Tafuta

Askofu Aldo Berardi, O.SS.T., Msimamizi wa Kitume wa Arabia ya Kaskazini aliadhimisha Misa huko Doha,Qatar katika kanisa la Mama Yetu wa Rozari. Askofu Aldo Berardi, O.SS.T., Msimamizi wa Kitume wa Arabia ya Kaskazini aliadhimisha Misa huko Doha,Qatar katika kanisa la Mama Yetu wa Rozari. 

Jumuiya katoliki iliadhimisha misa kama ishara ya tumani na umoja huko Doha,Qatar

Ni ishara ya matumaini na umoja kwa jumuiya ya Kikatoliki iliyoadhimishwa katika nafasi ya kwanza ya ibada ya Kikristo huko Quatar mnamo tarehe Mosi Januari 2024.Aliyathibitisha hayo Askofu Aldo Berardi, O.SS.T., Msimamizi wa Kitume wa Arabia ya Kaskazini,ambaye,alieleza mbele ya washiriki elfu 30 wa misa zote za siku hiyo,wakati akiongoza misa adhimu katika Kanisa la Mama Yetu wa Rozari huko Doha,Qatar.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ibada ya Misa Takatifu ambayo Kanisa Katoliki nchini Qatar iliadhimisha tarehe Mosi Januari 2024 ilikusudiwa kuwa ishara ya matumaini na umoja kwa jumuiya ya Kikatoliki, inayojumuisha watu wa makabila na mataifa mbalimbali, lugha na ibada mbalimbali za Kikatoliki. Haya ni maneno ya Askofu Aldo Berardi, O.SS.T., Msimamizi wa Kitume wa Arabia ya Kaskazini, ambaye, alieleza mbele ya washiriki elfu 30 wa misa zote za siku hiyo, wakati akiongoza misa adhimu katika Kanisa la Mama Yetu wa  Rozari huko Doha, Qatar, kwa mujibu wa Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides.

Kanisa la Mama Yetu wa Rozari lilijengwa 2006 huko Qatar

Kanisa lililoanzishwa mnamo 2006, la Mama yetu wa Rozari ni Kanisa la kwanza la Kikatoliki lililoidhinishwa huko Qatar kwa ombi la mabalozi waliopo nchini humo, hasa yule wa Ufaransa na kujengwa kwenye ardhi iliyotolewa na Sheikh Hamad bin Khalifa bin Hamad bin Abdullah bin Jassim bin Mohammed Al Thani ambaye ni mwanachama wa familia ya kifalme ya Al Thani Qatari. (Alikuwa Sheihki mtawala wa Qatar kuanzia 1995 hadi 2013 alipong'atuka kiti cha ufalme, akikabidhi madaraka kwa mwanawe Tamim bin Hamad Al Thani.) Kwa hiyo Kanisa hilo liliwekwa wakfu mnamo  tarehe 15 Machi 2008 na Kardinali Ivan Dias, ambaye wakati ule alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. “Ni Kanisa kubwa, karibu na uwanja mpya wa ndege,” alisema Askofu Berardi. “Liko katika 'Kiwanja cha Kidini' ambamo ndani yake kuna makanisa ya Kiprotestanti, Kihindi, Kikopti na Kiorthodox.

Pamoja na Kanisa kubwa katoliki kuna la Waorthodox,Wakopti na wa Kiinjili

Kanisa Katoliki ndilo kubwa zaidi lililowekwa katika eneo hilo la kidini na tungependa kujenga jingine  katika eneo jingine la nchi. Ijumaa inashangaza, kwani Wakatoliki wengi hufika katik misa, Waorthodox, Wakopti, Wakiinjili, na waaminikutoka makanisa ya India. Eneo hilo limeendelea pande zote. Shule za India na Ufilipino zilijengwa.” Wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya tarehe 1 Januari 2024, Padre Xavier D'Souza, Paroko wa Kanisa la Mama Yetu wa Rozari, alimshukuru Askofu Berardi kwa kuadhimisha Ekaristi hiyo ambayo ni mwanzo wa mwaka mpya wa 2024 katika kuiongoza jamii yao. Kisha Paroko huyo alimshukuru hata Waziri Mkuu, Familia nzima ya Kifalme ya Qatar na watu wa Qatar kwa wema wao wa kutoa vifaa na vibali vyote muhimu kwa ajili ya huduma, na Mamlaka ya Serikali na Polisi wa usalama.

Shukrani kwa Mamlaka ya Barhain,Qatar na Kuwait

Padre D’Souza shukrani za pekee zilitolewa kwa Mariam Nasser Al Hail, Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa Masuala ya Utumishi, ambaye ni nyenzo muhimu katika kupata vibali maalum na kutoa msaada wote muhimu kwa huduma zao hapo. Msimamizi wa Kitume aidha aliongeza kusema kuwa “Hali katika Vicariate ya Kaskazini mwa Arabia, ambayo inajumuisha Barhain, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia, inabadilika kulingana na nchi na tofauti zake, sheria, tamaduni, makabila, mielekeo ya Waislamu yenye misimamo mikali au kidogo.” Pamoja na Mwakilishi wa Kitume na Paroko, waliodhimisha misa tarehe 1 Januari 2024, miongoni mwa wengine pia kulikuwa na Padre Alber Joseph wa Shirika la Wakarmeli Waliotengwa,(OCD,) Padre Kachappilly na Padre Biju Thomas(OFMCap.), Padre Rodel Aclan, Padre Samer Hani Tawfiq Haddad, Padre Abraham Barnabas, Padre Michael Cadhit George, Padre Shaji Mathews Vazhayil, Padre Charbel Mhanna, wa Shirika la Maronite Mariamite OMM,na Padre Nirmal Vezhaparambil (OFMcap).

Misa ya Siku Kuu ya Bikira Mama wa Mungu tarehe Mosi Januari 2024 juko Doha,Qatar
08 January 2024, 16:53