Kanisa la Kiorothodox nchini Ethiopia wanaadimisha Siku Kuu ya Epifania huko Addis Ababa. Kanisa la Kiorothodox nchini Ethiopia wanaadimisha Siku Kuu ya Epifania huko Addis Ababa.  (ANSA)

Timket,Kanisa la Ethiopia linaadhimisha Tokeo la Bwana ambalo kwao ni Ubatizo wa Kristo

Timket ni Epifania ya Kanisa la Kiorthodox la Ethiopia tofauti na Epifania ya Kanisa Katoliki tuliyozoea kwa ujio wa Wafalme Watatu yaani Mamajusibadala yake wao wanaadhimisha ubatizo wa Kristo.Siku Kuu hii kubwa inaangukia Januari 19-20 wakati wa mwaka.Kwa hiyo ni siku ya mapumziko kwa Waorthodox nchini Ethiopia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Timkat ni Epifania ya Kanisa la Kiorthodox la Ethiopia tofauti na Epifania ya Kanisa la Magharibi kama Italia haiadhimisha ujio wa Wafalme Watatu,  yaani Mamajusi, badala yake, wao wanaadhimisha Siku Kuu ya Ubatizo wa Kristo. Ambao unaangukia kati ya Januari 19(Januari 20 wakati wa mwaka wa kurukaruka), Timket ni siku za mapumziko makubwa zaidi ya Wakristo wa Kiorthodox nchini Ethiopia ambayo hudumu kwa siku tatu, za safari na sala na mikesha.

Maadhimisho ya Epifania ambayo kwa Kanisa la Kiorthodox Ethiopia ni Ubatizo wa Bwana
Maadhimisho ya Epifania ambayo kwa Kanisa la Kiorthodox Ethiopia ni Ubatizo wa Bwana
Mapadre wa kiorthodox wakiwa katika Bwawa la Maji
Mapadre wa kiorthodox wakiwa katika Bwawa la Maji

Ketera, Mkesha wa Timket

Usiku wa kuamkia Timket unaitwa Ketera. Wakati wa siku huo Tabot, ambayo ni mfano wa Sanduku la Agano na mbao za Sheria ambazo Musa alipokea kwenye Mlima Sinai, kutoka kwa kila kanisa hubebwa kwa maandamano kuelekea mto au bwawa la maji ambapo sherehe ya siku inayofuata inaadhimishwa mahali. Hapa kuna hema maalum ambalo kila tabot hupumzika huku washiriki wa kwaya ya kanisa wakiimba nyimbo. Hii inaambatana na ngoma maalum ya mapadre.

Masanduku katika maandamano yenye agano
Masanduku katika maandamano yenye agano
Mapadre wa kiorthodox katika sala
Mapadre wa kiorthodox katika sala

Usiku wa kabla ya Timket

Mapadre, wakiwa wamevaa mavazi ya kiutamaduni na miavuli iliyofumwa kwa uzi wa dhahabu, husali usiku kucha, huimba na kucheza kwa ngoma na ala za kienyeji, wakipeperusha chetezo ambacho hutoa harufu ya uvumba  na kuingia hewani, wakibariki maji kuzunguka mwamba wa bwawa au mto au ziwa ambapo sherehe hufanyika siku inayofuata.

Mapadre wakiwa na miavuli kwenye maandhimisho ya Timket
Mapadre wakiwa na miavuli kwenye maandhimisho ya Timket
Waamini wakiwa wanakesha katika sala
Waamini wakiwa wanakesha katika sala

Usiku kucha, maelfu ya mahujaji, wakiwemo wanawake wengi waliovalia nguo nyeupe, wanawasili kutoka  nchini kote, wakitembea kwa siku baada ya nyingine ili kushiriki katika wakati huu wa kukumbukwa, karibu kana kwamba ni msafara wa kibiblia. Saa 2:00 asubuhi siku inayofuata, misa takatifu huadhimishwa, sherehe hizo hufikia kilele alfajiri, wakati watu wanajizamisha ndani ya maji na kusali.

Wanawake wakiwa wamevalia nguo nyeupe, makundi kwenye maandamano
Wanawake wakiwa wamevalia nguo nyeupe, makundi kwenye maandamano
Waamini ni wengi katika maadhimisho haya ya kila mwaka wakikesha 19-20 Januari
Waamini ni wengi katika maadhimisho haya ya kila mwaka wakikesha 19-20 Januari
Waamini na nguo za utamaduni wakiomba
Waamini na nguo za utamaduni wakiomba

Siku ya Timket

Baada ya sala, Padre mzee hutumia msalaba wa maandamano ya dhahabu kubariki maji na kuzima mshumaa uliowekwa wakfu unaowaka ndani ya maji. Kisha wanawanyunyiza maji juu ya washiriki lililokusanyika katika ukumbusho wa ubatizo wa Kristo.

Kuhani akiwanyunyizia maji baada ya kubarikiwa na mshumaa
Kuhani akiwanyunyizia maji baada ya kubarikiwa na mshumaa
Kiongozi Mkuu akiwa na msalaba wa kuwabariki wote
Kiongozi Mkuu akiwa na msalaba wa kuwabariki wote

Sherehe ya Timket ni ukumbusho, si ubatizo wa kila mwaka. Baada ya ubatizo, Tabot za kila Kanisa, isipokuwa Kanisa la Mtakatifu Mikaeli, huanza kurudi kwenye makanisa yao. Wazee huandamana kwa heshima, wakisindikizwa na uimbaji, makuhani na vijana wanaoruka, kupigwa kwa fimbo na vijiti vya maombi kukumbusha taratibu za kale za Agano la Kale.

Sherehe kubwa katika  Bwana kwa maadhimisho 20 Januari 2024 nchini Ethiopia
Sherehe kubwa katika Bwana kwa maadhimisho 20 Januari 2024 nchini Ethiopia
Waamini wakikesha katika kusali nchini Ethiopia
Waamini wakikesha katika kusali nchini Ethiopia

Siku iliyofuata ya tarehe 20 Januari ni sikukuu ya Malaika Mkuu Mikaeli, Mtakatifu maarufu zaidi wa Ethiopia, uhaadhimishwa. Na ni asubuhi hiyo tu ambapo Tabot ya Mtakatifu Mikaeli hurudi kanisani kwake. Ndivyo inavyohitimisha sherehe ya siku tatu, muhimu sherehe ya kipekee ya Kanisa la Kiorthodox nchini  Ethiopia.

Siku Kuu kubwa huko Ethiopia
Siku Kuu kubwa huko Ethiopia
Umati ni mkubwa mno katika siku kuu ya epifania au ubatizo wa Bwana nchini Ethiopia
Umati ni mkubwa mno katika siku kuu ya epifania au ubatizo wa Bwana nchini Ethiopia

 

 

20 January 2024, 11:13