Tafuta

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema, anasimikwa rasmi kuwa Kiongozi mkuu wa KKKT, Dominika tarehe 21 Januari 2024 Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema, anasimikwa rasmi kuwa Kiongozi mkuu wa KKKT, Dominika tarehe 21 Januari 2024  

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa Mkuu wa Kanisa la KKKT, Tanzania

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema, anasimikwa rasmi kuwa Kiongozi mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dominika tarehe 21 Januari 2024: Vipaumbele vyake katika awamu hii ya pili ya maisha na utume wake ni kujenga na kudumisha umoja na ushirikiano wa Kanisa; Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili; ndani na nje ya Tanzania.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani aliyezaliwa tarehe 18 April, 1961 katika kijiji cha Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Tanzania, na kuchaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania anayetarajiwa kusimikwa rasmi kwa awamu hii ya pili hapo tarehe 21 Januari 2024, katika mahojiano maalum na Radio Vatican anazungumzia kuhusu: Tukio la kusimikwa kwake kuwa Mkuu wa KKKT; Umoja wa Wakristo Tanzania; Majadiliano ya Kiekumene nchini Tanzania pamoja na changamoto zake: Injili ya mafanikio, Chaguzi za kisiasa pamoja na mchango wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican katika kukuza na kudumisha majadiliano ya kiekumene. Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani inayounganisha mkoa wa Dar es Salaam, Pwani Unguja na Pemba, tarahe 21 Januari 2024 anasimikwa rasmi kama Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania, hii ikiwa ni awamu ya pili, baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumchagua kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania. Kwa mara ya kwanza alichaguliwa kunako mwaka 2007 na kuliongoza Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania kwa kipindi cha Miaka 8. Akapata muda wa kupumzika na kutafakari matendo ya Mungu katika maisha yake.

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania
Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania

Askofu Malasusa ana mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumkirimia utume huu mpana na anawaomba waamini na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika maisha na utume wake kwa njia ya sala sanjari na kudumisha ushirikiano na mshikamano. Ujumbe mahususi kwa watu wa Mungu nchini Tanzania ni kwamba, watambue kuwa Mwenyezi Mungu anaita watu wake, kwa wakati wake na kwa mapenzi yake; jambo muhimu ni ushirikiano, kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na bidii ili kutekeleza makusudi ya Mungu kwa wakati huu. Hii ni changamoto kwa Kanisa la Mungu nchini Tanzania kufanya kazi kwa ushirikiano, ili kuinjilisha pamoja na kumwakilisha Mungu katika maisha na utume huu. Na kwa njia ya unyenyekevu wawe tayari kumsikiliza Roho Mtakatifu, ili waweze kutenda kadiri ya mapenzi ya Mungu.

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa akiwa katika studio za Radio Vatican.
Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa akiwa katika studio za Radio Vatican.

Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema, anasimikwa rasmi kuwa Kiongozi mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dominika tarehe 21 Januari 2024 kwenye Kanisa kuu la Kiinjili la Kiluteri, Azania Front na kwamba, maandalizi yote hadi sasa yanakwenda vizuri. Kikubwa zaidi ni kwamba, watu wa Mungu wameendelea kusali ili kuombea siku hii ili iweze kuwa ni siku ya neema, baraka na Kristo Yesu ainuliwe! Vipaumbele vyake katika awamu hii ya pili ya maisha na utume wake ni kujenga na kudumisha umoja na ushirikiano wa Kanisa; Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili; ndani na nje ya Tanzania. Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa ana kaza kusema, bado nchini Tanzania kuna umati mkubwa watu hawajabahatika kusikiliza Habari Njema ikitangazwa wala kushuhudiwa sanjari na huduma ya “Diakonia.” Kwa Wakristo mchakato wa uinjilishaji ni dhamana na kazi kikubwa, kwani Wakristo wanapaswa kushirikishana tunu msingi za maisha. Huu ni wakati muafaka wa kutangaza na kushuhudia Habaro Njema ya Wokovu.

Askofu Alex Malasusa
19 January 2024, 14:32