu siku ya Kwaresima wakati, akiwa amejitenga nyumbani na kutafakari juu ya kifungu cha Maandiko, alichomeka kwa hamu ya kuwa na ufahamu kamili juu yake kuwa: “Unataka kupata uzoefu ninachokuambia? ... Kisha yule aliyeniongoza akaongeza kwamba akili ya Injili ilikuwa ni kitu cha juu sana ambacho mtu akiielewa, si tu kwamba angesahau kila kitu cha kidunia, bali pia yeye mwenyewe kabisa ... Kuanzia siku hiyo na kuendelea, uhakika mwingi na nuru nyingi sana na upendo kwa Mungu, hivi kwamba niliendelea kurudia, nikisadikishwa kabisa, kwamba hakuna kitu kinachohubiriwa kuhusu furaha ya Mungu.[14]

Sala kwa Mtakatifu Angela wa Foligno

Hakika tunaweza kujifunza taalimungu ya kiroho ya Mtakatifu Angela wa Foligno. Kwa hiyo Maombi ya Mtakatifu Angela wa Foligno ni maombi yenye nguvu ambayo hutuongoza kuelekea kumjua Mungu na mabadiliko ya ndani. Kupitia maombi haya, tunaweza kupata muungano wa kina na Mungu na kupokea neema yake: “Ee Mungu, chanzo cha nuru na upendo wote, tafadhali angaza akili na mioyo yetu. Utujalie neema ya kuelewa mafumbo yako na kuishi sawasawa na mapenzi yako. Mtakatifu Angela wa Foligno, wewe uliyepata furaha ya kimungu, utuombee ili tuwe wazi kwa uwepo wa Mungu katika maisha yetu.” Amina.

 

 

03 January 2024, 17:46