Tafuta

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na harakati ya kukusanya vifaa kwa ajili ya kusaidia maskini na wahitaji Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na harakati ya kukusanya vifaa kwa ajili ya kusaidia maskini na wahitaji 

Jumuiya ya Mt.Egidio:kulinda na kusaidia anayeishi barabarani

Katika kukabiliana na tatizo la baridi linaloendelea,kulinda na kusaidia anayeishi barabarabarani,ndiyo tendo maalumu la kukusanya vitu vya kujifunika kama mablanketi na vitu masweta kwa ajili ya watu wasio na makazi maalum.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Usibaki kutojali, lakini simama, kulinda na kusaidia. Katika kukabiliana  na wimbi la baridi la kwanza la majira ya baridi hii, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ilizindua wito kwa taasisi, lakini pia kwa wananchi wote. Kwa sababu kila mtu anaweza kufanya kitu ili kulinda wale walio katika hatari siku hizi, si tu kutokana na hali ya joto au  baridi zaidi, lakini kutokana na upweke. Jumuiya pia inahamasisha mkusanyo maalumu wa  blanketi, mifuko ya kulalia na vifaa vya pamba kwa watu wasio na makazi, ambavyo vitasambazwa wakati wa chakula cha jioni ambacho hutolewa kwa mwaka mzima na vinywaji na milo ya moto kwa watu wanaolala nje.

Uhamasishaji huo tayari unatumika katika miji yote ya Italia ambako Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ipo. Katika mji wa Roma, msaada unaweza kuletwa katika Chama cha Mshimamano kupitia njia ya Porto Fluviale 2 na katika vitongoji vingine (anwani na ratiba zinaweza kuonekana kwenye tovuti: www.santegidio.org. Wakati huo huo, mapokezi ya usiku yataendelea katika Jumba la Migliori (karibu na Uwanja wa Mtakatifu Pietro) - inayosimamiwa pamoja na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo,  katika Villetta della Misericordia, ndani ya hospitali ya Gemelli, katika makanisa ya Mtakatifu Calisto na Mchungaji Mwema huko Trastevere na katika maeneo mengine kwenye mji mkuu Roma.

Mshikamano ulioenea wakati wa Noeli  kwa  msaada wa watu wengi wa kujitolea, kwa chakula cha mchana na maskini kilichoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  kilihusisha watu 80,000 nchini Italia kwa hiyo inaonesha kwamba idadi ya wale wanaotaka kuchangia ujenzi wa miji yenye hadhi  zaidi inakua. Habari zaidi juu ya maeneo na nyakati (zinasasishwa) ili kuweza kusaidia, sio Roma tu bali pia katika miji mingine ya Italia. Kwa maelezo zaidi unaweza kupata taarifa kupitia tovuti yao: www.santegidio.org.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na juhudi za kuwasaidia walio wa mwisho
11 January 2024, 15:17