Tafuta

Wagonjwa wa akili wakati mwingine wanatengwa katika nyumba za mbali na watu kwani wanaogopwa huko Ivory Coast. Wagonjwa wa akili wakati mwingine wanatengwa katika nyumba za mbali na watu kwani wanaogopwa huko Ivory Coast. 

Ivory Coast:kituo cha kimisionari cha Consalata cha afya ya akili

Nchini Ivory Coast,kama ilivyo katika bara kubwa la Afrika,ugonjwa wa akili una jambo lisiloeleweka ambalo huwaogopesha watu wa kawaida.“Inaweza kusemwa kuwa wagonjwa wa akili ni mawakala wa ulimwengu wa afya:wale ambao hakuna mtu ambaye anawakaribia, na hakuna mtu anayetaka kushughulika nao.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vijijini hawaonekani. Inaonekana hawapo. Badala yake wapo. Wamefichwa kwenye vibanda vya nyumba. Watu wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo wanaishi maisha ya kutengwa, mbali na jamii. Kwa sababu wanawaogopa. Wanachukuliwa kuwa wamepagawa na pepo wabaya au mbaya zaidi (wa kutisha) na mwelekeo usioonekana wa maisha. Nchini Ivory Coast, kama ilivyo katika bara kubwa la Afrika, ugonjwa wa akili una jambo lisiloeleweka ambalo huwaogopesha watu wa kawaida. “Inaweza kusemwa kuwa wagonjwa wa akili ni mawakala wa ulimwengu wa afya: wale ambao hakuna mtu ambaye anawakaribia, ambapo hakuna mtu anayetaka kushughulika nao.” Alisema hayo Matteo Pettinari, Mtawa wa Kiitaliano wa Wamisionari wa Consolata, anayefanya kazi huko Dianra, kaskazini mwa nchi ya Ivory Coast.

Mwandishi wetu Enrico Casale anabainisha kuwa msemo wake ni kutaka kusisitiza jinsi ambavyo afya ya akili bado haijachunguzwa katika eneo la pembezoni, kama Mtume wa watu alivyobainisha Utume ambao unawalenga wale ambao bado hawajafikiwa na tangazo la Injili. Ivory Coast ilikumbwa na mzozo mkali wa kisiasa na kijeshi kati ya mwaka 2002 na 2011 ambaoyo iliishia katika mgawanyiko wa nchi hiyo, katika sehemu mbili kwa karibu miaka kumi. Kaskazini, inayodhibitiwa na waasi, imeshuhudia kuachwa na kuoza kwa miundo ya serikali iliyopo tayari, ikiwa ni pamoja na ya kiafya. Taifa liliibuka kutoka katika mzozo huo kwa magoti. Miundombinu mingi ilikuwa haifanyi kazi tena na haitoi tena huduma. Watu wote waliathirika na kuathirika kisaikolojia na kijamii kutokana na machafuko na mapigano yaliyoitikisa nchi. Ugonjwa wa akili umeenea, lakini utunzaji wa kiafya kwa magonjwa ya kiakili ni mdogo. Nchini Ivory Coast  kuna hospitali mbili tu za umma za magonjwa ya akili na karibu madaktari thelathini wa magonjwa ya akili kwa zaidi ya wakazi milioni 26.

Akiwa amewasili Dianra mnamo mwaka wa 2011, tangu amekuwa msimamizi wa kituo cha afya cha “Joseph Allamano”, Padre Matteo ameshiriki kikamilifu, mwaka 2014, katika Umoja wa wanaume na wanawake watawa katika vituo vya afya na kazi za kijamii nchini Ivory Coast (UrssCI), uratibu wa miundo ya Kikatoliki inayofanya kazi katika ulimwengu wa dharura za afya na kijamii. Asséman Médard Koua, wakati huo akiwa mkurugenzi wa Hospitali ya magonjwa ya Akili huko Bouaké, mnamo mwaka wa 2016,aliigeukia kituo pekee cha afya cha serikali ambacho kinashughulikia afya ya akili katika eneo lote la kaskazini na ambacho kina eneo la watu milioni kumi na moja. Kwa mujibu wa Padre Pettinari alieleza kuwa: “Profesa Koua alitujia kama wanachama wa USSRCI”, na mbele ya mkutano wa wakuu zaidi ya sitini wa vituo vya afya vya Kikatoliki, alituambia kwamba afya ya umma inajitahidi kuwafuata wagonjwa hawa. Alituomba tushinde chuki na kusitasita juu ya dhiki ya kiakili na kupeleka jukumu letu na uaminifu kama watu wa imani kusaidia wagonjwa walio na magonjwa haya. Na akakhitimisha akisema: “Mkiwakataa, basi nani atawanusuru?”

Kituo cha Afya cha “Joseph Allamano” kilikubali changamoto hiyo. Kwa hivyo, mazungumzo haya ya kwanza yalifuatiwa na kikao cha mafunzo ambacho daktari wa magonjwa ya akili alifanya na timu yake katika kituo cha Kijiji cha Dianra chenyewe, kilichosimamiwa na Wamisionari wa Consolata, na kuanza kwa ushirikiano ambao pia ulihusisha Wilaya mpya ya Afya ya Dianra kupitia mkurugenzi wake. Hivyo, mpango  wa majaribio ulianza ambao ulianza kutoa baadhi ya huduma za usaidizi: “Tangu ziara ya kwanza ya Profesa Koua kwenye kituo cha afya tuliona moja kwa moja uharaka wa kutoa huduma katika eneo hili.” Kwa kuongezea alisema: Sisi wamisionari hatukuwa tumetangaza sana jambo hilo hapo awali. Tulikuwa tumetoka tu kutangaza, wakati wa misa na katika jumuiya za kimsingi, kwamba daktari aliyebobea katika afya ya akili atakuja na kwamba, ikiwa kuna mtu yeyote anayejua watu wenye matatizo ya aina hii, angeweza kuwaomba waje kwa mashauriano: watu sabini na wawili walionyesha. siku ya kwanza peke yake.”

Leo kituo cha majaribio cha Kijiji cha Dianra kinafanya kazi kwa kutumia itifaki za kisayansi na kutoa ushauri kwa wagonjwa ili kutambua kwa usahihi aina ya ugonjwa na kisha kufafanua tiba. Muundo ulizingatia patholojia tatu: kifafa, psychosis na unyogovu; matatizo yote ambayo leo yanaweza kuwekwa chini ya udhibiti na matibabu ya pharmacological ambayo yanahakikisha ubora wa maisha kwa wagonjwa. Hata hivyo, wamisionari hao hukabili tatizo kubwa la kiutamaduni. Nchini Ivory Coast, na barani Afrika kwa ujumla, watu hujitahidi kukubali ugonjwa sugu na kukatiza matibabu. “Ni jambo lililoenea sana barani Afrika alisema Padre Matteo – na kwamba  haihusu mfadhaiko wa kiakili tu. Wagonjwa huchukua dawa hizo, lakini wanapojisikia vizuri, huacha matibabu mara moja. Hii inahusishwa na sababu za kiutamaduni na pia kwa maono potofu ya imani, kwamba “Mungu lazima akuokoe kutokana na ugonjwa na kudumu kwa hiyo inaonekana kama uponyaji wa nusu na haukubaliwi.” Ili kutibu shida yam songo wa  akili ni muhimu kuingilia kati katika kiwango cha matibabu, lakini pia kiutamaduni na kiroho.

Viwango hivi lazima viendelee sambamba ikiwa tunataka kushughulikia mzizi wa tatizo na hatua kwa hatua tuendelee kuelekea utatuzi wake.” Kupitia kituo cha majaribio, wafanyakazi wa afya wanaweza kuandamana na wagonjwa kadhaa ambao hapo awali walikuwa wameachwa kando. Sasa, mmishonari anamalizia, “tunajaribu kupanua uzoefu wetu kwenye vijiji vingine vya wilaya. Katika miezi ya hivi karibuni pia tumekuwa tukitekeleza hatua ya kuongeza uelewa, tukiwataka wanaowafahamu wagonjwa wanaougua magonjwa ya akili kuwapeleka katika kituo chetu. Katika tendo hili pia tunawahusisha watu wa kidini wa imani tofauti, kama vile maimamu na wachungaji wa kiinjilisti. Ujumbe tunaotaka kuwasilisha ni kwamba unaweza kutoka katika msongo wa mawazo na kuwa na maisha ya amani.”

Wagonjwa wa misongo ya mawazo huko Ivory Coast
11 January 2024, 14:48