Tafuta

Hali nchini Hiti inazidi kuwa mbaya Hali nchini Hiti inazidi kuwa mbaya  (AFP or licensors)

Haiti na UN,uhalifu ni mzito na Maaskofu wanasali kwa ajili ya kuachiliwa mateka

Nchini Haiti mwaka wa 2023 zaidi ya mauaji 5,000 na utekaji nyara 2,490.Tarehe 24 Januari ni siku ya maombi kwa ajili ya watawa waliotekwa nyara.Uhalifu unaofanywa na magenge yaliyopangwa,mauaji,unyanyasaji wa kingono na utekaji nyara,bado haujaadhibiwana ongezeko la 119.4% la mauaji yaliyoripotiwa 2023 ikilinganishwa na 2022.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Tarehe 24 Januari 2024 ni siku ya sala kwa ajili ya kuombea watawa  ili wakombolewe waliotekwa nyara tarehe 19 Januari 2024 na kwa ajili ya mateka wote walioshikiliwa nchini Haiti. Mwaliko wa kujikita katika sala, tafakari na kuabudu Ekaristi ulizinduliwa na askofu mkuu Max Leroy Mesidor, wa mji mkuu wa Port-au-Prince na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Haiti, na Padre  Morachel Bonhomme, Rais wa Baraza la Watawa wa Haiti, ambaye katika kulaani utekaji nyara wa watu nane (watawa 6 wa Shirika la Mtakatifu Anna, mwanamke kijana na dereva) aliwaalika waamini kushiriki katika mlolongo wa  maombi ya kudumu ya kuachiliwa kwa watu waliotekwa nyara na familia zao, katika parokia na jumuiya zote za nchi. Eneo ambalo utekaji nyara huo ulifanyika ni eneo linalozozaniwa na magenge mawili  makubwa ya  Ravine na Kijiji cha Mungu lakini hadi sasa hakuna aliyekiri kuwateka nyara watawa hao.

Wito wa CELAM

Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini na Caribbean (CELAM) lilituma barua kwa Askofu Mkuu Max Leroys Mésidor, wa Port-au-Prince na rais wa Baraza la Maaskofu la Haiti, ambapo linaonesha mshikamano wo na watu wa Haiti, na kualika Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini na Caribbean kujiunga na mlolongo huu wa maombi ili kufuatilia "mapambano ya kila siku ya amani ya kijamii na hali bora ya maisha katika nchi hiyo pendwa". "Tunaungana nanyi kuwomba watekaji nyara uhuru wa ndugu na dada hawa ambao wamejitolea maisha yao kwa manufaa ya watu wa Haiti na ambao heshima yao daima ni bora kuliko migogoro au maslahi yoyote," CELAM inasema.

Familia nyingi zikiwa barabarani zikikimbia magenge huko Solino karibu na mji wa Port au Prince,Haiti
Familia nyingi zikiwa barabarani zikikimbia magenge huko Solino karibu na mji wa Port au Prince,Haiti

Wimbi la ghasia zinazoishtua nchi hiyo ya Caribbean limezidi kuwa mbaya katika mwaka uliopita kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa tarehe 23 Januari 23 2024 na Katibu Mkuu Antonio Guterres. Ripoti hiyo inalaani kuongezeka kwa ghasia za magenge nchini Haiti, huku idadi ya mauaji ikiongezeka maradufu mwaka wa 2023, na kufikia karibu waathiriwa 5,000. Hali hiyo, hasa huko Port-au-Prince, inaelezwa kuwa mbaya na kuhatarisha maisha ya Wahaiti. Uhalifu unaofanywa na magenge yaliyopangwa, mauaji, unyanyasaji wa kingono na utekaji nyara, bado haujaadhibiwa, na ongezeko la 119.4% la mauaji yaliyoripotiwa katika 2023 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Guterres pia anaangazia ongezeko la kutisha la idadi ya utekaji nyara, ambayo iliongezeka kutoka 1,359 mnamo 2022 hadi 2,490 mnamo 2023.

24 January 2024, 15:47