Kanisa la Huruma ya Mungu huko China. Kanisa la Huruma ya Mungu huko China. 

Makanisa mapya yashuhudia Kristo katika wilaya mpya za mjini na nje miji,China

Askofu wa Beijing alisisitiza ukweli wa kanisa jipya ambalo liko katikati ya eneo jipya la maendeleo la Beijing,eneo la kilomita za mraba 225 lililoundwa kukaribisha wakazi 290,000,wengi wao wakiwa vijana wanaofahamu zana za uunganishaji wa kidijitali,wajasiriamali,wataalamu na wafanyakazi katika taaluma za kiakili.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kanisa jipya lililowekwa wakfu kwa Mtakatifu Yohane lililozinduliwa hivi karibuni mjini Beijing linawakilisha vizuri wasiwasi ambao jumuiya za Wakatoliki wa China ambao hufanya kazi ya kutoa ushuhuda wa Yesu hata katikati ya wilaya mpya za mijini ambazo zimetokea hivi karibuni katika maeneo ya miji mikubwa. Kanisa hilo jipya liko katika eneo kubwa zaidi la maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia la Beijing, linalojulikana kama BEDA, au kama Mji wa E Beijing (Beijing Yizhuang), katika Barabara ya tano ya Kusini mwa mji mkuu wa China. Sehemu mpya ya ibada iliwekwa wakfu na kuzinduliwa na Askofu Joseph Li Shan mnamo  tarehe 30 Desemba. 2023 Katika fursa ya siku hiyo ya kuwekwa wakfu, walishikiri Mapadre 20, watawa kadhaa na walei zaidi ya 300.  Askofu wa Beijing alisisitiza ukweli kwamba kanisa jipya ambalo liko katikati ya eneo jipya la maendeleo la Beijing, eneo la kilomita za mraba 225 ambalo limeundwa kukaribisha wakaazi wa watu 290,000, wengi wao wakiwa vijana wanaofahamu zana za uunganishaji wa kidijitali,wajasiriamali, wataalamu na wafanyakazi katika taaluma za kiakili.

Mama Maria wa Sheshan msimamizi wa Nchi ya China
Mama Maria wa Sheshan msimamizi wa Nchi ya China

 

Askofu Li Shan alihimiza kila mtu kumwiga Mtakatifu Mlezi wa Kanisa hilo jipya, akiomba kuwa “mitume wapendwa wa Yesu” ili kutolea kila mtu ushuhuda wa Kristo mwenyewe, na kutumikia jumuiya nzima kwa maneno na matendo ya Injili. Askofu wa Beijing alisisitiza ukweli kwamba Kanisa jipya ambalo liko katikati ya eneo jipya la maendeleo la Beijing, eneo la kilomita za mraba 225 ambalo limeundwa kukaribisha wakaazi wa watu 290,000, wengi wao wakiwa vijana wanaofahamu zana za uunganishaji wa kidijitali, wajasiriamali, wataalamu na wafanyakazi katika taaluma za kiakili. Askofu Li Shan alihimiza kila mtu kumwiga Mtakatifu Mlezi wa Kanisa hilo jipya, huku akiomba kuwa “mitume wapendwa wa Yesu” wajitolee kila mtu ushuhuda wa Kristo mwenyewe, na kutumikia jumuiya nzima kwa maneno na matendo ya Injili.

Hapa ilikuwa wakati wa mIsa ya kubariki mafuta matakatifu
Hapa ilikuwa wakati wa mIsa ya kubariki mafuta matakatifu

Katika maadhimisho ya Mama Maria Mama wa Mungu ambapo Siku ya Amani Duniani pia inaadhimishwa, Askofu Antonio Dang Mingyan wa Jimbo la  Xi'An pia alizindua Kanisa jipya la Guanshan (lililojengwa upya katika mahali ambapo  kkuna Kanisa la kale lenye historia ndefu) katika eneo masikini zaidi la Jimbo. Mapadre thelathini na watatu, watawa ishirini na walei wengi waliotoka katika parokia na manispaa jirani walishiriki katika kuwekwa wakfu. Baadhi yao waliandamana na sherehe ya kuweka wakfu kwa kwaya na muziki uliochezwa na orchestra. Paroko pia aliwashukuru wale wote waliotoa mchango wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Bwana.

Mwanzoni mwa 2024, kwa hiyo jumuiya ya Tangshan, katika jimbo la Hebei, pia ilizindua mwaka maalum wa kichungaji uliowekwa kwa ajili ya uinjilishaji. Mapadre wa madhehebu 8 kwa pamoja walieleza mpango wa kichungaji wa kimisionari, uliotolewa wakati wa misa ya ufunguzi wa Mwaka mpya wa Uinjilishaji, wakiwaalika wabatizwa wote ‘kutembea pamoja kutangaza Injili ya Kristo.’ Walei wa jumuiya walionesha nia yao ya kushirikiana na matendo yao ya kawaida na ya kila siku katika kazi ambayo “Utatu Mtakatifu utataka kuikamilisha” katika mwaka wa Uinjilishaji. Mapadre pia wamejitolea kuonesha kwa kila mtu upeo wa utume kwa njia ya mahubiri na kazi ya ukuhani.

Kanisa la China na ushuhuda wake
10 January 2024, 16:16